TUSHIRIKISHANE Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Kigamboni

TUSHIRIKISHANE Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Kigamboni

Athari za uvuvi wa mabomu Tanzania
140904124633_marine_life_624x351_bbc_nocredit.jpg


Tanzania inasifika sana kwa mazingira yake ya bahari ambayo imeiweka kwenye ramani
''Uvuvi wa mabomu unaharibu mazingira ya chini ya bahari ambayo huwezesha samaki kuzaana na hiyo imetuathiri sana sisi tunaovua kwa kutumia nyavu kuvua -idadi ya samaki imepungua sana,sio kama hapo awali''.

Anasema mvuvi mmoja ambaye aliomba jina lake kubanwa,huku akijiandaa kuingia baharini kuvua pamoja na wenzake.

''Tunawaripoti kwa polisi wale wanaotumia mabomu lakini wanapokamatwa wanatoa hongo na kuachiliwa na wanapogundua tumewaripoti wanaweza kuandana chombo chetu na kuturushia vilipuzi, wanatishia kufanya hivyo na ndio sababu wakati mwingine tunaogopa kusema''anasema

Kwa miaka minane mvuvi huyo amekuwa akitegemea maji ya Bahari Hindi ambayo yana utajiri wa maelfu ya samaki aina mbalimbali. Bahari hindi hukumbatia Tanzania kwa umbali wa maelfu ya kilomita. Kila siku boti za uvuvi huelea juu ya bahari hiyo. Lakini sasa uvuvi wa kutumia vilipuzi unatishia kuangamiza raslimali hiyo muhimu. Baadhi ya wavuvi hutumia vilipuzi hivyo ili kuweza kuvua samaki wengi.

Kulingana na shirika la Smart Fish, ambalo linashirikiana na serikali kukabiliana na tatizo hilo, Tanzania ndiyo nchi pekee barani Afrika ambapo uvuvi huo haramu unafanyika kwa kiwango kikubwa. Uvuvi huo hufanyika katika maeneo mengi ya pwani kuanzia Dar es Slaam,Mtwara hadi Tanga, visiwani, na kumekuwepo ripoti za mabomu kutumiwa katika bahari ya Kaskazini mwa Zanzibar.

'Maji yanayolipuka'

140904122835__77360596_img_9345.jpg


Wavuvi ambao hutumia nyavu kuvua wanalalamika kuwa Samaki wamekuwa wachache baharini
Kulingana na Baraka Mngulwi, ambaye ni Naibu Mkurugenzi wa uhifadhi wa raslimali za uvuvi nchini Tanzania, vilipuzi hivyo hupatikana kwa njia haramu kutoka maeneo ya uchimbaji madini, utengezaji barabara na wakati mwingine watu huvitengeneza nyumbani.

Kulingana na Mngulwi, watu wamekuwa wajanja kiasi cha kuyatengeneza mabomu hayo nyumbani kwa kutumia kemikali fulani ambazo zina uwezo wa kulipuka.

Vilipuzi hivyo huwashwa moto na kurushwa ndani ya bahari. Mlipuko ambao hutokea huwashtua na kuwaua samaki na hapo wavuvi hutumia nyavu kuwavua.

140904125010__77360594_img_9062.jpg


Baadhi wanasema wanapowaripoti wanaotumia mabomu kuvua huandamwa
Wataalam wanasema mlipuko mmoja unatosha kuua samaki na viumbe vyote hai vilivyo umbali wa mraba mita 20-na kuua Samaki wapatao 400 kwa wakati mmoja. Matokeo yake ni uharibifu mkubwa wa mazingira ya chini ya bahari ambayo huwezesha Samaki kuzaana.

Vilipuzi hivyo ni hatari sio tu kwa mazingira ya chini ya bahari lakini pia kwa wavuvi huku ajali zikitokea mara kwa mara. Mwanya Sleiman 40 amewahi kutumia mabomu hayo kuvua. Anasema '' mwanzoni nilikua na mikono yangu miwili, baadaye ikawa bomu nililokuwa nikiandaa ili kuvua likanilipukia mikononi sasa nikawa muathirika.

140904124333_athari_za_fish_blasting_624x351_bbc_nocredit.jpg


Mwanya Sleiman ni mwathiriwa wa ajali zinazotokana na mabomu yanayotumiwa kuvua Samaki
''Nilikua napenda tu kwamba ule mchezo ulikua unaninogea na niliweza kulipua na kupata Samaki na kisha kuwauza lakini sikujua kuhusu athari ambayo ingetokea kwangu mwenyewe au hata kwa mazingira ya chini ya bahari, sikuwa na ufahamu huo,'' asema Sleiman kwa majuto.

Kwa sasa yeye hushiriki katika mpango wa kuhamasisha jamii kuhusu athari za uvuvi wa mabomu ambao unaungwa mkono na serikali.

140904130457_matumbao_kavu_624x351_bbc_nocredit.jpg


Image captionSehemu ambapo Samaki huvuliwa kwa mabomu husalia pakavu
Filamu ya mazingira ya chini ya maji ambayo nilionyeshwa katika idara ya uvuvi inaonyesha bayana kiwango cha uharibifu. Inaonyesha Mandhari ya kupendeza na maji safi ya bahari huku Samaki aina mbalimbali wakiogelea. Baada ya kulipuliwa matumbao hayo na maeneo ambayo Samaki hutaga mayai yanaonekana kama mji uliolipuliwa kwa roketi- na hakuna ishara yoyote ya uhai.

Uharibufu huo husababisha upungufu wa samaki baharini na unapotokea hakuna njia yoyote ya kurekebisha.

Uvuvi wa mabomu ni haramu nchini Tanzania na wanaopatikana wakitumia mbinu hiyo hufungwa miaka 5 na miezi 12 kwa kupatikana na vilipuzi. Katika kipindi cha miezi 24 iliyopita shirika la Smart Fish linasema limeweza kuisadia serikali kukamata kili 300 za vilipuzi, vyombo vitano vya uvuvi kuzuiliwa na watu watano kufunguliwa mashtaka.

'Biashara imenoga'

140904122843__77360721_arrestedfishermenwithexplosivesandscubagear_whichisusedsoscoopupdeadfishtoodeeptocapturefreediving.jpg


Washukiwa wa uvuvi wa mabomu wanapokamatwa wao hutoa hongo na kuachiliwa
Mlipuko mmoja unammuwezesha mvuvi kuvua hadi kilo 400 za samaki hiyo ikiwa ni faida ya $1,800 sokoni. Ni faida kubwa lakini ya muda mfupi ikilinganishwa na uharibifu unaofuata.

Soko kuu la samaki Jijini Dar es salaam linapakana na Bahari Hindi kwa upande mmoja .Kila asubuhi wavuvi huleta samaki huku wakisubiriwa na mamia ya wanunuzi. Pindi tu wavuvi wanapowasili madalali huanza kunadi samaki, kufumba na kufumbua samaki wote wananunuliwa.
140904122845__77369038_fishmarketdaressalaam.jpg

Haki miliki ya pichaBBC WORLD SERVICE
Image captionWanunuzi wa Samaki huwa na wakati mgumu kutambua Samaki waliovuliwa kwa mabomu na nyavu

Hakuna muda wa kuchunguza njia zilizotumika kuvua samaki hao. Bala Gomwa 41,Mmoja wa madalali ananiambia kwamba sio watu wengi wanaoweza kutambua samaki waliovuliwa kwa kutumia mabomu.

140904122837__77360598_img_9116.jpg

Haki miliki ya pichaBBC WORLD SERVICE
Image captionWanunuzi sokoni huwa ni wengi ishara ya biashara nzuri ila ni wachache wanaotambua Samaki waliovuliwa kwa mabomu
''Sio rahisi kutambua Samaki aliyevuliwa kwa mabomu hasa kama hauana uzoefu. Kati ya madalali 60 unaweza kupata kwamba labda wawili au watatu ndio wanaoweza kutambua.'' Anasema.

Mama mmoja muuzaji ananifahamisha kwamba anaweza kuwatambua '' Wanakuwa na magamba mengi sana na wanaoza haraka ''

'Changamoto'

Sio rahisi kuwakamata wavuvi wanaotumia mfumo huo haramu wa uvuvi kama nilivyogundua nilipoandamana na maafisa wanaoshika doria baharini. Wanaoendesha shughuli hiyo wamo katika mtandao wa kisiri,wenye mpangilio wa juu na ambao umekuwa ukiendelea kwa miongo mingi.

Ripoti ya shirika la Sea Sense ambalo huhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kuhifadhi viumbe wa baharini inazungumzia ugumu ambao huwakabili maafisa wanaoshika doria bahariki katika vita dhidi ya uvuvi wa mabomu huku baadhi yao wakikiri kutishwa na wavuvi au wafadhili ya shuguli zao.

Ripoti hiyo inatoa mfano wa afisa mmoja ambaye alimwagiwa kemikali usoni na kusababisha apoteze uwezo wa kuona.

Wataalam wanaonya kwamba iwapo uvuvi wa kutumia mabomu hautasitishwa, hatimaye Tanzania huenda ikasalia na bahari isiyo na viumbe hai.
 
Uvuvi Haramu

KWA kipindi cha zaidi ya mwaka mmoja, Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET) kimekuwa kikifanya uchunguzi kuhusu kuongezeka kwa uvuvi haramu wa kutumia baruti katika mwambao wa bahari ya Hindi.

Uchunguzi huo uliohusisha waandishi wa habari za uchunguzi wa JET uliwawezesha kutembelea vituo kadhaa vya uvuvi katika mwambao huo kuanzia Pangani, Tanga mjini, Kilwa hadi Mtwara.

Katika uchunguzi huo, jopo la waandishi wa JET liliweza kuzungumza na kuwahoji wadau mbalimbali wa sekta ya uvuvi; kuanzia kwa wavuvi wenyewe, wananchi wa kawaida, viongozi wa serikali, polisi, wafanyakazi wa idara ya mahakama, NGOs na wadau wengine wengi.

Picha ya jumla iliyopatikana kutokana na uchunguzi huo katika vituo hivyo mbalimbali vya uvuvi huko Pangani, Tanga mjini, Kilwa na Mtwara, inafanana; nayo ni kwamba uvuvi huo unaongezeka kwa kasi kwa sababu mbili kubwa.

Sababu ya kwanza ni usaliti unaofanywa na viongozi na wanasiasa. Kote ambako JET ilitembelea ilisimuliwa, kwa mfano, jinsi doria za kupambana na wavuvi haramu wanaotumia baruti zilivyosimamishwa wakati wa uchaguzi mkuu wa rais na wabunge wa mwaka 1995, 2000, 2005 na hata uchaguzi wa mwaka juzi 2010.

Katika chaguzi zote hizo, maofisa uvuvi wa sehemu husika walipewa maelekezo kutoka “ngazi za juu” kwamba doria zisimamishwe wakati wa kipindi cha kampeni ili chama tawala (CCM) kisinyimwe kura kwenye vijiji vya wavuvi.

Haikuwa rahisi kwa JET kufahamu nani hasa kutoka “ngazi za juu” aliyekuwa akitoa maagizo hayo; kwani mara zote yalikuwa ni maagizo ya mdomo tu na si ya barua rasmi (maandishi).

Wakati watumishi serikalini walikuwa wakizungumzia suala hilo kwa sharti kuwa majina yao yasitajwe ili wasije kuadhibiwa na wakubwa wao, viongozi wa NGOs na jumuiya za kiraia pamoja na viongozi wa baadhi ya vijiji, walikuwa tayari kuelezea waziwazi hisia zao juu ya jambo hilo.

“Viongozi ngazi za vijiji wana nia ya dhati kukomesha uvuvi haramu, lakini tatizo lipo ngazi za juu kuanzia kwenye halmashauri. Huwezi kuamini, lakini wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu doria zinapunguzwa kwa sababu ya maelekezo kutoka juu,” anasema Thecla Myovela ambaye ni ofisa wa WWF.

Ofisa huyo aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa JET, hivi karibuni, mjini Mtwara ambako walijionea tatizo hilo lilivyokithiri katika mwambao wa Mtwara na juhudi zinazofanyika kupambana nalo.

Kauli kama hiyo ilipata pia kutolewa na aliyekuwa ofisa uvuvi katika Manispaa ya Tanga, Aneny Nyirenda wakati waandishi wa JET walipozungumza naye, mjini Tanga, Novemba 2005.

Madai ya wadau hawa kwamba kuna usaliti unaofanywa na wanasiasa wa kutoa maagizo ya kupunguza doria wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu, yanathibitishwa pia na takwimu zilizopatikana. Takwimu hizo zinaonyesha kwamba kote – Tanga, Kilwa hadi Mtwara, idadi ya milipuko baharini ilikuwa kubwa katika kipindi cha kampeni za uchaguzi mkuu.

Tatizo jingine kubwa linalochangia kuongezeka kwa uvuvi haramu wa kutumia baruti katika pwani ya Tanzania, ni sheria dhaifu ya uvuvi isiyotoa adhabu kali kwa wanaotiwa hatiani; lakini pia ni usimamizi legelege wa sheria hiyo dhaifu.

Hilo ni moja ya mambo yaliyolalamikiwa sana na wadau wa sekta ya uvuvi wanaoendesha mapambano dhidi ya uvuvi wakati wa ziara hizo za JET ikiwemo ya majuzi mkoani Mtwara.

“Sheria si kali. Haitoi adhabu kali kwa wanaotiwa hatiani. Mtu anakamatwa, anapelekwa mahakamani, anatiwa hatiani; lakini hupigwa faini ndogo mno. Analipa na kurejea kijijini mwake kuendelea tena na uvuvi huo huo,” anasema ofisa mmoja wa uvuvi katika Manispaa ya Mtwara ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini.

“Faini ndogo wanazopigwa mahakamani (mfano Sh. 20,000) zimewafanya wasiingiwe na hofu yoyote. Hawajali; kwani hata kama watakamatwa, watalipa faini na kuachiwa huru,” anasema Nassoro Mijai ambaye ni mvuvi katika pwani ya Mtwara.

Jambo la kushangaza ni kwamba sheria inayolalamikiwa na wadau hao wa sekta ya uvuvi hairuhusu adhabu ya faini kwa wanaotiwa hatiani. Sheria hiyo ya mwaka 2005 inasema kuwa mvuvi haramu anayetumia baruti, anayetiwa hatiani atahukumiwa kifungo si chini ya miaka mitano na si zaidi ya miaka 10.

Ni vipi sasa baadhi ya mahakama zitoe adhabu za faini au vifungo vya chini ya miaka mitano; ilhali sheria haisemi hivyo? Hali hiyo inathibitisha ulegelege uliopo katika kusimamia sheria hiyo ya uvuvi.

Sheria hii ya mwaka 2003, ambayo adhabu ya juu kabisa ni kifungo cha miaka 10 jela, imelalamikiwa na wadau wengi. Wengi wanataka adhabu ya juu iwe hata miaka 30 kama ilivyo kwa makosa ya ujambazi.

Japo serikali iliahidi kuwa itaifanyia sheria hiyo marekebisho, hakuna marekebisho ambayo yamefanyika mpaka sasa.

Redfred Ngowo, ambaye ni Kaimu Mhifadhi Mfawidhi katika Hifadhi ya Bahari ya Ghuba ya Mnazi na Maingiliano ya Mto Ruvuma, ni mmoja wa wadau wa sekta ya uvuvi anayekerwa na ulegelege wa usimamiaji wa Sheria ya Uvuvi ya Tanzania.

Akizungumza na ujumbe wa JET, hivi karibuni, mjini Mtwara, Ngowo alitoa mfano wa Sheria ya Uvuvi nchini Msumbiji ambayo ni kali mno; kiasi cha kuwafanya wavuvi haramu waiache shughuli hiyo nchini mwao na kukimbilia Tanzania kuendelea nayo.

“Nchini Msumbiji kosa la kuhusika na uvuvi wa baruti ni kifo. Ukikutwa umelipua baruti baharini, wewe ni risasi tu. Hii imewatia woga mkubwa wavuvi haramu wa huko, na ndio maana wanakimbilia upande wetu,” anasema Ngowo.

Ngowe hasemi moja kwa moja kwamba Tanzania nayo iwe na sheria ya kuwapiga risasi wanaokutwa wakilipua baruti baharini; bali anasisitiza kwamba sheria ya sasa ni dhaifu, na inahitaji kuimarishwa.

Malalamiko ya ulegelege wa Sheria ya Uvuvi ya Tanzania pia yalitolewa na wadau wa sekta hiyo mkoani Tanga, mwaka jana, wakati ujumbe wa JET ulipofanya ziara ya uchunguzi huko.

Wadau hao waliisifu sheria ya nchi jirani ya Kenya kwamba ni kali, na kwamba ndiyo sababu wavuvi haramu wa huko hukimbilia kuufanya uharamia huo katika eneo la bahari la upande wa Tanzania (mkoani Tanga).

Ni kwa sababu gani Serikali ya Tanzania imekubali kuachwa nyuma na Kenya na Msumbiji katika suala hilo la sheria ya uvuvi, ni jambo lisiloeleweka wazi; lakini kama ilivyoelezwa mwanzo, ahadi za kuirekebisha zimetolewa muda mrefu ila tu utekelezaji ndio hauonekani.

Ukiachilia mbali usaliti wa wanasiasa na ulegelege wa usimamiaji wa Sheria ya Uvuvi, kuna sababu nyingine kadhaa zinazochangia pia kuongezeka kwa uvuvi haramu wa kutumia baruti katika mwambao wa Tanzania ambao, kila mwaka, huangamiza maelfu ya tani za samaki wachanga na kuharibu kabisa mazalia ya samaki.

Hizo ni pamoja na ufahamu duni wa wavuvi kuhusu athari za muda mrefu za uvuvi huo, zana hafifu za kuvulia zinazowafanya wakimbilie kwenye uvuvi huo haramu, ukosefu wa fedha za kutosha kuendesha doria, upatikanaji kirahisi wa baruti (tnt) zinazotumiwa kwenye uvuvi huo, pamoja na kukithiri kwa rushwa katika ngazi mbalimbali zinazohusika na sekta ya uvuvi.

Hata hivyo, pamoja na matatizo yote hayo, JET inaweza kuthibitisha kwamba kuna maeneo mafanikio yamepatikana; hasa pale ambapo serikali imeungana kwa dhati na NGOs kuendesha mapambano ya pamoja dhidi ya uvuvi huo haramu.

Mfano mzuri ambapo ushirikiano wa namna hiyo umesaidia kudhibiti kidogo wimbi la uvuvi haramu ni mkoani Mtwara ambako Manispaa ya Mtwara imeshirikiana na WWF (Ofisi ya Mtwara) na Hifadhi ya Bahari ya Ghuba ya Mnazi na Maingilio ya Mto Ruvuma, kuendesha vita ya pamoja dhidi ya uvuvi huo.

“Zamani kwa siku moja kulikuwa na wastani wa milipuko kumi baharini, lakini kwa sababu ya doria hizi za pamoja sasa kwa siku wastani ni milipuko miwili tu au usitokee kabisa,” anasema Ofisa Uvuvi Msaidizi wa Manispaa ya Mtwara, Jesse Mlaki.

Athari kubwa ya uvuvi wa kutumia baruti ni kwamba si tu unaharibu maeneo ya mazalia ya samaki, lakini pia huua samaki wachanga. Mambo hayo mawili yamechangia mno kupunguza idadi ya samaki katika pwani ya Tanzania.

Nassoro Mitai, ambaye kwa miaka 20 amefanya shughuli za uvuvi na uchuuzi wa samaki mkoani Mtwara, ni shuhuda mzuri wa hoja hiyo ya kupungua kwa idadi ya samaki baharini.

Anasema hivi: “Zamani mvuvi aliweza kuvua kati ya kilo 50 na 60 za samaki kwa siku, lakini siku hizi akipata kilo 15 anashukuru Mungu. Na kwa sababu ya uchache huo, bei ya samaki sasa haishikiki”.

Kwa sababu ya uchache huo wa samaki baharini ambao unachangiwa kwa kiasi kikubwa na uvuvi usio endelevu, bei ya samaki katika masoko ya samaki nchini imepaa mno katika kipindi cha miaka sita iliyopita.

Na hiyo maana yake ni kwamba iwapo vita hii dhidi ya uvuvi usio endelevu (hususan wa kutumia baruti) haitahitimishwa haraka na kwa mafanikio, samaki watazidi kupungua katika pwani ya Tanzania, na hao wachache watakaokuwa wakipatikana bei yake itakuwa haishikiki.

Ni muhimu, hivyo basi, si tu kuongeza mapambano dhidi ya uvuvi huo haramu, lakini pia kuwatafutia wavuvi shughuli mbadala ili kupunguza msongo wa matumizi ya rasilimali za bahari.

Na katika hilo, kuna asasi mbili mkoani Mtwara ambazo zimeifanya kazi hiyo vizuri mno kama ambavyo ujumbe wa JET ulivyojionea katika ziara yake ya hivi karibuni huko Mtwara.

Asasi hizo ni WWF (ofisi ya Mtwara) ambayo kwa miaka minne imekuwa ikiendesha mradi unaoitwa “Maendeleo ya Jamii na Matumizi Endelevu ya Raslimali za Bahari”. Asasi nyingine ni Marine Park – Hifadhi ya Bahari ya Ghuba ya Mnazi na Maingiliano ya Mto Ruvuma.

WWF (Tanzania), kupitia mradi huo unaogharimiwa na WWF (Denmark), imewasaidia wavuvi wengi wa Mtwara kupunguza safari za kuvua samaki baharini kwa kuwawezesha kufanya shughuli nyingine mbadala za kujiongezea kipato.

Shughuli hizo mbadala ni pamoja na kufuga nyuki, kuanzisha bustani za mboga, ufugaji ng’ombe na shughuli nyinginezo kama hizo. WWF (Mtwara) pia iliwezesha kuanzishwa kwa vikundi vya Benki za Kijamii maarufu kama VICOBA (community banking) kwa ajili ya kutoa mikopo midogo midogo kwa wavuvi hao ili wafungue miradi hiyo mbadala.

Si hivyo tu; kwani WWF Mtwara imesaidia pia kuanzishwa kwa Chama cha Ushirika wa Wavuvi Mtwara ambacho mpaka sasa kina wanachama (wavuvi) 1, 200. Kupitia chama hicho, wavuvi hupewa elimu kuhusu madhara ya uvuvi haramu na pia husaidiwa kuelewa vifungu mbalimbali vya sheria ya uvuvi.

“Chama hiki, miongoni mwa mambo mengine, kinawasaidia wavuvi kujua haki zao, kujua mipaka yao na pia kujua sheria ya uvuvi inasema nini,” anasema Thecla.

Kwa upande wake, Hifadhi ya Bahari ya Ghuba ya Mnazi na Maingiliano ya Mto Ruvuma nayo imewasaidia wavuvi kuwa na shughuli mbadala kwa kuwafundisha ufugaji wa ng’ombe, ufugaji wa samaki na kuku ili wasiende baharini kila siku kuvua samaki ambao ni wachache.

Hata hivyo, uanzishwaji wa hifadhi hiyo, kama ilivyokuwa kwa mradi wa WWF, nao ulitokana kwa kiasi kikubwa na fedha za wafadhili (UNDP). Swali la kujiuliza ni je; mambo hayo mema iliyowaanzishia wavuvi wa Mtwara yatadumu wakati ufadhili huo utakapokoma?

Vyovyote vile; serikali inapaswa kuongeza ushirikiano wake na wadau wote katika sekta ya uvuvi ili mapambano dhidi ya uvuvi wa kutumia baruti yapambe moto kote katika pwani ya Tanzania.

Na hii ni kama bado serikali inataka kitoweo cha samaki kiendelee kuwepo mezani wakati wa maakuli kwenye nyumba za Watanzania wengi nchini; maana, kwa hali ilivyo sasa, kitoweo hicho kimeanza kutoweka kwa kasi mezani wakati wa chakula.

Chanzo: RAIA MWEMA
 
Wavuvi wanahitaji leseni moja kwa shughuli za uvuvi na sio leseni kwa kila nahodha, baharia, aina ya samaki na eneo la nchi-Dkt Ndugulile
 
Dkt Ndugulile: Kigamboni inakuwa kwa kasi. Mahitaji ni 20MW. Umeme uliopo ni 8MW. Ujenzi wa line toka Kurasini unaendelea. Bajeti ya Substation ipo 2016/17
 
Mbunge wa Kigamboni Dkt Faustine Ndugulile akiongea na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa baada ya kukamilisha ziara yake ya kutembelea Kigamboni. Waziri Mkuu alizindua wodi ya wazazi katika Zahanati ya Kisarawe ii iliyojengwa kwa ufadhili wa kampuni ya mafuta ya Oilcom.
C1Tbz1bWQAAQLdm.jpg
 
IMG_4310.JPG

Kivuko cha MV Magogoni na MV Kigamboni vikipishana kuvusha abiria kutoka na kuingia Kigamboni

Wavuvi wakiwa katika heka heka za uvuvi eneo la soko la samaki feli jijini Dar es Salaam

Wavuvi wakiandaa samaki ambao wamewavua kwa ajili ya mnada katika soko la samaki la wavuvi la Feli jijini Dar es salaam japo pamoja na serikali kuwajengea soko ila bado wanafanya shughuli zao nje ya soko hilo na katika mazingira machafu jambo ambalo ni hatari kwa afya za walaji
 
Daraja la kisasa la Kigamboni linalounganisha eneo la Kigambonina upande wa Kurasini likikatisha bahari ya Hindi.
1.jpg
3.jpg
4.jpg
6.jpg
5.jpg

hqdefault.jpg
kiga 3.jpg

Hapa ni Sehemu ya kulipia tozo kwa Magari yanayoenda na Kutoka Kigamboni
 
Suala la usalama halipo katika mipango yako, nadhani halikuwa pia sehemu ya ahadi za mbunge lakini ni emerging issue ambayo nadhani inastahili kupewa nafasi katika utekelezaji!
Kigamboni si sehemu salama sana hasa kwa kuwa ukuaji wake umekuwa kwa kasi sana kuliko speed ya ukuaji wa huduma za jamii ikiwemo upanuzi wa vituo vya polisi na uwepo wa miundo mbinu bora kwa ajili ya doria. lakini ukubwa wa eneo lisilo na wakazi hasa maeneo ya kata ya Pemba mnazi inayopakana na mkuranga na mipaka ya Temeke maeneo ya Mikwambe na Mbagala kuu/kijichi ambayo pia hutumiwa na waharifu kuingia au kutoka ktk Jimbo lako! Uwepo wa majengo mengi yasiyokwisha, viwanja ambavyo havijalimwa katikati ya makazi ya watu na ongezeko la wageni hasa mafundi ujenzi na walinzi wa majengo yasiyo na wakazi yaeongeza ugumu katika kuboresha ulinzi miongoni mwa raia. Maoni yangu katika kudhibiti uhalifu hasa huu wa ndani ni kama ifuatavyo:-
  1. Viongozi wa mitaa na wananchi wakusaidie katika kusimamia na kutambua majengo yote yasiyo na wakazi na waamuru wenye majengo hayo kuhakikisha yanakuwa salama kwa kufungwa/kudhibiti matumizi mabaya au kama wataweka walinzi basi watambulishwe rasmi kwa viongozi wa maeneo husika.
  2. wananchi wenye maeneo yasiyoendelezwa kwa muda mrefu wakasafishe maeneo yao au ile sheria ya uendelezwaji viwanja ndani ya miaka mitatu itumike kama sehemu ya kuwalazimisha wamiliki wafanye uendelezaji hata kama ukiwa ni ule wa kusafisha eneo tu.
  3. Askari wa doria waongezwe, Kigamboni kuna askari wengi wa barabarani (Traffic Police) mchana kuliko idadi ya doria wakati wa usiku! sioni shida kubwa ya usalama kwa watumiaji wa vyombo vya moto na watumiaji wa barabara kwa kigamboni kiasi cha kuwa na idadi kubwa ya traffic mchana, instead usiku ambapo majanga ni mengi, kuna gari za patrol chache sana! Hamasisha kuwepo hata na spots maalum za camp za police mida ya usiku labda Kisarawe 2, Mikwambe/NSSF na Gezaulole endapo maeneo haya yakiwa na walinzi standby kila siku usiku labda tunaweza kuokoa maisha ya wakazi wa kibada.
  4. Itisha /omba uitishwe mkutano wa pamoja wa askari wa upelelezi na wakuu wa vituo vikubwa vya polisi ktk majimbo ya Mbagala, Mkuranga, Kigamboni na Temeke ili muweze kujadili juu ya ushirikiano katika kuhakikisha usalama wa maeneo yenu!
  5. Kwa wananchi wa Kigamboni
    • Mlinzi namba moja wa mali na maisha yako ni wewe mwenyewe, hivyo tuimarishe ulinzi kwenye nyumba zetu, tushirikiane na majirani zetu na tutoe ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama ili tuweze kuifanya kazi hii kwa ufanisi!
Point hapa ni kuwa hayo maendeleo yote yatakuwa na tija kama Kigamboni iko salama, kwa hiyo usalama ni suala la kwanza kabla ya chochote!
 
Wavuvi wa samaki katika soko la kimataifa la feri Jijini Dar es salaam wameiomba serikali kuangalia namna ya utaratibu wa uuzaji wa samaki kwa njia ya mnada ufutwe ili waanze kuuza kwa kilo na kujipatia faida. Hayo wamebanishwa wakati wakizungumza na Habari extra ambapo wamesema kuwa uuzaji wa mnada kwao unawapa hasara kubwa kwani kila siku bei inabadilika bila kufuata utaratibu wowote.

Wavuvi hao wamesema kuwa soko la feri ni soko linalobeba samaki kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi hivyo utaratibu wa mnada unawaumiza sana wavuvi wa hapa nchini katika kupangiana bei na wachuuzi kutoka nje ya nchi.
 
Katika huu Mradi wa Tushirikine katika Mipango ya Maendeleo Kigamboni, ahadi namba moja ambayo wananchi walikubaliana na Mbunge kutekeleza ilikuwa ni Kukarabati vivuko vilivyopo pamoja na kupata kivuko kipya. Hadi sasa Vivoko vyote vinafanya kazi vizuri na Kivuko kipya ni kama Kimekamilika naweza kusema. Hii ni ahadi Mbunge aloitoa katika Mradi wa Tushirikishane ambayo imetimia naweza kusema hivyo. Aliahidi kuhakikisha kivuko kipya kinaongezwa.

========

ZIARA YA PROFESA MAKAME MBARAWA KWENYE KIVUKO KIPYA CHA MV KAZI KITAKACHOTOA HUDUMA KATI YA MAGOGONI NA KIGAMBONI

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mh.Profesa Makame Mbarawa akikagua mojawapo ya injini ya kivuko cha MV KAZI wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kivuko hicho. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Kampuni ya MS Songoro Marine Boatyard na Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu. Kivuko hiki kitakapokamilika kitatoa huduma kati ya Magogoni na Kigamboni.

Muonekano wa kivuko kipya cha MV KAZI kinachotengenezwa na Kampuni ya MS Songoro Marine Boatyard kikiwa katika hatua za mwisho kukamilika wakati wa ziara ya Mh.Profesa Makame Mbarawa katika eneo la ujenzi wa kivuko hicho bandarini Dar es Salaam. Kivuko hiki kitakapokamilika kitatoa huduma kati ya Magogoni na Kigamboni.

Mkurugenzi wa kampuni ya MS Songoro Marine Boatyard Major Songoro akimuonyesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mh.Profesa Makame Mbarawa alama za kuendeshea kivuko kipya cha MV KAZI kitakachotoa huduma kati ya Magogoni na Kigamboni. Nyuma yake ni Dkt. Mussa Mgwatu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mh.Profesa Makame Mbarawa akiwasili katika kivuko cha MV KAZI kukagua maendeleo ya ujenzi wa kivuko hicho, kushoto kwake ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu na nyuma yao ni Mkurugenzi wa Ukodishaji Mitambo na Huduma za Vivuko TEMESA Mhandisi Japhet Maselle.

Kivuko hiki kitakapokamilika kitatoa huduma kati ya Magogoni na Kigamboni.

mbarawa(4).jpg

Waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amefanya ziara bandari ya Dar es Salaam kukagua ujenzi wa kivuko kipya cha MV Kazi na kuutaka uongozi wa wakala wa ufundi na umeme nchini (TEMESA) kushiriki kikamilifu shughuli za matengenezo ya vivuko vya serikali ili kupata ujuzi kwa sababu wao ndio wenye dhamana ya vivuko hivyo na hivyo serikali haitakuwa tayari kutafuta watalaamu wa nje kwa ajili ya matengenezo wakati wao wapo.

Akizungumza na bandarini hapo mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kivuko hicho ,waziri Prof. Makame Mbarawa amesema kuwa kupitia ujenzi wa vivuko hivyo serikali itaweza kuokoa fedha nyingi ambazo kwa sasa inatumia kulipa kampuni binafsi zinazojenga na kukarabati vivuko.

Kwa upande wake mtendaji mkuu wa wakala huo Dkt. Musa Mgwatu, amemtaka mkandarasi wa kampuni ya Songoro Marine transport kuhakikisha anafanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha kivuko hicho kwa muda uliopangwa.

Meneja mradi wa kampuni ya Songoro Marine Transport, Bw. Major Songoro amemhakikishia waziri Mbarawa kumaliza kivuko hicho kwa wakati ambapo amesema ifikapo tarehe 15 mwezi huu kivuko hicho kitakabidhiwa kwa serikali.
 
Kipaombele no 3 kimenigusa sana, hii barabara ya toka darajani hadi kibada stendi iwe ya kiwango cha lami, tusimane pamoja wana kigamboni tujiletee maendeleo yetu.
 
Afya: JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI LAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI KWA KUTEMBELEA KITUO CHA PEDDEREF SOBER HOUSE KIGAMBONI
ZINA-1.jpg

Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jennifer Shirima ambaye aliambatana na msemaji wa Jeshi hilo katika ziara hiyo akiwasisistizia wanawake hao kutoajiingiza tena kwenye utumiaji wa madawa ya kulevya na kuwakumbusha kuwa “Wanawake ni msingi wa mabadiliko kiuchumi” (kulia) ni Mkurugenzi wa kituo hicho bi. Nuru Salehe na (kushoto) ni Mrakibu Msaidizi Puyo Nzalayaimisi ambaye pia ni msemaji wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
ZINA-2.jpg

Moja ya wanawake waathirika wa madawa ya kulevya bi.Jacqueline Samson aliyesimama (katikati) akitoa shukrani kwa viongozi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ambao hawapo picha kwa kuwatembelea kituoni hapo pia kwa msaada waliowapatia.
ZINA.jpg

Maafisa na Askari (Wanawake) wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na Mkurugenzi wa People With Drugs Dependence Relief Foundation (Pedderef)bi. Nuru Salehe wa kwanza mbele (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na wanawake waliopata kuathirika na madawa ya kulevya kituoni hapo, ambapo wanawake hao wameanza kurejea katika hali zao za kawaida mara baada ya kupewa elimu na malezi yanayostahili.

Katika kuadhimisha siku ya wanawake Duniani Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limeungana na wanawake duniani kuadhimisha siku hiyo

Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ambaye pia ni msemaji wa Jeshi hilo Puyo Nzalayaimisi alisema katika kuunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya tano (5) kupiga vita dhidi ya madawa ya kulevya, kupitia Jeshi hilo Nzalayaimisi aliwaongoza Askari (wanawake) kutembelea kituo cha Pedderef Sober House na kutoa msaada wa mahitaji mbalimbali.

Ambapo aliiomba jamii isiwanyanyapae pamoja na elimu wanayoendelea kuipata kituoni hapo ameiasa jamii kujitokeza kuwasaidia na kuwawezesha kwa hali na mali ili waweze kujiajili wenyewe kwani wanapotoka kituoni hapo wanakuwa hawana uwezo wakujiajili na kujikuta wanarudia tena kwenye janga la madawa hayo.

Pia Nzalayaimisi aliendelea kusema kwa kutoa pongezi kwa serikali na wadau mbalimbali wote waliojitokeza na kuthubutu kufanya maamuzi ya kujitoa katika kupambana na janga hilo na pia alimpongeza mkuu wa mkoa wa dar es salaam paul makonda kwa kuongoza mapambano hayo.

Mkurugenzi wa kituo hicho bi. Nuru Salehe naye alisema napenda kutoa shukrani za kipekee kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa msaada wao wa hali na mali waliotupatia na kuomba taasisi nyingi na wadau mbalimbali kujitokeza katika kusaidia kituo hiki kwani wengi wamenufaika kutokana na elimu na malezi wanayoendelea kuyapata kituoni hapo.
 
Mradi wa Tushirikishane (JamiiForums yazindua rasmi mradi wa "Tushirikishane") umeanza rasmi jimbo la Kigamboni chini ya Uongozi wa Mheshimiwa Dr. Faustine Engelbert Ndugulile Dr F. Ndugulile

View attachment 427363
Washiriki wa Warsha ya Tushirikishane Kigamboni katika picha ya pamoja na timu ya Jamii Media baada ya kumalizika kwa warsha ya siku tatu ya mradi huo.
Tokana na misingi ya TUSHIRIKISHANE iliyoelemea katika kuwawezesha wabunge wa kuchaguliwa kutekeleza ahadi zisizopungua 4 kati ya jumla ya ahadi walizotoa wakati wa uchaguzi kwa urahisi kwa kushirikiana na wananchi; mada hii itatumika kuwasilisha, kujadili na kupeana taarifa ya kile kinachojiri Kigamboni.

Katika Warsha ya Kigamboni, Mh. Ndugulile alikubaliana na jumla ya ahadi 5 zilizokubaliwa na wananchi ndani ya mradi huu.

View attachment 427362
Mbunge wa Jimbo la Kigamboni Mh. Faustine Ndugulile (Kushoto) na Mwanzilishi mwenza na mmoja wa Wakurugenzi wa Jamii Media Mike Mushi (Kulia) baada ya kusaini makubaliano ya kushiriki katika utekelezaji wa Mradi wa Tushirikishane.


TUSHIRIKISHANE – AHADI ZA MBUNGE
KIGAMBONI

1. Kukarabati vivuko vilivyopo pamoja na kupata kivuko kipya.

2. Kuongeza miundombinu ya umeme na kujenga kituo kipya cha kufulia umeme Kigamboni.

3. Ujenzi wa barabara ya Darajani- Kibada- Mjimwema kwa kiwango cha lami.

4. Kukomesha uvuvi haramu, kuwawezesha wavuvi kwa kuwapa nyenzo za kufanya uvuvi wa kina kirefu (Deep sea fishing) na kupunguza utitiri wa leseni kwa wavuvi.

5. Kujenga hospitali ya wilaya na kuboresha zahanati na vituo vya Afya.


Mada hii itatumika zaidi na Wana Kigamboni kutupa taarifa.


Baadhi ya Washiriki watakuwa:-

1. Mh. Mbunge Dr. Faustine Ndugulile Dr F. Ndugulile
2. Afisa habari Kigamboni, Vedasto Prosper Dustan Vedasto Prosper

Na washiriki wote wa Warsha hiyo na wale wote wenye mapenzi ya Maendeleo ya Kigamboni.

Karibuni.

[HASHTAG]#Tushirikishane[/HASHTAG] [HASHTAG]#Kigamboni[/HASHTAG]

Kufahamu majimbo mengine yenye mradi huu tembelea - JamiiForums yazindua rasmi mradi wa "Tushirikishane"

========

Akaunti za mradi wa Tushirikishane katika mitandao ya Kijamii:

Tushirikishane (@tushirikishane) • Instagram photos and videos

Tushirikishane | Facebook

Tushirikishane (@tushirikishane) | Twitter





Mimi nataka kuweka kiwanda sijui kunamaendeleo gani kuhusu vile viwanja iliyotaja mheshimiwa makonda .
 
Moja ya ahadi za Mbunge katika mradi wa tushirikishane ni Kukomesha uvuvi haramu, kuwawezesha wavuvi kwa kuwapa nyenzo za kufanya uvuvi wa kina kirefu (Deep sea fishing) na kupunguza utitiri wa leseni kwa wavuvi.

Wavuvi wa Kigamboni moja ya kero yao kubwa ni kutokuwa na uhakika wa ajira yao, wanaomba Mbunge na Serikali, iwasaidie wawe na Ajira za Uhakika, Waajiriwe kama Sekita nyingine wanavyoajiri pia wapewe Mikataba ya ajira.
wavuvi.JPG
 
Moja ya ahadi za Mbunge katika mradi wa tushirikishane ni Kukomesha uvuvi haramu, kuwawezesha wavuvi kwa kuwapa nyenzo za kufanya uvuvi wa kina kirefu (Deep sea fishing) na kupunguza utitiri wa leseni kwa wavuvi.

Wavuvi wa Kigamboni wanlalamikia kutokuwa na Soko la uhakika wanapotoka kuvua Samaki. Bei inabadilika badilika, Wanaomba Mbunge na Serikai iwasaidie wawe wanauza Samaki kwa Kilo kutokana na aina ya Samaki badala ya kuuza kwa Mnada . Sababu kubwa ni kwamba Soko wanalotumia ni soko la Kimataifa la Feri ambapo wanakuja wafanyabiasha wa kimataifa na kuuza Samaki wao kwa Kilo tofauti na Wavuvi wa Kigamboni.
wavuvi3.JPG
 
Wavuvi wa Dar es Salaam Kigamboni wanataka wanapokata Leseni basi iweze kutumika Tanzania nzima. Sasa hivi ukikata leseni ukiwa dar es salaam inatumika hapo hapo dar es salaam.

Ukienda nje ya Dar es salaam, Mfano uende Bagamoyo, nao wanataka wakukatie Leseni yao. Hii ni moja ya Kero ya Wavuvi wa Kigamboni
DSCN8875.JPG
 
Wavuvi wa Kigamboni wanaomba Mbunge na Serikali iwasaidie kuwawekea mfumo mzuri ili waweze kujiunga na Mifuko ya Pensheni. Kwani sasa hawana mfumo sahihi wa ajira hivyo kuwakosesha kujiunga na Mifuko hii ya Hifadhi ya Jamii.
Pg-4.jpg

Hifadhi ya Jamii ni mfumo ambao jamii husika ujiwekea kwa lengo la kujikinga dhidi ya majanga yasiyotarajiwa. Majanga hayo ni kama Maradhi, Ulemavu, Kupoteza kazi, Kuacha kazi kwa sababu ya uzee (kustaafu).

Sera ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii

Nchini Tanzania mfumo wa Hifadhi ya Jamii umegawanyika katika nguzo kuu tatu (3), ambazo ni:
Nguzo ya kwanza - Nguzo hii inahusisha Hifadhi ya Jamii katika mfumo wa huduma za kijamii zinazogharamiwa kwa kodi ya Serikali, mashirika ya wahisani wa ndani na nje na taasisi za kijamii

Nguzo ya pili - Katika nguzo hii, Hifadhi ya Jamii inahusisha uchangiaji wa lazima wa wenye kipato na walio katika ajiriwa. Hii ndio nguzo ambayo Mifuko ya Hifadhi ya Jamii inahusika. Uchangiaji katika mifuko hiyo ugharamiwa kwa pamoja kati ya Waajiri pamoja na Wafanyakazi.
Nguzo ya tatu - Hifadhi ya Jamii katika nguzo hii hutolewa kwa mfumo uchangiaji wa hiari ambao unawalenga zaidi watu wenye kipato cha ziada na huchangia kama ziada baada ya kutekeleza majukumu ya kisheria kwenye nguzo ya pili.

Mfuko wa Pensheni

Mfuko wa pensheni ni uwekezaji wa mali unaolenga kuzalishaji na ukuaji wa uchumi imara kwa muda mrefu, na kutoa pensheni kwa wafanyakazi pindi watakapofika ukomo wa kufanya kazi na kuanza maisha ya kustaafu.

Mifuko ya Pensheni Nchini Tanzania

Tanzania bara kuna Mifuko ya pension ya lazima mitano nayo ni;
Mfuko wa kustaafu wa GEPF
Mfuko wa Pensheni wa LAPF
Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF)
Mfuko wa Pensheni wa PPF
Mfuko wa Pensheni wa PSPF

Kwa ujumla Mfuko hii yote usajili na kusimamiwa Mamlaka ya Usimamizi na udhibiti wa sekta ya hifadhi ya jamii
Umuhimu wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.

Kuongeza wigo wa Hifadhi ya Jamii (Social Security Coverage)

Kupunguza umasikini kwa Watanzania

Kuongeza kinga kwa Watanzania katika Nyanja kama vile elimu, afya, uzazi, ulemavu na uzee.

Kuongeza uwekezaji na kutoa fursa kwa Wajasiriamali kupitia vikundi mbalimbali vya kijamii

Kuchangia maendeleo ya miradi mbalimbali ya Serikali

Kuongeza ajira kwa Watanzania kupitia miradi inayoendeshwa na Mifuko hiyo

Mafao yanayotolewa
Kuna aina mbili za mafao yatolewayo na mifuko ya hifadhi za jamii Tanzania; mafao ya muda mrefu na muda mfupi
Mafao ya Muda Mrefu
• Pensheni ya Uzeeni - kustaafu
• Pensheni ya Ulemavu
• Pensheni ya Urithi (kifo)

Mafao ya Muda mfupi
• Uzazi – kwa baadhi ya mifuko
• Kuumia kazini – kwa baadhi ya mifuko
• Afya – kwa baadhi ya mifuko
• Msaada wa mazishi
• Elimu – mfuko mmoja

Uhusika wa sekta isiyo rasmi kwenye Mifuko ya hifadhi ya Jamii
Sekta isiyo rasmi inahusika katika Mifuko isiyo rasmi kwa kujiunga kwenye mfumo wa huchangiaji wa hiyari unaratibiwa na Mifuko ya pensheni.lakini pia sheria inawapa uhuru wa kuanzisha mifuko ya hiari kwenye sehemu au makundi yao ya kazi na kuisaji kwa mamlaka.

Uhuru wa kuchagua mfuko wa kujiunga

Kwa mujibu wa kifungu cha 30 cha Sheria ya SSRA, kila mwajiriwa mpya ana haki ya kuchagua Mfuko ni mfuko upi ajiunge nao tena ni kosa la kisheria muajiri au mtu yoyote kumchagulia mwanachama mpya mfuko upi ajiunge nao.
 
Wavuvi wa Kigamboni wanataka Serikali na mbunge iwasaidie katika Mambo ya Usalama. Waendapo kuvua baharini katikati wanakuwa hawa vifaa vya Usalama kama Maboya, hivyo ajali inapotokea watu hupoteza Maisha. Wengine hugombania vitu ambavyo havizami kama Madumu ya Mafuta.

Hivyo wameomba Kabla ya kusajili boti au chombo chochote cha kuvulia Samaki, Serikali ihakikishe inavyo vifaa vya Usalama vinavyotakiwa. Pia wameomba Ukaguzi wa Mara kwa Mara wa Vifaa vya Usalama ufanyike na ambaye atakuwa hana vifaa vya Usalama, Wachukuliwe hatua.
download (3).jpg
download (2).jpg
fire-extinguishers1.jpg
images (2).jpg
budget_life_jacket.jpg

img_0824.jpg

water-sports-safety-equipment-sport-myopia-eyewear.jpg
 
Picha: Kivuko kipya cha kuvusha abiria Kigamboni chaingizwa kwenye maji
1.jpg

Kivuko cha MV KAZI kikielea majini baada ya kushushwa kwa mara ya kwanza tayari kwa kufanyiwa ukaguzi wa mwisho kabla ya kuanza kazi. Kivuko hicho kitakua kikitoa huduma zake kati ya Magogoni na Kigamboni na kitakua na uwezo wa kubeba abiria 800 na magari 22 kwa wakati mmoja.
2.jpg

Muonekano wa kivuko kipya cha MV KAZI mara baada ya kushushwa majini kwa mara ya kwanza tayari kwa kufanyiwa ukaguzi wa mwisho kabla ya kuanza kazi, kivuko hicho kitatoa huduma zake kati ya Magogoni na Kigamboni na kitakua na uwezo wa kubeba abiria 800 na magari 22.
3.jpg

Kivuko cha MV KAZI kikisubiri kushushwa kwa mara ya kwanza majini kufanyiwa ukaguzi wa mwisho, kivuko hicho kitakua kikitoa huduma zake kati ya Magogoni na Kigamboni na kitakua na uwezo wa kubeba abiria 800 na magari 22.
4.jpg

Kivuko cha MV KAZI mara baada ya kushushwa majini kwa mara ya kwanza tayari kwa kufanyiwa ukaguzi wa mwisho kabla ya kuanza kazi, kivuko hicho kitatoa huduma zake kati ya Magogoni na Kigamboni na kitakua na uwezo wa kubeba abiria 800 na magari 22.
5.jpg

Mkurugenzi wa kampuni ya MS Songoro Marine Boatyard ya jijini Mwanza Major Songoro mwenye kofia akiwa kwenye kivuko cha MV KAZI mara baada ya kukishusha majini kwa mara ya kwanza tayari kwa ukaguzi wa mwisho. Kivuko hicho chenye uwezo wa kubeba abiria 800 na magari 22 kitakua kikitoa huduma zake kati ya Magogoni na Kigamboni.
 
Back
Top Bottom