Happiness Essau
Senior Member
- Aug 9, 2016
- 166
- 100
TAARIFA JUU YA TATIZO LA MAJI NDANI YA MANISPAA YA BUKOBA.
1. Ieleweke kuwa miaka yote BUWASA hakuwa na mtandao wa maji katika kata zote za manispaa ya bukoba, kata ambazo mpaka sasa ziko ktk mtandao wa maji ya BUWASA ni kata 10.5, kata 3.5 ambazo haziko ktk mtandao wa BUWASA ni *kahororo, buhembe, nyanga na 0.5kagondo* hivyo maeneo hayo kutokuwa na maji si ajabu japo ni kero.
2. Kata zinazopata shida ya mgao wa maji kwa sasa ni zile za ukanda wa juu, *kitendaguro, ijuganyondo, kibeta na rwamishenye* kwa nini? Kwa sababu ikumbukwe kulikuwa na agizo la mkuu wa nchi kwa Tanesco kuwakatia huduma ya umeme wadaiwa wote, na BUWASA ilikuwa ni moja wapo, umeme ulipokatwa awali uliathili huduma ya maji kwa manispaa nzima mpaka BUWASA walipofanya juhudi za kulipa sehemu ya deni lililosaidia huduma ya maji kupatikana kwa mjini kati, lkn Tanesco wakagoma kuwarejeshea umeme wa kuendesha mitambo kusukuma maji kwenda matanki ya kata za ukanda wa juu mpaka sasa.
Kwa nini buwasa inashindwa kulipa deni lote? Ni kwa sababu kwanza deni ni kubwa na kulikuwa na makubaliano kati ya BUWASA na serikali kuwa, kwa sababu gharama ya umeme wa kuendeshea mitambo mipya ni kubwa mno kiasi kwamba kama gharama yote itabebwa na BUWASA basi gharama ya bills za maji inaweza kuwa mara mbili ya ilivyo sasa hivyo serikali ikaahidi kuchangia gharama za umeme na BUWASA nusu kwa nusu, lkn pia kuna deni la umeme linalotakiwa kulipwa na mkandarasi wa mradi wa bunena kwa umeme alioutumia wakati wa ujenzi wa mradi ambalo linahesabika kwa BUWASA, mkandarasi yuko tiyari kulipa deni hilo atakapokuwa amekamilishiwa malipo yake ya kazi toka kwa mamlaka husika na akisha lipa deni hilo na serikali kuongeza luzuku zake basi umeme utarejeshwa na mitambo kusukuma maji bila shida yoyote, lkn pia BUWASA na wao wanazidai taasisi za serikali pesa nyingi hivyo na wao pesa nyingi iko nje kwa wadeni.
BUWASA haikukaa kimya kwa sababu inajua maji ni uhai, ilikimbia na kwenda kufufua chanzo cha maji cha kagemu kwa gharama zisizopungua mil 21 na ndicho ambacho kinasaidia kufanya mgao wa maji kwa kata za ukanda wa juu zenye kero ya maji kwa sasa.
HABARI NJEMA
Wafadhili wamekubali kupanua mradi wa usambazaji wa maji ndani ya manispaa ya bukoba, hivyo kata nufaika na mradi huo zitakuwa ni kata za *kahororo na maeneo ya kashai kisindi, buhembe, na nyanga* ambazo hazikuwa zimefikiwa na mtandao wa maji tangu awali, mkataba kati ya BUWASA na mkandarasi unafanyika ndani ya siku chache zijazo.
Hivyo kama mradi utakuwa umekamilika na tatizo la umeme kutatulika, tatizo la maji itakuwa historia ndani ya manispaa nzima ya bukoba.
Kuhusu uwezo wa mradi wa bunena ni kwamba ule mradi una nguvu ya kusukuma maji mpaka nje ya mipaka yote ya manispaa ya bukoba hivyo kinachosubiliwa ni kumalizia deni la umeme na upanuzi wa mtandao wa BUWASA kwa maeneo ambayo hayakuwa yamefikiwa tangu historia.
Binafsi na kama ofisi ya Mbunge jimbo la bukoba mjini tupende kutoa shukrani za dhati kwa mamlaka ya maji bukoba BUWASA kwa juhudi zao za kuboresha huduma za maji ndani ya manispaa yetu ya bukoba.
Tuwaombe wananchi wawe wavumilivu kwa muda wakati ambapo mipango ya kutatua kero ya maji ikiendelea kwa msukumo wa hali ya juu kupitia ofisi ya Mbunge Jimbo la Bukoba mjini.
Asanteni sana kwa baadhi ya wananchi ambao wamekuwa wakionyesha ushirikiano na ofisi ya Mbunge jimbo la Bukoba mjini kwa kutoa taarifa ya kero mbali mbali ndani ya jamii zetu, na sisi tutasimama kidete kuhakikisha tunashirikiana vyema na taasisi husika kwa kuweka msukumo na kuhakikisha huduma bora kwa jamii zinaimarika.
Asanteni sana,
BUKOBA ITAJENGWA KWA UPENDO, USHIRIKIANO NA MSHIKAMANO BAINA YETU.
Imetolewa na Ofisi ya Mbunge jimbo la Bukoba mjini.