Ndio home town sioNzega bado haina high school hata moja
high school ni muhimu mno
halafu kiwepo chuo kimoja hata cha wauguzi tu
Hata mimiBashe ni MwanaCCM pekee ninayemkubali,kila la kheri.
kiongozi unaitaji msaada upi kutoka kwa afisa habari tumpm ajeafisa habari kaingia uvunguni nn?
Tupo pamoja kiongozi karibu katika hoja tulisogeze gurudumu la maendeleo ya nzega mbeleafisa habari kaingia uvunguni nn?
Hongera wana Nzega, tuko pamoja. Good initistive, mie jirani yenu wa Kasubuya.Mradi wa Tushirikishane (JamiiForums yazindua rasmi mradi wa "Tushirikishane") umeanza rasmi jimbo la Nzega mjini chini ya Uongozi wa Mheshimiwa Mbunge Hussein Bashe
Tokana na misingi ya TUSHIRIKISHANE iliyoelemea katika kuwawezesha wabunge wa kuchaguliwa kutekeleza ahadi 4 kati ya jumla ya ahadi walizotoa wakati wa uchaguzi kwa urahisi kwa kushirikiana na wananchi; mada hii itatumika kuwasilisha, kujadili na kupeana taarifa ya kile kinachojiri Nzega mjini.
Ahadi walizochagua kufuatilia wananchi wa Nzega mjini kwenye mradi wa TUSHIRIKISHANE
a. Kukamilisha ujenzi wa kituo kipya cha mabasi-Nzega
b. Ujenzi wa Nyumba ya Daktari-Kituo cha Afya Nhobora
c. Kukamilisha mpango wa muda mfupi wa upatikanaji wa Maji safi na salama-Nzega kwa kuongeza mita za ujazo 1300
d. Kukamilisha mabweni na madarasa ya kidato cha 5&6-Sekondari ya Bulunde
Mada hii itatumika zaidi na Wana Nzega kutupa taarifa.
Baadhi ya Washiriki watakuwa:
1. Mh. Mbunge Hussein Bashe
2. Gideon Anyona (Katibu)
3. Josephat Sanga (Afisa habari Nzega)
4. Na washiriki wote wa Warsha hiyo na wale wote wenye mapenzi ya Maendeleo ya Nzega mjini.
Karibuni...
Hayo madarasa mbona hayana madirisha?View attachment 391755 View attachment 391755 View attachment 390727 View attachment 390728 View attachment 390729 picha ni madarasa mawili ya kidato cha tano na cha sita ambayo yamekamilika, pia jengo ambalo ni bweni la wanafunzi ambalo lipo katika ujenzi unaoendelea katika shule ya sekondari
Bulunde
Kitu kingine wadau tukumbushane mradi huu upo katika halmashauri ya mji nzega halmashauri ambayo ni mpya kwaiyo ndio inaanza jiimalisha
Kipindi nzega haijagawanywa ni halmashauri moja ya wilaya zilikuwepo shule za kidato cha tano na cha sita shule mbili
Shule ya sekondari UCHAMA ambayo si ya serikali na shule ya sekondari KILI iliyopo Bukene hii ni shule ya serikali
Hivyo basi baada ya wilaya ya nzega kugawanywa kuwa na halmashauri mbili ambayo ni halmashauri ya mji nzega ambayo ndio jimbo la nzega mjini Mbunge wake Husen bashe na kuwepo kwa halmashauri ya wilaya ya nzega ambayo ni jimbo la nzega vijijini Mbunge wake Mh Dr Kigwangala
Basi jimbo la nzega mjini likajikuta halina shule ya kidato cha tano na cha sita ambayo ni Mali ya umma kwani KILI SEKONDARI ilibakia katika jimbo la nzega vijijini ambayo ni halmashauri ya wilaya ya nzega
Shule iliyopo ya kidato cha tano na sita kwa sasa katika halmashauri ya mji nzega ni ya UCHAMA ambayo si Mali ya umma (serikali)
Hivyo basi huu ujenzi wa sasa nihatua ya kuhakikisha mji wa nzega unakuwa na shule ya kidato cha tano na cha sita ambayo ni Mali ya umma (serikali)
High school wala usomi haihusiani na CCM. Kama hivyo kanda ya kaskazini wangekuwa ni CCM zaidi kwa kuwa kuna high school na wasomi na lami na hospitali nzuri tu. Zote zilijengwa na CCM hiyo hiyo lakini si kwa sera bali kwa ukabila na ubinafsi wa watu wa huko kushika hatamu serkalini. Hivi hukumbuki waziri mkuu ametoka kanda ya wapinzani mara 5, na mawaziri husika, lakini hasa watendaji idara nyeti za serkalini. Kanda hiyo haikujengwa kwa sera nzuri za upinzani bali kwa ukabila wa watendaji ndani ya serkali ambao wengi wao walitoja huko - sasa wanataka dola waanze ukabila wao tena. Nzega oyee! Iramba oyee! Chunya oyee! Wote mliosahauliwa sasa CCM iko kwa faida yenu. UKAWA ni walewale waliowadumaza walipokuwa CCM wakapeleka rasilimali za taifa kwao. Sasa tuna Waziri Mkuu toka Tandahimba na CCM inaelewa fika jinsi nchi hii ilivyokuwa inaliwa na ukanda mmoja haitotokea tena.Tabora si ndo maana CCM wanashinda asilimia 100 kila uchaguzi
tukipata hizo high school 10 na ccm inakufa