Dr F. Ndugulile tunaomba uje utoe ufafanuzi. Kuishi kigamboni na kufanyakazi upande wa mjini kwa mmiliki wa gari inakugharimu 3000/- per day. Gharama hii ni nje ya gharama nyingine yoyote.
Bado ili ulipe hio 3000/- inabidi kupita sehemu ambayo inaharibu kabisa gari lako. Mimi nimehamia huko miezi kama 7 iliopita, gari langu lilikuwa kama jipya, ndani ya miezi mitatu halifai kabisa! Nikabadili vikorokoro vyote vinavyohusiana na matairi ila sasa hivi tena halifai kabisa.
Hivi huwa unapita hii njia? Inawezekana unapita na VX kwahio huwezi kuhisi ubovu wa hii barabara. Ni aibu kipande cha 1.2km sasa hivi kinakaribia mwaka kinatusumbua. Daraja limegharimu 200bn lakini kipande ambacho gharama yake haiwezi kuzidi 2bn kinakuwa kibovu na kichafu hivi.
Hatuwezi kufanya kitu chochote kwa ukamilifu?