TUSHIRIKISHANE Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Kigamboni

TUSHIRIKISHANE Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Kigamboni

Kuna juhudi zinaendelea za kutaka kukarabati barabara za Kisota kwa ushirikiano kati ya wakazi wa Kisota ba Halmashauri.
Kama ni mkazi wa eneo na hauko kwenye mtandao wa wakazi wa Kisota. Ni-inbox jina na namba yako ili uweze kuunganishwa na kupata taarifa ya kinachoendelea.
Mkuu nmefurahi unatoa majibu..naomba utusaidie na hii njia ya dege kimbiji angalau lami isogee kule pamelala kwa sababu ya ubovu wa barabara,tumepima viwanja ila haviuziki kwa sababu ya ubovu wa Barbara..mngejitahidi angalau basis barabara ifike puna, yani kule pesa zipo ila tumezikalia tu,na kama mmeamua kuanza na barabara ya Kibada mwasonga basi tunaombaa msogee mpaka kimbiji!!
 
Barabara ya Kibada-Mwasonga ipo kwenye mpango wa kujengwa kwa kiwango cha lami. Kwa mwaka ujao wa fedha upembuzi yakinifu unaendelea.
Natambua kuwa barabara hii imeharibika sana katika kipindi hiki cha mvua. Tayari nimeshawajulisha Tanroads kuikagua na kuchukua hatua za dharura. Matenngenezo makubwa yatafanyika baada ya mvua kukatika.
Poa mkuu. Maana hata juzi umeskia malori na magari kama 30 hivi yamekwama kwenye hiyo njia. Cement iliyokuwa kwenye malor hayo iliganda. Nina plot mitaa hiyo lakini nashindwa kujenga kwa ajili ya barabara mbovu
 
Heshima kwenu wakuu,

Ujenzi wa Barabara inayotoka Daraja la J.K.Nyerere Kigamboni Dar es Salaam hadi Njia panda ya Kibada kwenda Kivukoni imeshaanza. Ujenzi umeanza kwa kasi kubwa.

Hapa chini nmeambatanisha picha zikionesha wafanyakazi wakiendelea na kazi.
ki5.jpg
ki4.jpg
ki3.jpg
k2.jpg
Ki1.jpg

Picha zinazoonesha Utengenezaji wa barabara ukiendelea.
 
Wakati huo huo, kivuko Kipya ambacho kilisimamiwa na Mradi wa Tushirikishane kimeanza kazi. Hii ni ahadi moja wapo ambayo Mbunge aliahidi kweenye huu Mradi na imekamilika.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amepokea Kivuko cha MV Kazi kutoka kwa Kampuni ya kizalendo ya M/S Songoro Marine Transport Boatyard ya Mwanza iliyokuwa inafanya kazi ya ujenzi wa Kivuko hicho mara baada ya ujenzi wake kukamilika.
Mbarawa 05.jpg

Baadhi ya wananchi wakiteremka katika Kivuko cha MV. KAZI mara baada ya kukabidhiwa rasmi kwa Serikali mapema hii leo Magogoni jijini Dar es Salaam toka Kampuni ya Songoro Marine Transport Ltd. Iliyokuwa ikikijenga Kivuko hicho

Akizungumza na wananchi, Prof Mbarawa alisema lengo la Serikali kuongeza Kivuko hicho ni kuboresha huduma za kusafirisha abiria na magari kati ya Magogoni na Kigamboni.

“Uwepo wa vivuko vitatu kutasaidia utoaji wa huduma kwa wakati na kwa urahisi na ikitokea Kivuko kimoja kimepelekwa kufanyiwa ukarabati huduma zitaendelea kama kawaida bila kuathiri utaratibu wa kawaida”.Alisema Prof Mbarawa.

Ameongeza kuwa ili kuendana na kasi ya Mhe. Rais John Magufuli Wizara yake itaendelea kuboresha huduma za Vivuko katika Mikoa mingine ikiwemo Mkoa wa Lindi , Kivuko cha Pangani, na Kivuko cha Kigongo Busisi Mkoani Mwanza.

Nae Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Dkt. Mussa Mgwatu alisema Kivuko cha MV Kazi kimejengwa kulingana na viwango vinavyotakiwa Kimataifa na ukaguzi wake umefanywa na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) na kuthibitishwa kuwa ni salama kwa ubebaji wa abiria na magari.

Ujenzi wa MV KAZI umegharimu Shilingi Bilioni 7.3 za Kitanzania na kina uwezo wa kubeba abiria 800 magari 22 sawa na jumla ya tani 170.

Kivuko hicho kimekabidhiwa leo kwa ajili ya kuanza kutoa huduma kati ya Magogoni na Kigamboni Jijini Dar es salaam na kuongeza idadi ya vivuko katika eneo hilo kufikia vitatu
 
miezi miwili imepita na hakuna chochote kinachofanyika,,, jaman Mbona Tanesco mnatutesa hivi wana kigamboni?
Mkuu nguzo zinaendelea kusambazwa. Mambo mazuri hayataki haraka. Kwani sasa Kigamboni itakuwa na Kituo chao wenyewe cha kupozea na Kusambaza Umeme.
 
Hao waliokipa kivuko jina mbona hawajiamini. Hilo jina hawakulitendea haki. Lingetakiwa liwe , "MV HAPA KAZI TU" fungukeni bwana mbona jamaa so far anastahili hiyo heshima kabisa.

Kama vile kuna kaubaguzi katika kutolea majibu changamoto zinazoletwa katika huu uzi? Nyengine zinapotezewa.


Na washawasha!
 
Hoa waliokipa kivuko jina mbona hawajiamini. Hilo jina hawakulitendea haki. Lingerakiwa liwe , "MV HAPA KAZI TU" fungukeni bwana mbona jamaa so far anastahili hiyo heshima kabisa.

Kama vile kuna kaubaguzi katika kutolea majibu changamoto zinazoletwa katika huu uzi? Nyengine zinapotezewa.


Na washawasha!
Hazipotezewi mkuu, kuna majibu mengine yanahitaji data sahihi. Hivyo utajibiwa usihofu.
 
Back
Top Bottom