TUSHIRIKISHANE Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Nzega

TUSHIRIKISHANE Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Nzega

Ujenzi wa Nyumba ya Daktari katika kituo cha Afya Nhobora

Maendeleo ya mpango huu Jana, Siku ya tarehe 10/10/2016 mtendaji kata wa kata ya Mbogwe, kapewa barua na mkurugenzi wa mji nzega, kuhakikisha mtendaji wa kijiji cha Nhobola aliyesimamishwa kazi kutokana na kukataliwa na wanakijiji wa kijiji cha Nhobola kuwa mtendaji wa kijiji hicho, ahakikishe anakabizi ofisi ndani ya Siku saba na kuruhusu mambo mengine yaendelee kuhusu maendeleo ya ujenzi wa nyumba ya Daktari.
 
Leo tarehe 11.10.2016 Mheshimiwa mbunge wa jimbo la Nzega mjini ameendelea na ziara yake ya ukaguzi wa miradi mbalimbali ndani ya jimbo lake ambayo imeanzishwa na nguvu za wananchi sambamba na kusikiliza kero za wananchi na kuzipatia ufumbuzi.

Kituo cha kwanza kilikua kwenye kijiji cha Undomo Kata ya Uchama. Hapa Mheshimiwa mbunge alikagua zahanati ya Undomo na kuchangia Tsh millioni moja kwaajili ya kufanya wiring na kuvuta umeme. Ikumbukwe kwamba zahanati hii ilikua bado haina umeme.

Kituo cha pili kilikua kijiji cha Idala ambapo napo kuna changamoto kubwa ya maji. Hapa Mheshimiwa mbunge amechangia Shillingi laki tano (500000) kwaajili ya kuchimba Bwawa la Idala na kuliongezea kina. Mheshimiwa mbunge pia amechangia matofali 10000 kwaajili ya ujenzi wa zahanati ya Idala.
Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa kikundi cha Umoja Mining Group kinachochimba kwenye mgodi wa namba 7 halisi ameahidi matofali 1000 na kujenga msingi wa zahanati.

Kituo cha tatu na cha mwisho kilikua kijiji cha Uchama. Kijiji hiki kina changamoto kubwa ya huduma ya afya kupatikana kwa mbali. Mheshimiwa mbunge amechangia tofali 10000 na mifuko 50 ya cement.
Katika hatua nyingine kikundi cha Umoja Mining Group katika jitihada za kumuunga mbunge kwenye shughuli za kimaendeleo, nao wamehaidi shillingi lako tano (500000 ) na Matofali 1000.

Imetolewa na Katibu Ofisi ya Mbunge.
 
IMG-20161011-WA0017.jpg
IMG-20161011-WA0008.jpg
Leo katika ziara ya Mheshimiwa Mbunge katika kijiji cha Undomo kuna ubadhirifu mkubwa sana umegundulika katika zahanati ya kijiji cha Undomo.

Wananchi wamekua hawapati dawa wanapokwenda hapo mida ya mchana na wagonjwa ambao kisera wanatakiwa kupata matibabu kukosa matibabu.

Baada ya kuuliza wananchi mh mbunge aligundua ;

1: Madawa yanayopelekwa na MSD mganga wa kituo hicho huhamishia katika duka lake binafsi.

2: Kamati ya Afya ya kijiji kutoshirikishwa ktk upokeaji wa madawa na kushiriki katika kufunga taarifa madawa yanapoisha.

3: Watu wenye kadi za CHF badala ya kutibiwa watu 6 badale yake wanatibiwa wawili

4: Wagonjwa kukosa huduma kila baada ya saa 6 mchana na kuambiwa wamechelewa.

Hatua alizochukua mbunge;

Mbunge aliamua kwenda kwenye duka na kukuta madawa ambayo yangetakiwa kwenda zahanati.

Mbunge aliunda kamati ya afya mpya katika mkutano huo wa hadhara.

Kuwaomba wananchi kutoa taarifa zozote zile za ubadhirifu Halmashauri au ofisini kwake.

Aidha Mheshimiwa mbunge aligundua ubadhirifu wa zaidi ya milioni 7 na kuagiza wiki ijayo mkutano wa kijiji uitwe chini ya Usimamizi wa sungusungu mapato yasomwe na mtendaji asipofanya hivo sungusungu wamkamate mtendaji na kuitaarifu jeshi la polisi.

imetolewa na Katibu wa Mbunge Nzega
 
Yupo vizuri na ana harufu ya mabadiliko kiongozi huyu.
 
Airtel Tanzania kupitia mpango wake wa Airtel FURSA “Tunakuwezesha” kwa kushirikiana na Nzega Urban Trust Fund asasi iliyoundwa kimkakati na Mbunge wa Jimbo la Nzega Mjini Mhe. Hussein Bashe ili kumaliza tatizo la umasikini wa kipato Jimbo la Nzega Mjini leo imezindua programu maalumu ya kuwezesha vijana iliyopewa jina la WanaNzengo Airtel FURSA.

Programu hii itawawezesha zaidi ya wajasiriamali 350 kunufaika na mikopo kupitia huduma ya Airtel Money. Mikopo hii itatolewa kwa kikundi kilichoundwa na vijana watano ambao watapewa mtaji kati ya shilingi Shs.100,000 hadi 1,000,000 kulingana na mahitaji yao.
IMG-20161012-WA0017.jpg
IMG-20161012-WA0013.jpg
 
Kiukweli Mala ya kwanza nilikuwa sina imani na Mh Bashe nilijua uyu mbunge sawa na wale wale waliotangulia kina seleli na Kigwangala ila sasa nimeanza kuona utofauti bashe ni mbunge wa kipekee, ila sifa tunazokupa usijisahau wananzega tunataka maendeleo hasa tatizo la maji ufumbuzi wa haraka unaitajika
 
IMG-20161020-WA0003.jpg

Kukamilisha mabweni na madarasa ya kidato cha tano na cha sita katika shule ya sekondaro Bulunde


MAENDELEO YA MRADI

Leo tarehe 13/10/ 2016 naibu Waziri wa TAMISEMI bwana Selemani Jaffo akiongozana na Mh Mbunge Hussein bashe wametembelea katika shule ya sekondari Bulunde, kuangalia maendeleo ya ujenzi wa madarasa ya kidato cha tano na cha sita ambapo madarasa mawili tayali ujenzi wake umekamilika, vile vile kuangalia maendeleo ya ujenzi wa mabweni ambao mpaka sasa bado unaendelea
 
IMG_20161013_174327.jpg
ikiwa ni mwendelezo wa ziara za Mh Mbunge kuonana na wakazi wa Jimbo la Nzega Mjini kwa lengo la kukagua mipango ya maendeleo ya jimbo, na kusikiliza changamoto za wanaichi, maoni, ushauri, pamoja na kuwapa mrejesho wa changamoto mbali mbali ambazo Mh Mbunge Hussein bashe amezishuguliakia na ambazo bado anaendelea zishugurikia

Leo tarehe 13 /10 /2016 Mh Mbunge alikuwa katika kata ya Nzega magharibi katika mtaa wa majengo, Mh Mbunge kasema kuanzia mwaka wa masomo 2017, wanafunzi wote watakao chaguliwa kujiunga na kidato cha tano haijalishi umechaguliwa shule iyopo ndani ya mji wa Nzega, au nje ya Nzega kinachoangaliwa tu mwanafunzi aliyechaguliwa kujiunga na kidato cha tano awe anatoka ndani ya Jimbo la Nzega Mjini, na shule aliyomaliza kidato cha nne iwe ipo ndani ya Jimbo la Nzega Mjini, Mh Mbunge kasema atawalipia ada mpaka pale watakapo maliza masomo yao ya kidato cha tano na cha sita, jambo hili ni endelevu mpaka pale mda wake walitumikia Jimbo la Nzega Mjini ni kuisha

Hii inatokana na ahadi alizo ahidi kipindi cha uchaguzi kuwa endapo atakuwa Mbunge wa Jimbo la Nzega Mjini, basi elimu ya kidato cha kwanza mpaka cha sita itakuwa bure, kwakua ahadi yake ili endana na moja wapo ya ahadi ya chama chake cha mapinduzi (CCM) kuwa endapo chama cha mapinduzi kitaongoza inchi elimu ya msingi itakuwa bure (kuanzia darasa la awali mpaka kidato cha nne) hivyo baada ya chama cha mapinduzi kushinda na kuongoza inchi ahadi ya elimu bure inatekelezwa

Kwa maana hiyo elimu ya kidato cha tano na cha sita kwa sasa siyo bure, ni ya kulipia hivyo basi ili kutimiza ahadi yake Mh Mbunge aliyo ahidi kipindi cha kampeni zake leo katamka kuwa garama hizo zote za kusoma kidato cha tano na cha sita Mbunge ata garamia endapo mwanafunzi atafauru kuendelea na masomo ya kidato cha tano na cha sita.
 
Hilo suala la kusomesha wanafunzi watakao chaguliwa kujiunga kidato ha tano na cha sita nampongeza Mbunge cha muhimu asikabidhi suala hili mikononi mwa watu vijana watapata shida uko mashuleni waendapo suala hili asimamei yeye kama yeye Mbunge
 
>Kukamilisha ujenzi wa kituo cha mabasi Nzega

MAENDELEO YA MRADI

Halmashauri ya mji nzega kuanzia kesho juma tatu ya tarehe 17/10/2016 itaanza kutoa fomu za maombi ya zabuni kwa mtu au kikundi kinachoitaji kujenga banda au vibanda vya biashara katika kituo kipya cha mabasi Nzega

Gharama za uchukuaji fomu ya maombi ni shilingi laki moja (100,000/=)
 
Ombi hapa kwenye ugawaji wa zabuni isije kutokea Mbunge, au madiwani wakachukua maeneo kwa kigezo cha wameshinda zabuni nzega tunaijua siye yani mkurugenzi hapo chonde chonde tunakuomba hilo uzingatitie isije hayo maeneo wapewe wafanya biashara tu ikiwezekana wanapokuja kuomba zabuni muweke na kipengere ili ushinde zabuni inabidi uwe na tin namba na leseni ya biashara ambayo ins zaidi ya mwaka maaana watu wa halmashauri watatumia watu kushika maeneo mfano hata Mbunge uyu asije jimilikisha maeneo kwa kutumia vijana wake
 
>ujenzi wa nyumba ya Daktari katika kituo cha afya Nhobora

IMG_20161017_135120.jpg
IMG_20161017_135120.jpg
MAENDELEO YA MPANGO

Mtendaji wa kata ya Mbogwe, leo tarehe
17/10/2016, amekabidhi ofisi ya afisa mtendaji wa kijiji cha Nhobola, kwa mwenyekiti wa kijiji cha Nhobola, akiwa pamoja na wenyeviti wa vitongoji wa kijiji cha Nhobola, ili mwenyekiti wa kijiji aweze kuitisha kamati ya kijiji ikae na kukubaliana ili wachague kaimu mtendaji wa kijiji wa mda na kwenda benki kuchukua pesa ili ujenzi wa nyumba ya Daktari katika kituo cha Afya Nhobora uweze kuendelea

Hatua hii imekuja baada ya mtendaji wa kijiji cha Nhobola kusimishwa kazi na mkurugenzi wa mji nzega na kuombwa akabidhi ofisi ndani ya Siku saba

Hivyo Siku ya ijumaa ya tarehe 14/10/2016 mtendaji wa kijiji cha Nhobola amekabidhi ofisi kwa mtendaji wa kata ya Mbogwe
 
Miye naombi kwa Mbunge, mkurugenzi, afisa habari na Katibu jamani mda waliotoa tuchukue fomu za zabuni ni mdogo yani Siku tatu leo juma tatu mpaka juma tano alafu jambo lenyewe tumetangaziwa jana ombi ebu wambie watuachie huu mwezi wote hii haraka haraka inaibua maswali kwanini haraka hivi au tayali wamekwisha gawia viwanja wao kwa wao ili ni ombi
 
View attachment 390714 View attachment 390716 View attachment 390717 View attachment 390718 View attachment 390718 View attachment 390719 MuView attachment 390719 View attachment 390713 muonekano tofauti tofauti wa kituo kipya cha mabasi Nzega kinachoendelea na ujenzi, jengo la kituo cha polisi na vyoo tayali vimekamilika, banda la kupumzikia wageni wakiwa wanasubilia magari linaendelea na ujenzi kama tunavyoona katika picha, ikiwa ni mwezi wa kwanza kuanza kwa mradi wa TUSHIRIKIANE NZEGA.

Mkuu hii stendi inajengwa sehemu gani?
 
Mkuu hii stendi inajengwa sehemu gani?
Kama mwenyeji wa nzega hiki kituo kinajengwa maeneo ya uswilu ila sasa kumepata umarufu kama maeneo ya stendi eneo hili lipo jirani na njia panda kati ya barabara inayokuja nzega mjini kutoka kitangiri, na bara bara iendayo shinyanga watu wa nzega wanaita barabara ya Uchama .
 
Taarifa ya mwezi wa tatu hadi mwezi wa Tisa mwaka 2016 juu ya shughuli mbali mbali zinazofanywa mojakwamoja na Ofisi ya Mbunge na Halmashauri ya Mji wa Nzega.
__________________

Ni takriban miezi tisa sasa tangu Mh Mbunge Hussein Mohammed Bashe apewe ridhaa na wananchi wa jimbo la Nzega mjini ya kuwawakilisha bungeni.

Katika kipindi hiki kifupi cha uwakilishi wake wa jimbo hili kuna miradi mingi ambayo imeanzishwa mengine tayari imekamilika na mingine ikiendelea na ipo kwenye hatua nzuri. Miradi hii imegawanywa katika sekta;

[emoji117] Uchumi
[emoji117]Afya
[emoji117] Elimu.
[emoji117] Maji
Kwenye sekta ya uchumi tuna miradi ifuatayo;

1. [emoji117] Stendi mpya ya mabasi Bulunde

2. [emoji117] Mgodi wa Namba saba Halisi

3. [emoji117] Fursa sawa kwa wote wa Airtel kwa kupitia Nzega Urban Trust Fund

4. [emoji117] Uwezeshwaji wa Mamantilie na ofisi ya Mbunge mojakwamoja

5. [emoji117] Mikopo kutoka Halmashauri ya asilimia 10% kwa makundi ya vijana na wanawake.

6. [emoji117] Mradi wa kutoa elimu ya ujasiriamali na kuwawezesha wananchi na rasilimali fedha kupitia shirika la TYEEO ( Tanzania Youth Enterprenurship and Empowerment Organization

7. [emoji117] Mikopo ya Pikipiki bodaboda kwa vikundi.

Kwenye sekta ya Afya kuna miradi ifuatayo;

1. [emoji117] Bima ya afya ya CHF

2. [emoji117] Kituo cha Afya cha Kijiji cha Nhobola Kata ya Mbogwe .

3. [emoji117] Ujenzi wa jengo la upasuaji kituo cha agya Zogolo Kata ya Nzega Ndogo

4. [emoji117] Mchakato wa kurudisha hospitali ya Wilaya kuja kwenye mamlaka ya Mji wa Nzega.

Sekta ya elimu ina miradi ifuatayo;

1. [emoji117] Mradi wa shule ya Bulunde ambao umelenga kuanzisha shule itakayotoa kidato cha 5&6.

2. [emoji117] Ujenzi wa majengo manne yaani madarasa 3 na ofisi ya walimu shule ya msingi Shalemwa.

3. [emoji117] Ujenzi wa madarasa mawili shule ya msingi maporomoko.

4. [emoji117] Ukarabati wa madarasa mawili shule ya msingi Kitengwe.

SEKTA YA UCHUMI:

1.[emoji117] Mradi wa stendi mpya ya mabasi Bulunde
__________________

Mradi huu umeshakamilika kwa asilimia 90% na ni moja kati ya miradi ambayo itazinduliwa na Mwenge tarehe 25.09.2016. Mambo ambayo tayari yameshakamilika katika mradi huu phase 1 ni;

[emoji810] Ujenzi wa kituo cha polisi

[emoji810] Ujenzi wa jengo la abiria yaani 'waiting hall'

[emoji810] Ujenzi wa vyoo vya abiria

[emoji810] Jengo la ofisi yaani 'Administration Block'

[emoji810] Miundombinu ya Umeme

[emoji810] Matenki ya Maji na miundombinu yake.

Shughuli zinazoendelea kwa sasa:
_________________

[emoji810] Ujenzi wa vibanda vya biashara kwa kupitia mfumo PPP ( Public Private Partnership ) ambapo kamati ya zabuni imeshaketi na kamati ya fedha imesharidhia na kubariki mikataba itayotolewa.

Katika mfumo huu wananchi watakua wanajenga vibada vyao na kurudisha gharama zao kwa kupitia makato yao ya kodi ya pango.

Kuanzia wiki ijayo wananchi wataanza kupewa mikataba.

2.[emoji117] Mgodi wa Namba saba Halisi.
_________________

Katika kutimiza ahadi yake ya kuwatafutia wananchi wake fursa za kiuchumi na kujiajiri, Mh Mbunge aliomba serikalini mgodi huu ambao hapo awali ulikua chini ya mwekezaji mmoja.

Serikali iliridhia ombi hilo na hatimae wananchi wakapewa eneo hilo kwaajili ya uchimbaji mdogo. Kwasasa eneo hilo lina takriban vijana 3000 ambao wanajishughulisha na uchimbaji na wana kipato halali.

3. [emoji117] Mradi wa Airtel fursa sawa kwa wote ambapo Airtel wametoa millioni 20

4. [emoji117] Mikopo kwa vikundi vya ujasiriamali vya Mamantilie ambapo mpaka sasa jumla ya vikundi 25 vimeshakopeshwa, na kupata mikopo isiyokuwa na riba.

5. [emoji117] Asilimia 10% ya mapato ya ndani ya Halmashauri fedha zinakopeshwa kwa vikundi vya wanawake na wanaume.

6. [emoji117] Mradi mkubwa ambao ni endelevu unaoendeshwa na shirika la TYEEO(Tanzania Youth Enterprenurship and Empowerment Organization ) likishirikiana na ofisi ya Mbunge . Katika mradi huu ambao upo jimbo zima wananchi watakua wana wanapewa elimu kwa muda wa miezi mitatu wakiwa wameandaliwa katika makundi ya watu wasiozidi 30 na baada ya miezi mitatu ya elimu ya ujasiriamali, wataanza kukopeshwa.

7. [emoji117] Mradi wa mikopo ya pikipiki za bodaboda ambapo jumla ya pikipiki 31 zimeshakopeshwa kwa vijana.

SEKTA YA AFYA:

1. [emoji117] Ujenzi wa jengo la upasuaji kituo cha afya Zogolo Kata ya Nzega Ndogo

2. [emoji117] Ujenzi wa nyumba ya Mganga katika kituo cha Afya cha Nhobola Kata ya Mbogwe

3. [emoji117] Ujenzi wa Zahanati ya Idudumo ambapo ofisi ya mbunge imechangi mifuko ya cement na Matofali ya ujenzi

4. [emoji117] Jitahada na mikakati inayoendelea ya kurudisha hospitali ya Wilaya kuja kwenye. mamlaka ya Mji.

5. [emoji117] Huduma ya Bima ya Afya ya CHF ambapo Mh Mbunge alikatia Kaya 200 zisizojiweza kwaajili ya huduma hii na wanachama wote wa chama cha bodaboda Nzega mjini.

SEKTA YA ELIMU :

1. [emoji117] Mradi wa Shule ya Bulunde ambapo ukikamilika utatoa nafasi kwa jimbo la Nzega kuwa na shule ya kidato cha 5&6. Phase 1 yaani awamu ya kwanza ya mradi huu imeshakamilika ambapo madarasa mawili yamejengwa. Phase 2 yaani awamu ya pili ni ujenzi wa bweni na vyoo vya bweni ndio unaendelea . Awamu ya kwanza imegharimu takriban millioni 40 fedha ambazo zimetoka mojakwamoja kwa Mh Mbunge.

2.[emoji117] Ujenzi wa nyumba ya mwalimu Mwanyagula 2 in 1.

3. [emoji117] Nyumba ya mwalimu shule ya Nhobola
4. [emoji117] Ujenzi wa madarasa matatu na ofisi ya walimu shule ya msingi Shalemwa . Ujenzi wa madarasa haya utawaokoa wanafunzi wanaotembea km 10 kwenda shule. Ikimbukwe kwamba shule hii ujenzi wake unafadhiliwa mojakwa moja na mbunge kwani ndio mwanzilishi wa shule hii baada ya kupokea maombi ya wananchi kuhusu watoto wao ambao walikua wakitembea km 10 kwenda kutafuta elimu.

5. [emoji117] Ujenzi wa madarasa matatu shule ya msingi maporomoko .

6. [emoji117] Ukarabati wa madarasa mawili shule ya msingi ya Kitengwe. Haya ni madarasa ambayo watoto walikua wanasoma kwenye sakafu ya vumbi.


7. [emoji117] Ujenzi wa madarasa mawili shule ya msingi ya Undomo.

8. [emoji117] Ulipiaji wa ada ya wanafunzi kama ifuatavyo;

[emoji810]Vyuo vikuu wanafunzi 14

[emoji810] VETA wanafunzi 19

[emoji810] SEKONDARI wanafunzi 34.

UJIO WA MWENGE TAREHE 25.09.2016
_________________

Ujio wa Mwenge katika Jimbo letu la Nzega Mjini utakuja kuzindua miradi ifuatayo;

1. [emoji117] Ujenzi wa stendi mpya ya mabasi

2. [emoji117] Mradi wa Bima ya afya kwa wazee waliozidi fikisha miaka 60 na zaidi

3.[emoji117] Kufungua Ofisi ya Serikali ya Kata katika kata ya Mbogwe.

4. [emoji117] Ujio wa Mwenge pia utatoa fursa kwa jimbo letu kupata msaada wa shillingi millioni 10 ili kusaidia jitiada za Mbunge za kuwawezesha wananchi kwa mikopo nafuu.

Lakini nimalizie kwa kutaja jitahada za Mh Mbunge ambazo anaendelea kuzifanya katika kuwaletea wananchi wake maendeleo;

1. [emoji117] Kurudisha eneo la uwanja wa ndege kwa wananchi ambapo tayari Mh Mbunge ameshaongea na waziri husika na tayari taratibu za kiserikali zinaendelea

2. [emoji117] Mh Mbunge ameshaongea na waziri wa elimu kuhusu madai ya walimu tofauti na mishahara yao. Tayari serikali imeshapokea maombi hayo na muda wowote kuanzia sasa walimu wataamza kulipwa madai yao.

3. [emoji117] Mh Mbunge ameongea na waziri wa nishati na madini kuhusu uwezekano wa kuongeza eneo la uchimbaji kitalu cha 3 kwenye mgodi wa Namba 7 halisi. Maombi haya yamepokelewa wizarani na maendeleo ni mazuri.

4. [emoji117] Maombi ya kuchukua majengo ya mchina kwenye kambi ya mkandarasi huyo ili kukigeuza kituo icho kuwa cha VETA. Tayari serikali imeshaachia majengo ya Tanroad.

5. [emoji117] Uwepo wa kituo pekee cha uwekezaji cha EPZ Kata ya Nzega Ndogo ambapo eneo tayari limeshapimwa na taratibu zingine za kiserikali zinaendelea.

6. [emoji117] Jitahada za kutatua kero ya maji. Suluhisho la muda mfupi tayari changamoto yake imeshatatuliwa ambapo takriban Tsh millioni 520,000,000/= zimeshapatikana kwaajili ya kujenga machujio mapya na kukarabati ya zamani.

Suluhisho la muda mrefu ni mradi wa Ziwa Victoria ambapo fedha zake zimeshapatikana kupitia Bank ya Exim India.

MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI JIMBO LA NZEGA MJINI.

Imeandaliwa na;

Katibu wa Mbunge Ofisi ya mbunge Jimbo la Nzega Mjini.View attachment 406099View attachment 406100View attachment 406101View attachment 406102View attachment 406103View attachment 406104
Umeandika vizuri mkuu ila kuna shirika moja World Vision limejitoa sana ktk wilaya hyo kutoa michango ya maendeleo ya jamii,nimejisikia vibaya kutoona hata umelitaja kwa uchache.au mashirika binafsi ni mwiko kuyasifia?wapeni na wao hongera zao mkuu!
 
Back
Top Bottom