Josephat Sanga
Senior Member
- Aug 29, 2016
- 151
- 98
Bwana step ushauri wako tutaufanyia kazi asante kwa mawazo yako mazuri
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kiongozi tunaomba uendelee kufuatilia huu mjadala wetu kwani moja ya huu mpango kazi ni kutatua kero ya maji katika mji wa nzega na makubaliano ni hatua ya awali kipindi huo mradi wa maji kutoka ziwa Victoria unasubilia basi makubaliano yamefanyika kuwa kipindi huu mradi upo mjini nzega basi hatua ya awali ya kupunguza changamoto ya maji nzega ifanyike na sasa imeanza fanyiwa kaziChangamoto ya huduma ya maji bado ni kubwa Nzega. Ule mpango wa kufikisha maji ya Ziwa Victoria sijui umefikia wapi?
Hapa Boss upo sahihi, pamoja na shule ya Bulunde kuwa high school, Halmashauri iangalie sasa shule nyingine ambayo itaendelezwa kuwa high school ndani ya kipindi hiki cha miaka mitano. Kwakuwa Nzega ilikuwa nyuma sana ni wakati muafaka wa kukimbia sasa mbio za maendeleoBado tatizo la kutokuwepo high school ni kuubwa sana
iwepo moja au mbili bado haitoshi
View attachment 391755 View attachment 391755 View attachment 390727 View attachment 390728 View attachment 390729 picha ni madarasa mawili ya kidato cha tano na cha sita ambayo yamekamilika, pia jengo ambalo ni bweni la wanafunzi ambalo lipo katika ujenzi unaoendelea katika shule ya sekondari
Bulunde
Kitu kingine wadau tukumbushane mradi huu upo katika halmashauri ya mji nzega halmashauri ambayo ni mpya kwaiyo ndio inaanza jiimalisha
Kipindi nzega haijagawanywa ni halmashauri moja ya wilaya zilikuwepo shule za kidato cha tano na cha sita shule mbili
Shule ya sekondari UCHAMA ambayo si ya serikali na shule ya sekondari KILI iliyopo Bukene hii ni shule ya serikali
Hivyo basi baada ya wilaya ya nzega kugawanywa kuwa na halmashauri mbili ambayo ni halmashauri ya mji nzega ambayo ndio jimbo la nzega mjini Mbunge wake Husen bashe na kuwepo kwa halmashauri ya wilaya ya nzega ambayo ni jimbo la nzega vijijini Mbunge wake Mh Dr Kigwangala
Basi jimbo la nzega mjini likajikuta halina shule ya kidato cha tano na cha sita ambayo ni Mali ya umma kwani KILI SEKONDARI ilibakia katika jimbo la nzega vijijini ambayo ni halmashauri ya wilaya ya nzega
Shule iliyopo ya kidato cha tano na sita kwa sasa katika halmashauri ya mji nzega ni ya UCHAMA ambayo si Mali ya umma (serikali)
Hivyo basi huu ujenzi wa sasa nihatua ya kuhakikisha mji wa nzega unakuwa na shule ya kidato cha tano na cha sita ambayo ni Mali ya umma (serikali)
karne ya 21 hamna high school hata moja?
Mama yangu mzazi!!!
Nzega ni mji wa kinyamwezi sana, uswahili mwingi kazi sifuri. Haiwezekani mpaka leo hamna shule ya kidato cha tano na sita kwa kisingizio kuwa ni halmashauri mpya ya mji. Wewe afisa habari unazua maswali mengi sana mana hoja zako ni mfu!
Ikumbukwe nzega mji ni mji uliojengwa na mkoloni na sisi kurithi tu, majengo ya Serikali ni mengi na mji umepangika. Jibu ni rahisi tu elimu sio kipaumbele chenu wanyamwezi kwani mnazidiwa hata na wilaya ya igunga ambao wana high school na ikumbukwe wilaya hii ilizaliwa na nzega miaka 1970,s na inaendelea kwa kasi ya ajabu. ushauri wa bure acheni ujanjaujanja jengeni shule sio kutegemea serikali.
Kiongozi shule ya kili sasa ina kidato cha tano na cha sita ina kama mwaka mmoja sasa na kitu tangu ianzeLink Kili imekuwa high school? Au mnataka kufunika aibu ya Nzega? Kifupi wilaya ya nzega haikuwa na high school hata moja ya serikali sasa Mhe.Bashe ameanza kuhamasija ujenzi was shule moja ya Bulunde.
Ikumbukwe Mhe. Kigwangala alitudanganya kuwa hadi anamaliza kipindi chake angekuwa amesaidia uanzishwaji wa high school 4 nazo ni Nzega day, Chief Ntinginya, Ndala na shule moja siikumbuki. Naomba turejee taarifa zake zipo mitandaoni tulimsifia sana akamaliza muda wake bilabila sasa hv humsikii akiliongelea.
Ninachoweza kumuomba Mhe. Bashe kuwa shule moja ya high school in mwanzo mzuri lakini ajitahidi tufikishe at least 4 za serikali kama tunania ya dhati ya kuwakomboa watu wake ki elimu.