TUSHIRIKISHANE Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Kigamboni

TUSHIRIKISHANE Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Kigamboni

Mbali na Daraja, Kigamboni pia ina vivuko viwili vya MV Magogoni na MV Kigamboni ambavyo kwa pamoja vinauwezo wa kubebe abiria 1000 na magari 78 kwa kila safari. Utaratibu umeshaanza wa kutengeneza kivuko kipya ambacho kipo hatua za Mwisho za utengenezwaji ili kurahisisha safari za Kwenda na kurudi Kigamboni.
kivuko1.jpg
 
Nashukuru Ndugu Nyabhingi kwa maoni yako. Kimsingi, michoro kwa ajili ya kipande kilichobaki imekamilika. Tunatarajia kazi kuanza muda wowote.

Suala la tozo pamoja na ufanisi wa huduma pale darajani ninaendelea kulifuatilia. Kumekuwa na kutupiana mpira kati ya NSSF, Wizara ya Ujenzi na SUMATRA kuhusiana na nani mhusika mkuu katika kufanya mapitio ya tozo. Naamini tutapata ufumbuzi hivi karibuni.
Ndugu mbunge hebu kumbuka hiyo ahadi hapo juu,unajua watu wanasema vibaya kuwa yule Jamaa wa ile kampuni ya mafuta pale kati amewatia mfukoni,leo ni February karibia miezi mitano sasa huo muda wowote haufiki.Please hebu fanya kweli bwana.
 
HUDUMA KTK HOSPITALI YA VIJIBWENI YALALAMIKIWA
Mkaazi wa Kigamboni amelalamikia huduma za Afya katika Hospitali ya Viibweni. Anasema;
Sijawahi kuwa na historia nzuri ya kupata huduma hospitali ya vijibweni. Kutokana na historia hiyo niseme wazi tu nina miaka zaidi ya mitatu sijaenda kupata huduma pale kutokana na ukaribu na dharura iliyompata mmoja wa wanafamilia wangu.

Nilifika hospitalini saa saba nikaenda moja kwa moja OPD. Nikiwa pale nikaelekezwa niende jengo jingine zinakotolewa huduma za NHIF. Ilipofika saa 9.30 bila kupata huduma, Dr. Was zamu akatoka akasema hatoi huduma muda wake wa kazi umeisha, twende jengo jingine. Hapo kulikuwa na wagonjwa kadhaa ambao angeweza kutumaliza na wote tulikuwa tumefika kabla ya saa 9.30. Kuna waginjwa, akiwemo wangu, walikuwa na umri zaidi ya miaka 70 na wengine hawezi kutembea vzr. Pamoja na kumuomba, Dr. Yule alikataa. Hivyo, tulitakiwa tutoke pale twende tukaanze foleni upya OPD ya kumuona dr, foleni nyingine maabara tukiungana na tuliowakuta, foleni pharmacy etc.

Nililazimika kuondoka pale nikaona ni heri nikaanze foleni mpya mahali pengine huku nikimhurumia bibi mmoja mwenye miaka zaidi ya 80 (makadirio yangu) aliyekuwa anatembea kwa msaada na kujiuliza hv kwanini dakitari huyu hakutaka kuwamaliza waginjwa waliopo waliofika kabla ya saa 9.30?

Mkurugenzi paangalie Vijibweni. Kesho nataka kuja kukueleza uzoefu wangu mbaya ya Hosp hiyo lkn ili tusijae ofisini kwako kujuletea kero, nashauri uweke/uandae utaratibu utakaotumiwa na wananchi kuleta kero zao.

Tkio limetokea Leo jumatatu tarehe 27/2/2017. Dr. Aliyekuwa sehemu ya NHIF anahusika.

Naamini hili tatizo litafanyiwa kazi na wahuhusika. Hii kero ilitolewa na Mwanakigamboni alojulikana kwa jina moja la James.
 
Kuanzia hapa hadi barabara ya lami itokayo kivukoni kwenda Kibada kupitia kisiwani ndo panalalamikiwa. Hapaa ndo mwisho wa lami itokayo daraja jipya la Kigamboni. Wananchi wanalalamikia hii barabara ya Vumbi ambayo haiendani na hadhi ya Daraja.
 

Abdul Razak Khaider Katibu wa Vijana maendeleo Wilaya ya Kigamboniakizungumzia Mradi wa tushirikishane Kigamboni amesema, ili tuendelee kusogea mbele, sisi watanzania tuna asili ya uoga kwa Viongozi wetu, Mradi huu nia kubwa ilikuwa ni kuwaweka wananchi karibu na viongozi lakini wananchi hawatumii fursa hii.

Mbunge ni mhusika mkuu, vijana wa Kigamboni hawawezeshwi. Hivyo Mbunge awaangalie kwa ukaribu. Mbunge ajaribu kushuka chini.

Maofisini na watendaji ndani ya Kigamboni bado kuna Urasimu.

Zaidi msikilize kwenye video hii
 
Muanze na namba tatu aisee mtakuwa mmetusaidia sana na hivi tunaelekea masika itakuwa balaa hiyo njia ya kibada tungi darajani.
 
Na wale Wa bandarini waweke lami eti wanamwaga sijui vifusi sijui mabaki ya lami barabara muhimu kama hivyo. Anyway mmetusaidia kidogo sasa tunaenda kwa kasi
 
Nazungumzia kero ya umeme Vijibweni. Tumeunganishiwa umeme kakini hauwaki hadi saa sits na usiku. Majibu ya TANESCO ni ya kukatisha tamaa kabisa. Tetesi za mitaani ni kutukomoa kwa sababu hatujatoa hsie kwa mafundi. Binafsi nafikiria kuchukua maamuzi magumu. Mh. Ndungulile naomba nenda TANESCO mshauriane utatuzi Wa jambo hilo kabla hatujaanza kulaumiana. Wasifikiri sie ni wajinga bwana mheshimwa.
 
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani amefanya ziara jijini Dar es Salaam ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa vituo vipya vya kupooza na kusambaza umeme vya Mbagala na Kurasini pamoja na kukagua eneo kutakapojengwa kituo cha Kupooza umeme katika eneo la Kigamboni.


Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (wa pili kulia, mstari wa mbele) akizungumza katika Kituo cha Kupooza na Kusambaza Umeme cha Mbagala jijini Dar es Salaam wakati alipofanya ziara ya kukagua vituo vya kupooza na kusambaza umeme jijini Dar es Salaam. Kushoto kwa Naibu Waziri ni Mbunge wa Mbagala, Mhe. Issa Ally Mangungu na wa kwanza kushoto Meneja wa Mradi wa Ukarabati wa Miundombinu ya Umeme jijini Dar es Salaam, Mhandisi Emmanuel Manirabona.

Baada ya ukaguzi huo Dkt. Kalemani alieleza kuridhishwa kwake na kasi ya ujenzi wa vituo hivyo. Hata hivyo aliwaagiza watendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) pamoja na mkandarasi, kuhakikisha kuwa ujenzi huo unakamilika mwishoni mwa mwezi wa Aprili mwaka huu ili wakazi wa Mbagala, Kurasini, Kigamboni na maeneo ya jirani wapate umeme wa uhakika usiokatika mara kwa mara.

Aidha aliwaagiza watendaji wa TANESCO kuhakikisha kuwa, wanaweka uzio katika eneo kutapojengwa kituo cha kupooza umeme cha Kigamboni ili lisiingiliwe na wavamizi na hivyo kukwamisha juhudi za Serikali za kupeleka umeme wa uhakika kwa wananchi.

Imeandaliwa na:

Teresia Mhagama,

Afisa Habari,

Wizara ya Nishati na Madini,

5 Barabara ya Samora Machel,

S.L.P 2000,

11474 Dar es Salaam,

Simu: +255-22-2121606/7, Nukushi: +255-22-2121606

Barua Pepe: info@mem.go.tz
 
Screenshot from 2017-03-05 17-22-26.png

Faustine Ndugulile: Leo nimeshiriki bonanza la michezo lililoandaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Hashim Mgandilwa kwa lengo la kufufua ari ya michezo na pia kutambulisha fursa mbalimbali zinazopatikana Kigamboni. Mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa DSM Paul Makonda.
 
Baraza la Madiwani Kigamboni lapitisha bajeti 2017-2018 yenye vipaumbele hivi
WhatsApp-Image-2017-02-28-at-12.02.32-660x400.jpeg

MOSHI SHABANI MALLEMA

Baraza la Madiwani Halmashauri ya Kigamboni limepitisha bajeti ya mwaka 2017-2018 yenye vipaumbele mbalimbali kwa maslahi ya wananchi wa wilaya hiyo.

Akivitaja vipaumbele hivyo Mstahiki Meya wa Halmashauri hiyo ya Kigamboni Maabadi Suleiman Hoja amesema bajeti hiyo itajikita zaidi kwenye kuongeza ukusanyaji wa mapato kutoka bilioni 2 mpaka bilioni 8, halikadhalika kuimarisha huduma za afya kwa kuongeza vifaa tiba, kupanua Zahanati, kuboresha huduma za maji, kuboresha masoko na maeneo ya wafanyabiashara, kuboresha sekta ya elimu kwa kuongeza madarasa, nyumba za walimu na kurekebisha matundu ya vyoo, pia usafi wa mazingira wilaya hiyo utakuwa moja ya vipaumbele kwenye bajeti hiyo.

Mstahiki Meya Hoja ameongeza kuwa wanataraji kupokea bilioni 49 kutoka vyanzo mbalimbali vya mapato ikiwemo ruzuku ya serikali, mapato ya ndani, wafadhili na wananchi ambapo amesisitiza kuwa ilikufikia malengo wanatakiwa watumie fursa zilizopo vizuri na kuongeza juhudi katika ukusanyaji wa mapato.
WhatsApp-Image-2017-02-28-at-12.02.05.jpeg
 
JE WAJUA HISTORIA YA KIJIJI CHA GEZAULOLE ("KIJIJI CHA WAZURURAJI")

Ndugu zangu,

Nakumbuka utotoni katika jiji la Dar es Salaam, nilishuhudia kwa macho yangu msako wa wazururaji. Ni katikati ya miaka ya 70.

Niliona jinsi mgambo wa jiji walivyokuwa wakiwadhalilisha vijana na watu wazima kwa kuwakamata, kuwafunga mashati na kuwapandisha kwenye malori tayari kwa safari za kwenda Gezaulole. Kosa lao? Walikuwa wakizurura mijini bila kazi. Hivi, anayetafuta kazi atabaki nyumbani kuisubiri, si ni lazima apige mguu kuitafuta? Nakumbuka kama mtoto nilijisikia vibaya sana kuona udhalilishaji ule uliofanywa kwa watu wazima.

Na sijui leo ukifanyika msako wa wazururaji Dar yatahitajika malori mangapi?

Na miaka ile ya sabini tulipokuwa watoto tulisikia hata nyimbo za redioni kuhimiza ‘ wazururaji’ waende kwenye vijiji vipya vilivyoandaliwa na Serikali kama makazi ya ‘ Wazururaji’. Watoto wa enzi hizo huenda tunakumbuka wimbo huu;

“ Gezaulole baba, Gezaulole mama ee,Twendeni Kibugumo na Mwanadilato kwenye makao mapya,
Gezaulole baba, Geza ulole mama eee!”

Na Kigamboni ya enzi hizo ilikuwa shamba kweli. Wengi wa waliofikishwa huko Gezaulole na vijiji vingine kule Kigamboni wakayaanza maisha mapya ya vijijini.

Kuna waliokimbia Gezaulole wakarudi tena mjini au kwenye vijiji vyao vya asili. Kuna waliobaki huko Gezaulole, wakafyeka mapori yao. Wakaanza kilimo. Wakaizoea hali mpya. Wakajenga familia zao huko.

Ajabu, leo wenye fedha ndio wanaokwenda kuyanunua kwa bei ya hadaa, maeneo ya watoto na wajukuu wa ‘ wazururaji’ wa enzi za Mwalimu. Kuna watoto na wajukuu wa ‘wazururaji’ waliobaki na vieneo vidogo. Miongoni mwao ndio hao wanaofanya shughuli za kusukuma mikokoteni na kuendesha maguta.

Maggid,
Iringa
 
Majanga tena: Tumejiandaaje kukabiliana na kipindupindu jijini Dar es Salaam?
HIVI karibuni, mtu mmoja Ramadhan Kiumbo ‘Popo’, mkazi wa Kibada wilayani Kigamboni aliripotiwa kufariki dunia na wengine 12 kulazwa hospitalini kutokana na ugonjwa wa kipindupindu.

Marehemu alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Kigamboni ya Vijibweni ambako pia wagonjwa hao wengine walikuwa wamelazwa.


Tukio hilo lilisababisha shule zote za Halmashauri ya Kigamboni kufungwa siku ya Ijumaa kwa hofu ya wanafunzi kupata maambukizi.

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa, alithibitisha kuwepo kwa ugonjwa huo ndani ya halmashauri yake na kwamba wengine walikuwa wakipatiwa matibabu.

"Ni kweli ugonjwa huu umeingia, tumechunguza na kugundua umeanzia eneo la Kichangani ambapo watu wote waliomeletwa hospitali waliupatia eneo hilo walipokwenda kwenye msiba,” alisema na kuongeza kwamba maofisa wa afya walikuwa wamechukua hatua kwa kupulizia dawa katika nyumba ili kuua vijidudu vya ugonjwa huo.

Taarifa zilizopo ni kwamba, baadhi ya maeneo jijini Dar es Salaam tayari yamekwishavamiwa na ugonjwa huo, hususan Vingunguti na Temeke.

FikraPevu inafahamu kwamba ugonjwa huo hatari na unaoua haraka kwa miaka mingi umekuwa ukishambulia sana Jiji la Dar es Salaam na kusababisha vifo vingi.

majitakaa-550x366.jpg


Hata hivyo, hofu iliyopo ni kwamba, huenda ugonjwa huo ukaleta madhara makubwa jijini humo hasa kutokana na kuwepo kwa dalili za kuanza kwa mvua za masika, ambazo kwa kiasi kikubwa husababisha maambukizi kuongezeka.

Katika miaka yote, ugonjwa huo umekuwa ukileta madhara makubwa jijini Dar es Salaam huku jitihada za kupambana nao zikiwa ndogo, achilia mbali mikakati madhubuti ya kuutokomeza.

Mazingira ya jiji hilo ni machafu, miundombinu duni huku wananchi wenyewe wakiwa hawana utamaduni wa kudumisha usafi.

FikraPevu inatambua kwamba, moja ya njia zinazochangia kuenea kwa kipindupindu ni matumizi ya maji machafu, yanaweza kuwa ya visima ama bomba, ambayo hayawekwi dawa kuua vijidudu na kama hayatachemshwa kabla ya kutumika.

Kwa kuwa miundombinu mingi, hasa ya ukusanyaji wa majitaka, ni duni jijini humo, maji machafu, hususan ya mvua, hutiririka na kujaa kwenye visima ambavyo vinatumiwa na jamii kwa shughuli mbalimbali.

Kuziba kwa mitaro, uchakavu wa miundombinu, ujenzi holela unaosababisha kuziba kwa njia za maji, pamoja na tabia isiyofaa ya baadhi ya wakazi kuzibua mabomba ya maji machafu na kuyaelekeza kwenye mitaro na makazi ya watu, ni mambo yanayosababisha vimelea vya ugonjwa wa kipindupindu (Vibro Cholerae) vinavyoishi kwenye maji yaliyochafuliwa kwa kinyesi, kusambaa na kuleta madhara.

Aidha, FikraPevu inafahamu kwamba jiji hilo lina idadi kubwa ya visima venye vimelea ambavyo vinaweza kusababisha magonjwa ya milipuko, hasa kipindupindu na homa za matumbo.

Maeneo mengi ya Dar es Salaam yanapata huduma hafifu ama kutofikiwa kabisa na maji yanayosambazwa na Kampuni ya Kusambaza Maji Dar es Salaam (Dawasco), hivyo kutegemea maji ya visima ambayo siyo safi wala salama, hasa maeneo ya Buguruni, Kigogo, Yombo, Vingunguti na kwingineko.

Maji mengi ya visima, vifupi na virefu, ambavyo wakazi wa jiji hilo wamevichimba kiholela, mara nyingi huwa hayawekwi dawa za kuua vijidudu, hali ambayo ni ya hatari.

Wakazi wengi wanaotumia maji hayo ya visima wanakiri kuwa hawajawahi kuona maji yanayoingia kwenye matanki na kuuzwa kwa wananchi yakiwekwa dawa ili kuua vimelea, tofauti na ambavyo mamlaka za maji hutakiwa kutibu maji kabla ya kuwafikia wananchi.

Ingawa maji ya visima virefu na vifupi ni muhimu katika kutatua tatizo la maji, lakini hatua stahiki zinastahili kuzingatiwa, hususan katika kuyatibu kabla ya kutumiwa, hali itakayosaidia kupunguza uwezekano wa magonjwa ya milipuko kama kipindupindu na homa za matumbo.

Mamlaka zinazohusika na huduma ya maji ni lazima kuweka utaratibu wa lazima kwa kupima ubora wa maji kila mwaka katika visima vilivyopo na kuhakikisha vipya vinachimbwa baada ya kukamilisha taratibu zote na siyo kuacha kila mmoja kuchimba na kuuza maji holela.

Inawezekana tunatatua shida ya maji kwa kuchimba visima, lakini tunaweza kuwa tunazalisha matatizo mengine makubwa, kama kipindupindu ambacho kimegharimu maisha ya wananchi wengi.

Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam pamoja na Dawasco wanapaswa kuhakikisha miundombinu ya ukusanyaji wa majitaka inaimarishwa ikiwa ni pamoja na kukarabati ile iliyopo na iliyochakaa pamoja na kuweka mingine iliyo bora.

Kinyume chake, kipindupindu kitaendelea kuvinjari jijini humo kila mwaka na kusababisha vifo visivyotarajiwa.

Chanzo cha habari: Majanga tena: Tumejiandaaje kukabiliana na kipindupindu jijini Dar es Salaam?
 
MV Magogoni imekuwa ikitoa huduma za kusafirisha abiria na Magari kati Kigamboni na ng'ambo ya Pili tangu 2008.
16939503_10155041704105409_7156719731568990769_n.jpg
17103810_10155041704230409_1650758300213541932_n.jpg
 
Kigamboni imezungukwa na Bahari, lakini bado Wananchi wake hawaitumii ipaswavyo. Moja ya sababu Miundo mbinu mibovu, Kodi zisizo na mpangilio na Uvuvi haramu.

Katika Afrika Uvuvi ni Sekta inayo tambulika na kuwaletea Waafrika manufaa. Mbali na chakula, vilevile Uvuvi ni Biashara.

Hapa chini nawawekea Mahojiano na, mtaalam wa misitu, uvuvi na utawala

Uvuvi unachangia kwa uchache dola bilioni 10 katika uchumi wa Afrika kila mwaka. Katika nchi kama Angola, Misri na Namibia, uvuvi unashika nafasi ya juu katika kuendesha uchumi.

CAPE TOWN, Sep 1 (IPS) - Uvuvi pia ni muhimu kwa usalama wa chakula. Utafiti uiochapishwa na Mpango wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Uchumi Afrika mwaka 2007 ulisema kuwa baadhi ya watu milioni 200 barani Afrika wanategemea angalau sehemu ya samaki kwa ajili ya lishe.

Lakini sambamba na hali ya wakulima wengi wa Afrika, rasilimali za uvuvi barani Afrika kwa ujumla wake zinatoa kipato tete kwa wavuvi wadogo.

Mari-Lise du Preez, mtafiti wa zamani wa misitu na uvuvi katika taasisi ya Masuala ya Kimataifa ya Afrika Kusini alizungumza na IPS kuhusu jinsi gani uvuvi unaweza kuwa nguzo ya maendeleo ya jamii.

Swali: Uvuvi una umuhimu gani katika bara la Afrika?

Jibu: Wakati hifadhi ya uvuvi imeshuka katika maeneo mengine ya dunia, kipaumbele cha juu kimeanza kutolewa kwa nchi za Afrika, kwa mfano nchi za Afrika Magharibi na Kusini. Tuna meli kubwa za uvuvi kutoka Ulaya na Asia zinazovutiwa na uvuvi katika Afrika.

Kwa upande mwingine, unakuwa na nchi ambapo matumizi ya uvuvi madogo madogo yanaleta kipato kwa maisha ya wengi. Kwa mfano katika nchi kama Angola, zaidi ya asilimia 90 ya samaki wanaovuliwa siyo wa kusafirishwa kwenda nje: wanavuliwa kwa ajili ya matumizi ya wakazi wa nchini humo.

Nilimsikia Waziri wa Uvuvi wa Angola akisema, "Kutokuwa na nyama siyo suala kubwa nchini Angola lakini kunapokuwa na uhaba wa samaki linakuwa suala la kisisa."

Hali hiyo haifanani kila mahali lakini katika nchi ambapo watu wanapata protini nyingi kutokana na samaki.

Katika upande wa maendeleo, kama ukiangalia takwimu vizuri, duniani kote kuna chini ya watu milioni moja walioajiriwa na sekta kuu ya uvuvi, lakini inakadiriwa kuwa sekta kuu ya uvuvi inaajiri watu milioni 50.

Pamoja na mjadala juu ya nani anavua samaki wengi, kuna watu wengi zaidi walioajiriwa katika sekta ndogo – hii inaonyesha mchango wa uvuvi katika maendeleo ya kiuchumi.

Ni vigumu kutoa taarifa za ujumla, lakini kwa nchi zenye ukanda wa pwani, uvuvi una jukumu kubwa.

Swali: Kumekuwepo na taarifa kutoka pande mbalimbali za bara kuhusu jinsi gani wavuvi wadogo wadogo wanabaguliwa, na makampuni makubwa ya uvuvi katika pwani ya Senegal au Somalia, au kutokana na kuwa na matatizo ya leseni kwa jumuiya ya wavuvi nchini Afrika Kusini. Nini kinatakiwa kufanyika kulinda na kupanua fursa za wavuvi wakubwa na wadogo?

Jibu: Najua nchini Afrika Kusini wamekuwa wakizungumzia kuhusu sera ya wavuvi wadogo kwa muda mrefu. Ni suala zito ambalo bado halijapatiwa ufumbuzi na ni suala la kisiasa. Watu wanaweza kuchohswa.

Hata hivyo, kuna mifano ya kuangalia, kama vile nchini Angola, kuna wavuvi wadogo wengi mno.

Mfano mmoja kuweka wavuvi katika vikundi na kuanzisha vyama vya ushirika, kama ilivyo kwa vyama vya kilimo nchini Afrika Kusini. Hii ni njia moja [ya kusaidia sekta], kwasababu ni sekta ambayo siyo rasmi na ni vigumu kujua nini kinatokea katika sekta isiyo rasmi.

Suala gumu kuhusu uvuvi ni kwamba hakuna "jambo moja kubwa linaloweza kumaliza matatizo yao yote" kwasababu una jamii zenye changamoto tofauti. Una mifumo tofauti ya uvuvi yenye changamoto tofauti, kama ilivyo kwa uvuvi wa samaki jamii ya kamba nchini Afrika Kusini. Huwezi kuulinganisha na uvuvi wa chewa, kwani wote ni aina tofauti ya samaki ambao huzaliana kwa viwango tofauti.

Swali: Je ni kwa kiasi gani uvuvi katika bara la Afrika unasimamiwa katika hali endelevu?

Jibu: Tumekutana na matatizo mengi mno katika ulimwengu wa hivi karibuni, ambayo yanahusu mifumo ya asili. Kuna ongezeko la kutambuliwa kwa matatizo haya, ikiwa na maana kuwa kama unagusa sehemu moja, siyo tu kwamba unaathiri eneo hilo tu.

Katika hali kama hiyo, kitu kama vile eneo la maji mto unakoanzia, hata misitu: inafanya mabonde ya maji kuwa na afya; hii inafanya samaki pia kuwa na afya. Kwa mfano, jumuiya inayochafua vyanzo vya maji inaathiri samaki: hawawezi kuzaliana.

Swali: Ni jinsi gani usimamiaji bora wa maji unaleta mabadiliko kwa jumuiya za wavuvi?

Jibu: Kwa mfano kama ukiangalia bahari, inavutia kuona safari ambayo tumeshaifikia. Kwanza watu walidhani ingekuwa ya kuchosha. Lakini imekuwa ni ya wazi.

Wakati watu walipokubaliana kuwa rasilimali za baharini zinaweza kumalizika, zikaja sheria, kama vile kanda maalum za kiuchumi. Wazo lilikuwa ni kulinda thamani ya uchumi.

Hata hivyo mara nyingi kuna kukosekana kwa uhusiano mkubwa kutoka kwa watu ambao wanatoa maamuzi katika ngazi ya serikali kuu na watu katika jumuiya. Jambo linalotakiwa kutiliwa maanani ni kwamba watu katika jumuiya wanapaswa kutoa maamuzi [ambayo yanaathiri hifadhi ya mazingira] kila siku; jambo ambalo serikali zinapaswa kufanya ni kushirikisha jumuiya katika kusimamia rasilimali hizi.

Jambo linalotakiwa kujulikana ni matokeo makubwa ambayo uvuvi na rasilimali maji kwa ujumla wake zinaweza kuchangia katika kuboresha maisha ya wavuvi wadogo.

Je nini mpango wa Kigamboni na Nchi kwa ujumla katika kulishughulikia hili swala la Uvuvi?
 
Tanzania kukabiliana na uvuvi haramu baharini
_91063519_01.jpg

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alisema serikali itatuma kikosi maalum cha kukabiliana na uvuvi haramu unaoendelea katika bahari ili kudhibiti na tatizo hilo ambalo limeathiri sana mazalia ya samaki na kuchangia kupungua kwa samaki baharini.

Makamu wa Rais alisema katika kuhakikisha kazi hiyo inafanyika vizuri serikali pia itatuma wataalamu wa mazingira ambao watafanya tathmini ya uharibifu wa mazingira katika bahari ili kujua uharibifu uliofanyika na kuchukua hatua ya kukabiliana na hali hiyo.

Ameeleza kuwa serikali itachukua hatua hizo ili kuinusuru bahari kwa sababu imekuwa ni chanzo kizuri cha mapato kwa wananchi kutokana na shughuli za uvuvi na shughuli nyingine zikiwemo za utalii.

"Bahari yetu ndio mapato yetu, bahari yetu ndio maisha yetu tumeitumia vibaya mapato yamepungua na maisha hayawi mazuri hivyo ni muhimu tuitunze ili iendelee kutulea kwa manufaa mazuri."
 
DC Hapi avalia njuga uvuvi haramu

allyhappy_210_120.jpg

MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi ametangaza vita dhidi ya uvuvi haramu, huku akikabidhi majina ya watu 21 yakiwemo ya viongozi wanaojihusisha na uvuvi huo kwa Jeshi la Polisi, Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni.

Aisha, Mkuu huyo wa wilaya amesimamia uteketezwaji wa zana haramu za uvuvi za thamani ya Sh milioni 60 ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa vita dhidi ya uvuvi haramu.

Hapi alitangaza vita hiyo jana akiwa katika ziara ya siku 10 ya awamu ya pili ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo katika wilaya yake ambapo alisema, uvuvi huo unahatarisha uwepo wa samaki kutokana na kutumia zana zinazoangamiza mazalia ya samaki.

Alisema wavuvi haramu wamekuwa wakivua samaki ambao hawastahili kuvuliwa na kwamba wapo baadhi ya watu wanaotumia mabomu na milipuko wanaoenda chini ya bahari na kulipua.

"Wavuvi haramu wanatumia mabomu na milipuko, wanaua mazalia ya samaki, kama tusipochukua hatua mapema, watoto na vizazi vyetu hawatakula samaki," alisema Hapi.

Hapi alisema amekabidhi majina hayo kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Suzan Kaganda ili kuyafanyia uchunguzi na ikiwa watabainika kuhusika na uvuvi huo ili wachukuliwe hatua kali za listeria.

Alisema watu wanahusika katika uvuvi haramu wana nguvu kubwa lakini Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kutokomeza uvuvi haramu.

"Hatuwezi kuvumilia hali hii kuendelea, mbali na kimaliza mazalia ya samaki lakini hata wale watalii wanaokuja kuzamia kuangalia mandhari hawatakuja," alisema.

Hapi alisema wavuvi hao haramu wamekuwa wakitumia milipuko ambayo ni hatari na endapo isipozuiliwa inaweza ikachangia kujitokeza kwa matukio ya kihalifu pamoja na ugaidi.

Aliongeza kuwa utumiaji wa zana hizo haramu una madhara mengi ikiwemo watu kupata ulemavu wa viungo vya mwili na wengine kupoteza maisha kutokana na milipuko ya mabomu.

Aliongeza kuwa kila siku milipuko 50 imekuwa ikisikika kila siku katika ukanda wa fukwe za manispaa hiyo.

Ofisa Uvuvi Wilaya ya Kinondoni, Grace Katama alisema vifaa hivyo asilimia 80 vimekamatwa maeneo ya Kawe na Kunduchi.

Alisema shughuli za ukamataji zilianza Septemba mwaka jana hadi sasa na kwamba Matukio ya milipuko yamekuwa mengi
 
MHE. DKT. FAUSTINE E. NDUGULILE aliuliza Swali Bungeni kuhusiana na Uvuvi:-

Sekta ya Uvuvi hapa Tanzania inaajiri wananchi wengi lakini wavuvi hawanufaiki kutokana na changamoto mbalimbali:-
(a) Je, Serikali ina mpango gani wa kupitia mlundikano wa leseni kwani kuna aina nyingi sana za leseni, kwa mfano, leseni ya chombo, leseni ya mvuvi, leseni ya aina ya samaki, leseni ya eneo la uvuvi na kadhalika?

(b) Je, Serikali ina mpango gani wa kuwawezesha wavuvi nyenzo za uvuvi ili waondokane na uvuvi haramu?

(c) Je, Serikali ina mpango gani wa kuanzisha viwanda vya kuongeza thamani ya mazao ya uvuvi?

MAJIBU YA WAZIRI WA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Faustine Ndugulile, Mbunge wa Kigamboni, lenye sehemu (a), (b) na (c), kama ifuatavyo:-
(a) Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nikiri kwamba ni kweli sekta ya uvuvi ina wananchi wengi wanaojihusisha na uvuvi moja kwa moja na wengine wanaojihusisha na shuguli mbalimbali za sekta hii ya uvuvi. Sekta ya Uvuvi husimamiwa na Sheria ya Uvuvi Na. 22 na Kanuni za Uvuvi za mwaka 2009. Kwa mujibu wa sheria hii, kuna leseni ya chombo, leseni ya uvuvi na leseni ya aina ya samaki.

Pia Mamlaka ya Kusimamia Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) nao hutoa cheti cha usalama wa chombo. Aidha, Jeshi la Zima Moto na Uokoaji linataka kila chombo cha uvuvi kiwe na chombo cha kuzimia moto (fire extinguisher). Pia Mamlaka za Mtaa (Serikali za Mitaa) nazo zimetunga sheria ndogo ndogo kuhusiana na masuala ya uvuvi kama njia mojawapo ya kuongeza mapato katika maeneo yao. Hata hivyo, kwa sasa Serikali inapitia upya leseni na tozo zenye kero kwa wananchi ili kuona uwezekano wa kuzipunguza au kuzifuta ili kuwanufaisha wavuvi. (Makofi)

(b) Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imekuwa ikitoa elimu mara kwa mara kwa wavuvi juu ya athari zitokanazo na uvuvi haramu hususani kwa kutumia mabomu, sumu na zana zisizoruhusiwa kisheria. Aidha, Serikali imefuta Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwenye injini za kupachika (outboard engines), nyuzi za kushonea nyavu (twines), nyavu za uvuvi na vifungashio ili kupunguza gharama za zana na vyombo vya uvuvi.

Serikali inaendelea kuhamasisha sekta binafsi kuwekeza katika ujenzi wa viwanda vya nyavu na zana za uvuvi ambapo hadi sasa viwanda viwili vya kutengeneza nyavu vya Imara Fishnet (Dar es Salaam) na Fanaka Fishnet (Mwanza) na viwanda vinne vya kutengeneza boti za kisasa vya Yutch Club, Sam and Anzai Company Limited, Seahorse Company Limited vya Dar es Salaam na Pasiansi Songoro Marine (Mwanza) vimekwishajengwa.

Vilevile Serikali imeanzisha utaratibu wa kuwawezesha wavuvi wadogo wadogo ambapo jumla ya shilingi milioni 400 zilitolewa kama ruzuku ya zana za uvuvi na Serikali ilichangia asilimia 40 na mvuvi alichangia asilimia 60 na kupitia utaratibu huu injini za boti 73,000 zilinunuliwa.

(c) Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inaendelea kuhamasisha sekta binafsi kuanzisha viwanda vya kusindika samaki na mazao ya uvuvi ili kuyaongezea thamani mazao hayo. Jumla ya maghala 84 ya kuhifadhi mazao ya uvuvi na viwanda 48 vya kuchakata mazao ya uvuvi vimejengwa.

Viwanda hivyo vipo katika maeneo yafuatayo: Ukanda wa Pwani kuna viwanda 36; Ziwa Victoria kuna viwanda 11 na Ziwa Tanganyika kuna kiwanda kimoja. Pia Serikali imeendelea kutoa elimu kuhusu njia bora za uchakataji na uhifadhi wa samaki na mazao yake kwa viwanda na maghala hayo ili kulinda soko la ndani na nje ya nchi.
 
MHE. MARIAM N. KISANGI (k.n.y MHE. DKT. FAUSTINE E. NDUGULILE) aliuliza kuhusu TAFICO:-

Hapo zamani kulikuwa na Shirika la Uvuvi la TAFICO lenye Makao Makuu yake Kigamboni ambalo lilikufa kutokana na uendeshaji mbovu:-
(a) Je, Serikali ina mpango gani wa kufufua shirika hilo?

(b) Je, Serikali imejipanga vipi kusimamia deep fishing ili iweze kunufaika na mapato yatokanayo na uvuvi?

MAJIBU YA NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA (K.n.y. WAZIRI WA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI): Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Faustine Ndugulile, Mbunge wa Kigamboni lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Naibu Spika, Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO) lilianzishwa mwaka 1974, lengo likiwa ni kuendesha shuguli za uvuvi kibiashara. Aidha, mwaka 1996 TAFICO iliwekwa chini ya iliyokuwa Tume ya Rais ya Kurekebisha Mashirika ya Umma (PSRC) kwa ajili ya utaratibu wa ubinafsishaji. Mwaka 2005 TAFICO iliondolewa kwenye orodha ya Mashirika yaliyotakiwa kubinafsishwa na kurejeshwa Wizarani kuendeleza ubinafsishaji wake. Hata hivyo, mwaka 2007 Baraza la Mawaziri lilisitisha uuzwaji wa TAFICO na kuelekeza kuwa mali zisizohamishika ikiwemo ardhi zibaki kwa ajili ya matumizi ya Serikali.

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara kwa kushirikiana na wadau wengine inaendela na mpango wa kufufua Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO), ikiwa ni pamoja na kuwasilisha mapendekezo ya Baraza la Mawaziri kwa hatua husika.

(b) Mheshimwia Naibu Spika, ili kusimamia mapato yatokanayo na uvuvi katika ukanda wa uchumi wa bahari, Serikali zetu mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa pamoja zilianzisha Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi wa Bahari Kuu (Deep Sea Fishing Authority) kupitia Sheria ya Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi wa Bahari Kuu Na. 1 ya mwaka 1998 na marekebisho ya mwaka 2007. Taasisi hii ina jukumu la kusimamia uvuvi katika eneo la Uchumi la Bahari Kuu, ikiwemo utoaji wa leseni kwa meli za kigeni na za ndani zinazovua kwenye ukanda huo.

Aidha, mamlaka inaendelea kufanya doria za anga na kuhuisha mfumo wa kufuatilia meli, kufuatilia vyombo vya uvuvi baharini (Vessel Monitoring System) ili taasisi iweze kudhibiti wanaovua bila kulipa leseni. Pia Serikali inaendelea na taratibu za kuwezesha ujenzi wa bandari ya uvuvi ambayo itawezesha meli za kigeni zinazovua bahari kuu kutia nanga hapa nchini na hivyo kuongeza ajira na kipato kwa Watanzania pamoja na Pato la Taifa kwa ujumla.
 
MDAU ALIA NA UVUVI HARAMU KIGAMBONI
image001.jpg

Ukikaa Kijiji Beach ama Chadibwa Beach kuanzia muda wa asubuhi mpaka mchana milio ya mshindo kutoka baharini ni kitu cha kawaida kwa mara ya kwanza utashtuka baadaye utazoea kwani hawa jamaa wanafanya bila kuogopa na ni mfululizo.

Kwa wakazi wa Kigamboni jambo hili kwa sasa limekuwa kawaida kwani ukitembelea fukwe za kuanzia Chadibwa Beach na Kijiji Beach ambayo ni Kilometa 3 tuu kutoka Kigamboni Ferry hadi South Beach ambayo ni takribani 7 Kilometa kila baada ya nusu saa hadi dakika 45 utasikia mlio mshindo ukitokea maeneo ya baharini na kama macho yako yakiwahi utaona maji yakiruka juu kama picha inavyoonyesha, si kingine ni wavuvi wa kutumia baruti.

Kinachosikitisha zaidi hawa jamaa hawaogopi kupiga baruti zao, ikumbukwe kuwa ni takribani nusu kilomita kutoka Kambi ya jeshi ambayo iko pembezoni mwa Mikadi Beach. na si mbali kutoka ufukweni wanakuwa mahali ambapo hata ukimuita mtu anakusikia.

Tumeambiwa kuwa uvuvi huu mbali tuu kuua samaki na mazalia yao pia unaua viumbe vingine vya baharini.

Polisi wanawajua na taarifa wanazo kwani hata wakipigiwa simu wanaishia kusema tunakuja na hakuna kinachotokea, Mmiliki wa Kijiji Beach alijitahidi sana kutoa taarifa bila mafanikio na hakuna hatua zozote zilizochukuliwa mpaka sasa amekata tamaa. Inakera sana, tunaomba wahusika walivalie njuga na kulifanyia kazi suala hili.

Mdau Pius.
 
Back
Top Bottom