TUSHIRIKISHANE Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Kigamboni

TUSHIRIKISHANE Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Kigamboni

Kuna Mwanakigamboni katoa maoni yake kwa Mbunge wa Kigamboni, Kasema hivi, "Mh. Dr F. Ndugulile kwanza nakupongeza kwa uchapakazi wako na bidii unazozionyesha ingawa bado kuna changamoto nyingi zinazokukabili hasa wakati huu ambao Kigamboni inaenda kuwa wilaya. Mimi nna mambo mawili matatu bado nayaona kama changamoto kubwa kwako na pia ni kero kuu kwa wakazi na wazawa wa Kigamboni;

1. Utaratibu na Muongozo kuhusu Mradi wa Mji mpya.

2. Shule ya sekondari (high school) ni aibu kwa kigamboni ya leo hakuna sekondari ya form five na six

3. Stendi mpya, hii ni kero kubwa mheshimiwa pale nyumbani ferry sio mbali na stendi hebu siku uende ukajionee hali halisi ilivyo ni aibu yaani magari ni mengi sana na stendi ndogo mno.

Ni hayo tu mheshimiwa sina mengi, ahsante "
 
Mdau mwingine kutoka Kigamboni anahoji, anasema "Hivi jamani nataka kuliza, pale ferry sehemu ya kusubiria panton kwa nini choo tuna lipia? Ile sehemu ilibidi watu wajisaidi bure. Kwanini wanatutesa tulipie tiketi bado Ukifika ndani na Choo tulipie?" Amehoji.

Katika sehemu iliyotengwa kwaajili ya kusubiria Pantoni, kuna vyoo vya Umma. Kwakuwa wakati wa kuingia pale ndania anakuwa kalipa hela ya Pantoni, anataka ukiwa Mle ndani uweze kupata huduma ya choo bure. MwanaJamiiForums unazungumziaje hili swala?

Karibu kwa hoja
 
Kuna taarifa ya Katizo la Umeme Kigamboni na baadhi ya Sehemu katika Mkoa wa Temeke. Katika moja ya Mipango ya tushirikishane ni kuhusu tatizo la Umeme. Kumekuwa na hali ya kukata umeme mara kwa mara katika jimbo la Kigamboni. Kupitia tushirikishane, mipango imeshaanza ya kujenga kituo cha Kupozea Umeme Kigamboni.
7d17c46e-f645-4651-bd33-11eeaedde8b0.jpg

nyabhingi, sifi leo, theROOM, kipapi, johnsonmgaya, Kyatsvapi, Didier, kimbangu
 
Kile kipande bwana kinaharibu shoo yote ya daraja! Yani kweli walishindwa kukimalizia? Nina imani kitawekwa lami ndani ya mradi huu wa Tushirikishane
Kile kipande wakati wa uzinduzi mwaka Jana waliahidi kitakanilika mwezi wa 12 mwaka Jana.Lakini mpaka Leo zii ni magleda tu yanafukia fukia mashimo Siku zinaenda
 
Wakuu, Kuna hii barabara inatoka Feri na kwenda kutokea Kibada, Pamoja na kwamba kuna kipande kina lami, hiyo lami yenyewe imechoka sana kwani baadhi ya Sehemu kuna Mashimo Makubwa kiasi yanaweza kusababisha ajali.
kiba15.JPG

kiba2.JPG
kiba2.JPG
kiba3.JPG
kiba4.JPG
kiba5.JPG
kiba6.JPG

kiba7.JPG

kiba8.JPG

Hapa ndipo Kisiwani ambapo Kipande cha Lami kutoka Feri kinaishia. Kuanzia hapa kwenda hadi Kibada kwenye Makutano, hakuna lami bali ni Barabara iliyomwagiwa Kifusi ambayo nayo Imeanza kuchoka
kiba10.JPG
kiba11.JPG
kiba13.JPG
kiba14.JPG

Hapa ni Kibada ambapo Hii barabara inatokea. Hii ya Mkono wa kulia ni barabara inayotokea Kongowe kwenda Feri, na hii ya kushoto ni Barabara inayopitia Kisiwani hadi darajani na Nyingine kutokea Feri.

Kwa habari zilizopo ni kwamba Tenda imeshatangazwa ya Kujenga hii Barabara. Hii barabara pia imo katika Mradi wa Tushirikishane ambao unaendeshwa na Jamii Media Ukiwahusisha wananchi na Mbunge wa Kigamboni
 
..pia hiyo njia ya kutoka kibada hadi chekeni kupitia dar zoo...na kile kiwanda cha maziwa inahiaji itengenzwe kwa kiwango cha lami tena haraka mno....kwa kuwa kuna watu wengi wana ardhi maeneo hayo lakini wamekwama kuendeleza kwasababu ya miundo mbinu mibovu ya barabara...na umeme hamna kabisa....nashangaa wakati hata NHC wana nyumba zao huko...
 
Tunaomba mtutaarifu hatma ya huu mradi wa Eco Dege Village. Mbona umesimama kwa mda mrefu sana. Kuna sababu zozote zile za kusimamishwa mradi huu??
 
Katika vipaumbele vi5 sikuona kuhusu suala la maji. Kibada mitaa na barabara zilivyo jipanga vizuri lakini unapishana na watu na ndoo za maji kichwani. Mh mbunge hivi hili hukuliona kuwa ni la muhimu,

Na washawasha!
 
Pale Kigamboni kuna viwanja vya miradi vimepimwa kama Geza Ulole, Kibada, Muongozo nk, ni wakati muafaka huduma za jamii kama barabara, Umeme na Maji vikafikishwa haraka ili maeneo hayo yaendelezwe. Inakuwa haina maana wala motivation kama maeneo ya miradi ya serikali yanakuwa sawa na squatter.

Kuna tatizo lingine sugu la kuchelewesha vibali vya ujenzi. Yaani pale Temeke Luna watu wameomba vibali vya ujenzi hawajapata kwa zaidi ya miezi sita, kila ukienda eti Baraza la Madiwani halijakaa kupitisha vibali. Sasa sijui kati ya Madiwani na Engineers nani anatakiwa kutoa kibali?? Na ukianza ujenzi utawaona manispaa hao wamefika wanakutaka u-stop ujenzi. Rushwa tupu.

Sasa unajiuliza, kwa nini ukanunue Kiwanja kilichopimwa halafu kupata kibali cha ujenzi upate usumbufu kiasi hiki?? Why not opt for squatter?? Unajenga bila kumfuata mtu. Ndio maana nasema hakuna motivation, its very discouraging
Naungana na mchangiaji theROOM. Ila ningependa kujua mpaka ya Wilaya ya Kigamboni na Temeke baada ya kuanzishwa kwa wilaya mpya ya Kigamboni. Utata unakuja kwa wakazi wa Mikwambe maeneo ya nyumba za NSSF na NHC wako wilaya gani? Ni vizuri wananchi wakaelezwa kiutawala wa napata huduma wapi mfano kupata vibali vya ujenzi.

Utata mwingine ni Mbunge Dk Ndugulile anawakilisha eneo lipi ndani ya Kigamboni na kama mipaka ilizingatia uchaguzi uliopita?

Naomba kuelimishwa na nafahamu wananchi wengine wangependa kujua.

Hongera Dk Ndugulile kuendelea kuwatumikia waliokupa kura. Changamoto ni nyingi, mfano ni kuchonga barabara kwenye viwanja vililvyopimwa ili watu wapate motivation ya kujenga. Bila miundo mbinu vifaa vya ujenzi vitafikaje? Huku ni porini.
 
Kuna Mambo Mengi ya Maendeleo yanaendelea Jimbo la Kigamboni. Je wajua Kuna vyandarua vinagawiwa bure?
View attachment 468006 View attachment 468007
Mbunge Dkt Faustine Ndugulile ambaye ni akiwa na wajumbe wa Serikali ya Mtaa ya Kibene, Vijibweni baada ya kukagua zoezi la ugawaji vyandarua.

Kwa wale waliopoteza vocha au kutosajiliwa kupewa vocha mwezi Februari mwaka huu, waende kwenye ofisi za Serikali kuanzia siku ya Jumanne na watapatiwa utaratibu wa kupata chandarua.

NB: Vyandarua vinatolewa bure
Vyandarua vya nini? sisi tunataka maendeleo mnatuambia habari ya chandarua! Mliahidi kuleta Pantoni mpya ya tatu ili kupunguza kero ya kivuko cha ferry-magogoni hadi Leo hii hamna dalili.
Mradi wa mjimpya nao kimyaa hatujui A wala Z sijui hatujui kama upo, umeaitishwa, ama nini kinaendelea mpaka sasa au ndio mnasubiri uchaguzi ndio mlete sera hizi?
 
Katika ahadi za Mbunge katika Mradi wa Tushirikishane ni Kuongeza miundombinu ya umeme na kujenga kituo kipya cha kufulia umeme Kigamboni. Hata Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mh Hashim Mgandilwa alipofanya ziara katika Ofisi za TANESCO wilaya ya Kigamboni na baada ya kutembelea Ofisi mbalimbali na kujionea hali halisi ya utendaji kazi alizungumza na uongozi na wafanyakazi wa taasisi hiyo, DC Mgandilwa pamoja na kuwapongeza wafanyakazi kwa juhudi zao za kila siku kuboresha huduma za upatikanaji wa umeme wilayani hapa, alikemea vikali mambo ambayo yanasababisha kuzorota kwa huduma hiyo mara kadhaa.

Aliwataka kuboresha mifumo ya umeme na kumaliza tatizo la kukatikakatika kwa
umeme kila mara. Pia amesisitiza utoaji wa taarifa kwa wananchi kabla ya kukata umeme pale inapowalazimu kufanya hivyo kwa sababu za msingi. Hii naona imetekelezwa kwani juzi Jumamos ya Tarehe 18 Febuary 2017, tuliona Taarifa ya kukatwa kwa Umeme kutoka TANESCO ambayo ilitolewa kwa vyombo vya habari, nadhani hii ilikuwa moja ya tija kwani zamani taarifa zilikuwa hazitolewi ulikuwa unashitukia umeme umekatwa tu bila taarifa

Mkuu wa Wilaya aliwakumbusha wafanyakazi wa TANESCO dhana ya uwajibikaji katika nafasi walizonazo ili kuwaletea wananchi maendeleo na kuwa yeye hatasita kumchukulia hatua za kinidhamu mtumishi yeyote atalayeleta uzembe na tabia zisizokubalika zenye kusababisha huduma mbovu kwa wananchi.

DC Mgandilwa aliwataka viongozi wa taasisi hiyo kutengeneza ushirikiano mzuri na viongozi wa ngazi mbalimbali ili kurahisisha kuwafikia na kuwahudumia wananchi kwa wakati na kwa ufanisi mkubwa.

Pia Mkuu wa wilaya amewataka TANESCO kuharakisha taratibu za ujenzi wa Ofisi za TANESCO wilaya ya Kigamboni zinazotarajiwa kujengwa eneo la Somangila na kusisitiza matumizi mazuri na sahihi ya pesa itakayotolewa kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi hizo.

Swala la Umeme linamgusa kila Mwanakigamboni ndio maana likaweka kwenye akadi za Tushirikishane
IMG_20160920_101006.jpg

Mkuu wa wilaya ya Kigamboni (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa TANESCO mkoa wa Temeke Eng. Jahulula M. Jahulula aliyeko kulia
 
Mh Mbunge
SHULE ZA SEKONDARI KIDETE NA KIBUGUMO ZINA TATIZO KUBWA LA KUKOSEKANA UMEME MWAKA WA KUMI SASA
SHULE ZIPO JIRANI KABISA NA MAKAO MAKUU YA SASA YA MANISPAA YA KIGAMBONI
PIA NI KILOMETERS TAKRIBANI KUMI KUTOKA IKULU YA MH. MAGUFULI

AJABU NI KWAMBA SHULE HIZI TAYARI ZILISHAUNGANISHWA NA MIUNDOMBINU YOTE YA UMEME (INSTALLATION) AMBAYO INAANZA KUHARIBIKA HASARA KWA SERIKALI

PIA NI SHULE TATU TU KATIKA MANISPAA YA KIGAMBONI ZISIZOKUWA NA UMEME

SASA JE MH. MBUNGE NI LINI TUTAPATA UMEME. PIA NI LINI UTAKUJA KUTEMBELEA SHULE HIZI ZILIZO KATIKA MAZINGIRA MAGUMU

NAOMBA KUWASILISHA
 
Moja ya ahadi za Mbunge wa Kigamboni katika tushirikishane ni Kujenga hospitali ya wilaya na kuboresha zahanati na vituo vya Afya. Katika kufanikisha hilo, Mbunge kasema Tayari kuna mpango wa Kujenga Hospitali ya Wilaya. "Tuna mpango wa kujenga hospitali ya Wilaya Kigamboni,Rangi Tatu itaboreshwa kuwa hospitali kamili. Tunatarajia kujenga hospitali ya Wilaya kwenye kata ya Somangila."

Naamini hii ni hatua moja nzuri kwa Maendeleo ya Kigamboni.
 
Kipindupindu kimeingia kwenye Wilaya ya Kigamboni. Napenda kuwakumbusha wananchi wa Kigamboni kuzingatia kanuni za afya ikiwa ni pamoja na:

1. Kutumia maji yaliyochemshwa

2. Kutumia maji ya visima vifupi kwa tahadhari

3. Kula vyakula vya moto na kuepuka vyakula vya mitaani

4. Kuchukua tahadhari katika kuhudumia mgonjwa anayeharisha

5. Kuepuka vyakula vilivyopoa kwenye mikusanyiko ya watu

6. Kutotupa taka ovyo

Halmashauri ya Wilaya ya Kigamboni imeshachukua hatua zifuatazo:
1. Imeshaandaa wodi maalum kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa wa kipindupindu

2. Kuchukua sampuli toka baadhi ya vyanzo vya maji

3. Kutibu baadhi ya vyanzo kwa kutumia klorini

4. Kufukia baadhi ya visima vifupi ambavyo vimethibitika kutokuwa salama

5. Kusimamia kanuni za afya

6. Kutoa elimu kwa umma.

Natoa rai kwa wananchi wote wa Kigamboni kuchukua tahadhari ili tuweze kudhibiti ugonjwa huu.
Naomba tusambaze taarifa kwa wana Kigamboni wengine.

Asanteni

Dkt Faustine Ndugulile Mb
Mbunge-Kigamboni
23.02.2017
 
8ec5a23f-2b09-4d1b-b2c5-3a72815a3488.jpg

24 February 2017, Mh. Faustine Ndugulie (MB) alipata nafasi ya kutembelea kiwanda cha Lake Cement kilichopo Kigamboni, baada ya kumalizika shughuli za Uzinduzi wa bweni LA wanafunzi katika shule ya sekondari Kimbiji lililo jengwa na kampuni hiyo.
 
Tishio la Kipindupindu Kigamboni, Kwa sasa wagonjwa wameanza kupatikana maeneo mengine ya Wilaya yetu ya Kigamboni, sio Kibada tu.
 
Tishio la Kipindupindu Kigamboni, Kwa sasa wagonjwa wameanza kupatikana maeneo mengine ya Wilaya yetu ya Kigamboni, sio Kibada tu.


Kwenye hiyo orodha hapo juu ulipo orodhesha sababu za kupata kipindupindu. Je mmefanya utafiti mkagundua sababu zipi zimeleta kipindupindu Kigamboni? Je ni zote au baadhi tu ya hizo? Na kumbushia swali langu #49 la mtandao wa mabomba ya maji.

Na washawasha!
 
Wafanyabiashara wa daladala, kutoka Karume Machinga Complex hadi Kigamboni, Wanalalamikia Barabara mbovu na gaharama kubwa za dalajani. Wanaomba wapunguziwe tena tozo pale darajani sababu hali hii inafanya Daladala nyingine zinazotoa usafiri kwa Umama kutokwenda Kigamboni.
 
Back
Top Bottom