Taarifa ya mwezi wa tatu hadi mwezi wa Tisa mwaka 2016 juu ya shughuli mbali mbali zinazofanywa mojakwamoja na Ofisi ya Mbunge na Halmashauri ya Mji wa Nzega.
__________________
Ni takriban miezi tisa sasa tangu Mh Mbunge Hussein Mohammed Bashe apewe ridhaa na wananchi wa jimbo la Nzega mjini ya kuwawakilisha bungeni.
Katika kipindi hiki kifupi cha uwakilishi wake wa jimbo hili kuna miradi mingi ambayo imeanzishwa mengine tayari imekamilika na mingine ikiendelea na ipo kwenye hatua nzuri. Miradi hii imegawanywa katika sekta;
[emoji117] Uchumi
[emoji117]Afya
[emoji117] Elimu.
[emoji117] Maji
Kwenye sekta ya uchumi tuna miradi ifuatayo;
1. [emoji117] Stendi mpya ya mabasi Bulunde
2. [emoji117] Mgodi wa Namba saba Halisi
3. [emoji117] Fursa sawa kwa wote wa Airtel kwa kupitia Nzega Urban Trust Fund
4. [emoji117] Uwezeshwaji wa Mamantilie na ofisi ya Mbunge mojakwamoja
5. [emoji117] Mikopo kutoka Halmashauri ya asilimia 10% kwa makundi ya vijana na wanawake.
6. [emoji117] Mradi wa kutoa elimu ya ujasiriamali na kuwawezesha wananchi na rasilimali fedha kupitia shirika la TYEEO ( Tanzania Youth Enterprenurship and Empowerment Organization
7. [emoji117] Mikopo ya Pikipiki bodaboda kwa vikundi.
Kwenye sekta ya Afya kuna miradi ifuatayo;
1. [emoji117] Bima ya afya ya CHF
2. [emoji117] Kituo cha Afya cha Kijiji cha Nhobola Kata ya Mbogwe .
3. [emoji117] Ujenzi wa jengo la upasuaji kituo cha agya Zogolo Kata ya Nzega Ndogo
4. [emoji117] Mchakato wa kurudisha hospitali ya Wilaya kuja kwenye mamlaka ya Mji wa Nzega.
Sekta ya elimu ina miradi ifuatayo;
1. [emoji117] Mradi wa shule ya Bulunde ambao umelenga kuanzisha shule itakayotoa kidato cha 5&6.
2. [emoji117] Ujenzi wa majengo manne yaani madarasa 3 na ofisi ya walimu shule ya msingi Shalemwa.
3. [emoji117] Ujenzi wa madarasa mawili shule ya msingi maporomoko.
4. [emoji117] Ukarabati wa madarasa mawili shule ya msingi Kitengwe.
SEKTA YA UCHUMI:
1.[emoji117] Mradi wa stendi mpya ya mabasi Bulunde
__________________
Mradi huu umeshakamilika kwa asilimia 90% na ni moja kati ya miradi ambayo itazinduliwa na Mwenge tarehe 25.09.2016. Mambo ambayo tayari yameshakamilika katika mradi huu phase 1 ni;
[emoji810] Ujenzi wa kituo cha polisi
[emoji810] Ujenzi wa jengo la abiria yaani 'waiting hall'
[emoji810] Ujenzi wa vyoo vya abiria
[emoji810] Jengo la ofisi yaani 'Administration Block'
[emoji810] Miundombinu ya Umeme
[emoji810] Matenki ya Maji na miundombinu yake.
Shughuli zinazoendelea kwa sasa:
_________________
[emoji810] Ujenzi wa vibanda vya biashara kwa kupitia mfumo PPP ( Public Private Partnership ) ambapo kamati ya zabuni imeshaketi na kamati ya fedha imesharidhia na kubariki mikataba itayotolewa.
Katika mfumo huu wananchi watakua wanajenga vibada vyao na kurudisha gharama zao kwa kupitia makato yao ya kodi ya pango.
Kuanzia wiki ijayo wananchi wataanza kupewa mikataba.
2.[emoji117] Mgodi wa Namba saba Halisi.
_________________
Katika kutimiza ahadi yake ya kuwatafutia wananchi wake fursa za kiuchumi na kujiajiri, Mh Mbunge aliomba serikalini mgodi huu ambao hapo awali ulikua chini ya mwekezaji mmoja.
Serikali iliridhia ombi hilo na hatimae wananchi wakapewa eneo hilo kwaajili ya uchimbaji mdogo. Kwasasa eneo hilo lina takriban vijana 3000 ambao wanajishughulisha na uchimbaji na wana kipato halali.
3. [emoji117] Mradi wa Airtel fursa sawa kwa wote ambapo Airtel wametoa millioni 20
4. [emoji117] Mikopo kwa vikundi vya ujasiriamali vya Mamantilie ambapo mpaka sasa jumla ya vikundi 25 vimeshakopeshwa, na kupata mikopo isiyokuwa na riba.
5. [emoji117] Asilimia 10% ya mapato ya ndani ya Halmashauri fedha zinakopeshwa kwa vikundi vya wanawake na wanaume.
6. [emoji117] Mradi mkubwa ambao ni endelevu unaoendeshwa na shirika la TYEEO(Tanzania Youth Enterprenurship and Empowerment Organization ) likishirikiana na ofisi ya Mbunge . Katika mradi huu ambao upo jimbo zima wananchi watakua wana wanapewa elimu kwa muda wa miezi mitatu wakiwa wameandaliwa katika makundi ya watu wasiozidi 30 na baada ya miezi mitatu ya elimu ya ujasiriamali, wataanza kukopeshwa.
7. [emoji117] Mradi wa mikopo ya pikipiki za bodaboda ambapo jumla ya pikipiki 31 zimeshakopeshwa kwa vijana.
SEKTA YA AFYA:
1. [emoji117] Ujenzi wa jengo la upasuaji kituo cha afya Zogolo Kata ya Nzega Ndogo
2. [emoji117] Ujenzi wa nyumba ya Mganga katika kituo cha Afya cha Nhobola Kata ya Mbogwe
3. [emoji117] Ujenzi wa Zahanati ya Idudumo ambapo ofisi ya mbunge imechangi mifuko ya cement na Matofali ya ujenzi
4. [emoji117] Jitahada na mikakati inayoendelea ya kurudisha hospitali ya Wilaya kuja kwenye. mamlaka ya Mji.
5. [emoji117] Huduma ya Bima ya Afya ya CHF ambapo Mh Mbunge alikatia Kaya 200 zisizojiweza kwaajili ya huduma hii na wanachama wote wa chama cha bodaboda Nzega mjini.
SEKTA YA ELIMU :
1. [emoji117] Mradi wa Shule ya Bulunde ambapo ukikamilika utatoa nafasi kwa jimbo la Nzega kuwa na shule ya kidato cha 5&6. Phase 1 yaani awamu ya kwanza ya mradi huu imeshakamilika ambapo madarasa mawili yamejengwa. Phase 2 yaani awamu ya pili ni ujenzi wa bweni na vyoo vya bweni ndio unaendelea . Awamu ya kwanza imegharimu takriban millioni 40 fedha ambazo zimetoka mojakwamoja kwa Mh Mbunge.
2.[emoji117] Ujenzi wa nyumba ya mwalimu Mwanyagula 2 in 1.
3. [emoji117] Nyumba ya mwalimu shule ya Nhobola
4. [emoji117] Ujenzi wa madarasa matatu na ofisi ya walimu shule ya msingi Shalemwa . Ujenzi wa madarasa haya utawaokoa wanafunzi wanaotembea km 10 kwenda shule. Ikimbukwe kwamba shule hii ujenzi wake unafadhiliwa mojakwa moja na mbunge kwani ndio mwanzilishi wa shule hii baada ya kupokea maombi ya wananchi kuhusu watoto wao ambao walikua wakitembea km 10 kwenda kutafuta elimu.
5. [emoji117] Ujenzi wa madarasa matatu shule ya msingi maporomoko .
6. [emoji117] Ukarabati wa madarasa mawili shule ya msingi ya Kitengwe. Haya ni madarasa ambayo watoto walikua wanasoma kwenye sakafu ya vumbi.
7. [emoji117] Ujenzi wa madarasa mawili shule ya msingi ya Undomo.
8. [emoji117] Ulipiaji wa ada ya wanafunzi kama ifuatavyo;
[emoji810]Vyuo vikuu wanafunzi 14
[emoji810] VETA wanafunzi 19
[emoji810] SEKONDARI wanafunzi 34.
UJIO WA MWENGE TAREHE 25.09.2016
_________________
Ujio wa Mwenge katika Jimbo letu la Nzega Mjini utakuja kuzindua miradi ifuatayo;
1. [emoji117] Ujenzi wa stendi mpya ya mabasi
2. [emoji117] Mradi wa Bima ya afya kwa wazee waliozidi fikisha miaka 60 na zaidi
3.[emoji117] Kufungua Ofisi ya Serikali ya Kata katika kata ya Mbogwe.
4. [emoji117] Ujio wa Mwenge pia utatoa fursa kwa jimbo letu kupata msaada wa shillingi millioni 10 ili kusaidia jitiada za Mbunge za kuwawezesha wananchi kwa mikopo nafuu.
Lakini nimalizie kwa kutaja jitahada za Mh Mbunge ambazo anaendelea kuzifanya katika kuwaletea wananchi wake maendeleo;
1. [emoji117] Kurudisha eneo la uwanja wa ndege kwa wananchi ambapo tayari Mh Mbunge ameshaongea na waziri husika na tayari taratibu za kiserikali zinaendelea
2. [emoji117] Mh Mbunge ameshaongea na waziri wa elimu kuhusu madai ya walimu tofauti na mishahara yao. Tayari serikali imeshapokea maombi hayo na muda wowote kuanzia sasa walimu wataamza kulipwa madai yao.
3. [emoji117] Mh Mbunge ameongea na waziri wa nishati na madini kuhusu uwezekano wa kuongeza eneo la uchimbaji kitalu cha 3 kwenye mgodi wa Namba 7 halisi. Maombi haya yamepokelewa wizarani na maendeleo ni mazuri.
4. [emoji117] Maombi ya kuchukua majengo ya mchina kwenye kambi ya mkandarasi huyo ili kukigeuza kituo icho kuwa cha VETA. Tayari serikali imeshaachia majengo ya Tanroad.
5. [emoji117] Uwepo wa kituo pekee cha uwekezaji cha EPZ Kata ya Nzega Ndogo ambapo eneo tayari limeshapimwa na taratibu zingine za kiserikali zinaendelea.
6. [emoji117] Jitahada za kutatua kero ya maji. Suluhisho la muda mfupi tayari changamoto yake imeshatatuliwa ambapo takriban Tsh millioni 520,000,000/= zimeshapatikana kwaajili ya kujenga machujio mapya na kukarabati ya zamani.
Suluhisho la muda mrefu ni mradi wa Ziwa Victoria ambapo fedha zake zimeshapatikana kupitia Bank ya Exim India.
MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI JIMBO LA NZEGA MJINI.
Imeandaliwa na;
Katibu wa Mbunge Ofisi ya mbunge Jimbo la Nzega Mjini.