TUSHIRIKISHANE Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Nzega

TUSHIRIKISHANE Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Nzega

Mradi wa Tushirikishane (JamiiForums yazindua rasmi mradi wa "Tushirikishane") umeanza rasmi jimbo la Nzega mjini chini ya Uongozi wa Mheshimiwa Mbunge Hussein Bashe

Tokana na misingi ya TUSHIRIKISHANE iliyoelemea katika kuwawezesha wabunge wa kuchaguliwa kutekeleza ahadi 4 kati ya jumla ya ahadi walizotoa wakati wa uchaguzi kwa urahisi kwa kushirikiana na wananchi; mada hii itatumika kuwasilisha, kujadili na kupeana taarifa ya kile kinachojiri Nzega mjini.

Ahadi walizochagua kufuatilia wananchi wa Nzega mjini kwenye mradi wa TUSHIRIKISHANE ni:

a. Kukamilisha ujenzi wa kituo kipya cha mabasi-Nzega

b. Ujenzi wa Nyumba ya Daktari-Kituo cha Afya Nhobora

c. Kukamilisha mpango wa muda mfupi wa upatikanaji wa Maji safi na salama-Nzega kwa kuongeza mita za ujazo 1300

d. Kukamilisha mabweni na madarasa ya kidato cha 5&6-Sekondari ya Bulunde​

View attachment 390312
Picha ya pamoja na washiriki toka Nzega. Waliokuwa wamekaa ni madiwani
Mada hii itatumika zaidi na Wana Nzega kutupa taarifa.

Baadhi ya Washiriki watakuwa:

1. Mh. Mbunge Hussein Bashe
2. Gideon Anyona (Katibu)
3. Josephat Sanga (Afisa habari Nzega)
4. Na washiriki wote wa Warsha hiyo na wale wote wenye mapenzi ya Maendeleo ya Nzega mjini.​

Karibuni...

[HASHTAG]#Tushirikishane[/HASHTAG] [HASHTAG]#Nzega[/HASHTAG]

Kufahamu majimbo mengine yenye mradi huu tembelea - JamiiForums yazindua rasmi mradi wa "Tushirikishane"
daaah hapa napitaa tuu
 
Viwanda je wakuu - kuna fikra za kuwekeza hapo ?
kiongozi ukitaji uwekejazi wa viwanda katika mji wa nzega karibu

ni sehemu nzuri kwa ujenzi wa kiwanda cha maziwa kwani wafungaji ni wengi kwaiyo maziwa yapo kwa wingi

Vile vile ujenzi wa kiwanda cha kusindika matunda hususani maembe, pia ni eneo zuri kwani maembe yapo kwa wingi sana kwaiyo hiyo ni Fulsa ambayo ipo wazi
 
Hilo suala la viwanda, mbunge aliyepita Kigwangala aliwambiaga atawajengea kiwanda cha maziwa wana nzega ili wauza maziwa wawe wanauza maziwa katika kiwanda hicho Sijui mipango ilishiaga wapi maana mpaka anaacha ubunge hatujaona hata eneo tu lilowekwa jiwe la msingi kuwa kiwanda kinajengwa hapa
 
IMG-20161027-WA0046.jpg
Taarifa fupi :

Leo kulikua na kikao na ziara fupi ya maofisa ofisi ya mbunge, wenyeviti wa mitaa, wataalam wa maji kutoka wizarani na wadau wa maendeleo mjini.

Kikao kilihusu taarifa ya muendelezo wa mradi wa maji wa muda mfupi na mrefu yaani ule wa Lake Victoria.

Msafara ulianzia ofisi ya Mbunge kwenda Uchama kwenye eneo la uzalishaji maji.

Wajumbe walipokelewa na mtaalam engineer, na baada ya hapo taarifa ya muendelezo wa mradi wa maji ikatolewa kwa wajumbe pamoja na wajumbe kutembezwa kwenye mitambo inayozalisha maji.

Lengo la ziara:
____________

Ziara hii ililenga kuwapa elimu ya ufahamu wajumbe wote kama viongozi ambao wapo karibu na jamii ili kuwawezesha kupitisha ufahamu huo kwa wananchi na kuwaeleza wananchi nini haswa kinachoendelea na kinachotegemewa.

Ofisi ya mbunge inawashukuru wajumbe wote waalikwa walihudhuria.

Imetolewa na;

Katibu ofisi ya Mbunge.
 

Attachments

  • IMG-20161027-WA0048.jpg
    IMG-20161027-WA0048.jpg
    133.5 KB · Views: 49
Nashukuru kwa uzi huu wa tushirikishane, unaotupatia fursa kujadili maendeleo ya wilaya nzega
Kwanza niwapongeze na kuwashukuru sana kama mtoto wa kuzaliwa wa nzega, kwa juhudi zenu juu ya maendeleo na ustawi wa nzega yetu, nafarijika kuona ndugu zangu wakina Shija, mhoja n.k sasa wanapata nafasi ya kuonja maendeleo ya nzega yetu Kia kutengenezewa na kuboreshewa miundo mbinu na huduma mbalimbali kupitia nyinyi wadau, kwa heshima na taadhima nasema asante Sana,
Nimepita thread na nimeona jinsi Mambo yanavyosonga pale nyumbani nzega,
Nimpongeze mbunge wangu Hussein Bashe kwa kutokuwa mbinafsi na kukubali kushirikiana nanyi katika kuiendeleza nzega yetu ,naamini ana nia ya dhati ya kuitoa nzega mahali fulani na kuipeleka mahali pengine pazuri zaidi kijana huyu wa mzalendo wa nzega,

Mimi pia ni mdau wa maendeleo ya nzega kwa maana nashiriki kikamilifu katika kubuni mipango mbalimbali ya kupunguza umaskini na kuiendeleza nzega yetu,
Nimeandika maandiko kadhaa mojawapo lile nililoandika kuhusu kusaidia kupunguza (uharibifu wa chakula)kuoza kwa maembe wakati wa msimu wa maembe na kuichukua kama fursa kwa wakulima wenye maembe kufaidika zaidi na miembe yao na kuwasaidia kiuchumi zaidi tofauti na ilivyo sasa, nimeishirikisha organization moja ya kijerumani andiko hilo na ninasubiri mchakato wake, pia Wiki ijayo nitaenda ofisi za bakhressa kumshirikisha andiko hili, na kwa mdau yeyote wa maendeleo ya nzega atayehitaji naweza kumshirikisha andiko hili, nia yetu ni moja, kuipeleka nzega mahali flani
Niseme tena asanteni
 
Niko tayari kushirikiana na mtu yeyote bila kujali itikadi yeyote
Tunashukuru kwa mchango wako chief1, tunakukaribisha katika mjadala huu vile vile karibu ushee na sisi hilo andiko lako kwa ajili ya maendeleo ya watu wa nzega.
 
wadau wa maendeleo katika jimbo la nzega mjini, bwana kigulube, na bwana furaha wakiuliza maswali mafupi yenye tija kwa mtaalam wa Maji na kupatiwa majibu kuhusu tatizo la maji lililopo sasa katika jimbo la nzega mjini.

Hii ilikuwa ni ziara fupi ya kuangalia maendeleo ya mradi wa mpango wa uboreshaji miundombinu ya maji ili kuondoa tatizo la maji lililopo sasa katika jimbo la nzega mjini.

Ziara hii iliyofanywa tarehe 27/10/2016, na ofisi ya Mbunge, akiwa na wenyeviti wa mitaa wote wa nzega mjini pamoja na wadau wa maendeleo katika jimbo la nzega mjini,
 
Sasa huyo mtaalam mbona naye haeleweki atasemaje bwawa la Uchama linaweza kukizi maitaji ya nzega kwani mda huu maji bado yapo ajiulizi kuwa maji mpaka sasa yapo hapo kwa sababu hayatumiki ndio maaana kayakuta hapo
 
Mawazo ya Chief1 ni safi sana, Nzega ina watu elite wengi nashauri mbunge atafute namna ya kuwashirikisha na hawa ndo technical team bila kujali mambo ya siasa na team hii itaweza kumsaidia kimtazamo wa kuinua uchumi wa wilaya na kuibua fursa na uwekezaji. Mbunge awembunifu kutafuta watu kama hawa kwa ajili ya maendeleo ya NZG
 
TARIFA YA MAENDELEO YA MRADI KWA TUSHIRIKISHANE KWENYE JIMBO LA NZEGA

MJINI KATIKA KIPINDI CHA MWEZI SEPTEMBA MPAKA OCTOBA 2016

Mradi wa Tusirikishane katika Jimbo la Nzega ulizinduliwa rasmi tarehe 11/08/2016……Lengo kuu

la mradi huu wa ni kujenga mazingira wezeshi kwa viongozi wa kuchaguliwa kutimiza sera na

ahadi walizotoa wakati wa uchaguzi mkuu wa Octoba 2015 kwa urahisi. Vilevile Tushirikishane

ina lengo la kuchochea Halmashauri (Serikali za Mitaa) kutoa kuongeza ufanisi katika utoaji wa

huduma bora kwa jamii.

Katika warsha ya uzinduzi, washiriki ambao walitokana na wapiga kura wa Jimbo la Nzega Mjini

walipata fursa ya kupitia sera na ahadi zilizotolewa wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu na

Ndugu Bashe Hussein, akiwa kama mgombea wa Ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi

(CCM). Zoezi hili lilifanyika ili kuchagua ahadi chache zitazopewa kipaumbele na kusimamiwa

chini ya mradi wa Tushirikishane kwa miezi tisa.

Warsha hii iliyoendeshwa kwa siku tatu katika ukumbi wa Tanganyika, mjini Nzega, ilijumuhisha

wawakilishi wa makundi mbalimbali ya jamii walioshiriki katika uchaguzi mkuu uliopita hususani

wale waliopiga kura katika Jimbo la Nzega. Makundi hayo ni pamoja na:

 Viongozi wa Kisiasa (Madiwani)

 Wajasiriamali

 Boda boda

 Mama lishe

 Watumishi wa Serikali

 Wafanya biashara

 Walemavu

 wamama wa nyumbani

 Vijana wa jinsia zote

 Viongozi wa dini

AHADI ZILIZOPEWA KIPAUMBELE CHINI YA TUSHIRIKISHANE

Katika warsha iliyotangulia ufunguzi wa Mradi, wananchi na viongozi wa kuchaguliwa walipata

fursa ya kupitia ahadi zilizotolewa na mshindi wa kiti cha ubunge-Jimbo la Nzega Mjini, Mh.

Hussein Bashe na kuchagua ahadi nne (4) za kipaumbele ambazo zitasimamiwa chini ya mradi

wa Tushirikishane. Ahadi zilizochaguliwa ni hizi zifuatazo:

1. Kusimamia ukamilishaji wa ujenzi wa kituo kipya cha mabasi Nzega

2. Kuhakikisha ujenzi wa nyumba ya Daktari katika kituo cha Afya Nhobora unakamilika

3. Kusimamia ukamilishaji wa mpango wa muda mfupi wa upatikanaji wa maji safi na

salama –Nzega kwa kuongeza mita za ujazo 1300

4. Kukamilisha mabweni na madarasa ya kidato cha tano na cha sita katika shule ya

sekondaro Bulunde.

Ifuatayo hapa chini ni taarifa ya maendeleo ya utekelezaji wa ahadi zilizochaguliwa hapo juu.

MAENDELEO YA MRADI

1. Kusimamia ukamilishaji wa ujenzi wa kituo kipya cha mabasi Nzega

Katika tarifa iliyopita ya kipindi cha mwezi Agosti mpaka Septeba ilielezwa kuwa ujenzi wa

banda la kupumzikia wageni, vyoo pamoja na kituo cha polisi vilikuwa vimekamilika. Vile vile

nguzo za umeme zilikuwa tayri zimesogezwa katika eneo la kituo cha mabasi. Shughuli ya

kuchimba kisima cha maji kwa mpango wa matumizi ya mda mfupi, wakati maji ya bomba

yakisubiliwa kufika katika eneo la kituo hicho ulikuwa unaendelea. Na zabuni ya ugawaji wa

maeneo ya ujenzi wa vibanda vya biashara katika eneo la stendi ulikuwa mbioni kuanza.

MAENDELEO YA MAPYA KATIKA KIPINDI CHA MWEZI SEPT. – OKT. 2016

Kuanzia tarehe 17/10/2016 Halmashauri ya Mji wa Nzega ilianza kutoa fomu kwa ajili ya

maombi ya zabuni ya ujenzi wa vibanda vya biashara katika kituo kipya cha mabasi Sagara

Nzega. Zoezi hilo limekamilika tarehe 19/10/2016 na hatua inayoendelea sasa ni kupitia

maombi ya wazabuni ili kupata washindi. Mara tu baada ya kutangaza washindi, ujenzi wa

vibanda unapaswa kuanza mara moja.

2. Kuhakikisha ujenzi wa nyumba ya Daktari katika kituo cha Afya Nhobora unakamilika

Tarifa ya kipindi kilichopita ilizungumzia kuhusu chagamoto ya kiuongozi iliyopelekea ujenzi

kusisimama. Hakukuwa na Mtendaji wa kijiji ambaye ni mmoja wa watia saini muhimu katika

kuidhnisha pesa iliyoko katika akaunti ya Kijiji itolewe Benki. Mtendaji huyu alikataliwa na

wanakijiji kutokona na kukosa imani na uwezo wake katika kutekeleza majukumu ya kiutendaji

katika kijiji cha Nhobola.

MAENDELEO YA MAPYA KATIKA KIPINDI CHA MWEZI SEPT. – OKT. 2016

Mtendaji wa kijiji aliyekataliwa na wanakijiji wa Nhobola alisimamishwa kazi na Mkurugenzi wa Mji Nzega na kuamriwa akabidhi ofisi kwa uongozi wa kata ya Mbogwe. Kwa hiyo, siku ya

ijumaa ya tarehe 14/10 /2016, Mtendaji wa kijiji alikabidhi ofisi kwa mtendaji wa kata ya

Mbogwe, na Siku ya tarehe 17 /10 /2016, Mtendaji wa kata ya Mbogwe alikabidhi ofisi hiyo kwa

Mwenyekiti wa kijiji cha Nhobola ili Mwenyekiti wa kijiji aweze kuitisha kamati ya kijiji kukaa na kujadili maendeleo ya ujenzi wa nyumba ya Daktari.

Kamati ya kijiji ilifanikiwa kukaa na kujadiliana kwa mafanikio juu ya suala la maendeleo ya

ujenzi wa nyumba ya Daktari. Iliafikiwa kuwa pesa itolewe benki kwa ajili ya kununua vifaa vya kuendeleza ujenzi. Manunuzi yalifanyika na vifaa tayari vimefikishwa eneo la ujenzi. Mpaka sasa hakuna changamoto nyingine inayozuia ujenzi kuanza. Mara tu ujenzi ukianza itafanyika ziara itakayomhusisha Katibu wa Mbunge na kisha kuleta taarifa kupitia jukwaa la WhatsApp na mnakasha wa maendeleo ya mradi kwa Jimbo la Nzega Mjini uliopo JamiiForums.com..

3. Kusimamia ukamilishaji wa mpango wa muda mfupi wa upatikanaji wa maji safi na

salama –Nzega kwa kuongeza mita za ujazo 1300

Kwenye taarifa ya kipindi kilichopita ilitaarifiwa kuwa utekelezwaji wa mpango huu ulikuwa bado

haujaanza kutokana na ukosefu wa pesa. Fungu la utekelezwaji wa mpango huu linategemewa

kutoka serikali kuu.

MAENDELEO YA MAPYA KATIKA KIPINDI CHA MWEZI SEPT. – OKT. 2016

Pesa ya awali ya kwa ajili ya kuanza utekelezwaji wa mradi wa maji, kiasi cha shilingi milioni

mia mbili (TZS 200,000,000/=) imetolewa na serikali mwezi wa tisa. Jambo lililofanyika

mwanzoni mwa mwezi huu wa kumi 2016 ni kupima kiwango cha maji kinachoingia katika eneo ambalo maji husafiswa kabla ya kwenda kwa watumiaji. Hili limefanyika ili kufahamu ujazo unaoingia kutoka bwawa la Uchama na Kilimi. Pia kuangalia ujazo unaotoka kwenye eneo ambalo maji husafishwa ili kwenda kwa wanainchi. Lengo la zoezi hili ni kutambua uwiano uliopo baina ya ujazo unaongia na kutoka kwa ili kupata makadirio yanayoendana na uhalisia wa mahitaji halisi ya ukubwa wa matanki ambayo yanatakiwa kujengwa. Vilevile zoezi litawezesha kujua ukubwa wa mashine zinazotakiwa kusukuma maji. Na iwapo machine
zilizopo hazitosheleza basi kuangalia uwezekano wa kununua mashine zingine.

Tathmini na upembuzi wa mashine tayari umekamilika. Kwa sasa wataalamu wako katika hatua ya kukarabati chujio za maji. Kati ya chujio mbili zilizokuwa katika marekebisho, moja ilianza kufanya kazi siku ya tarehe 27/10/2016. Vile vile mafundi wameanza ukarabati wa matenki ya maji ambayo yalikuwa hayafanyi kazi. Ukarabati umeanza kwa tenki lililopo eneo la Pakingi na maeneo mengine

4. Kukamilisha mabweni na madarasa ya kidato cha tano na cha sita katika shule ya

sekondaro Bulunde.

Taarifa ya maendeleo ya mpango kazi huu wa mradi wa Tushirikishane kwa jimbo la Nzega

Mjini kwa mwezi Agosti mpaka Septemba 2016 ilionyesha kuanza kwa ujenzi wa vyoo katika

mabweni ya wanafunzi na kuinuliwa kwa kuta za jengo la bweni mpaka kufikia usawa wa lenta

MAENDELEO YA MAPYA KATIKA KIPINDI CHA MWEZI SEPT. – OKT. 2016

Ujenzi wa vyoo pamoja na uinuaji wa kuta za jengo umekamilika. Hatua iliyobakia ni kujenga

shimo ambalo litakuwa linatumika kuhifadhia maji machafu kutoka katika vyoo hivyo.

CHANGAMOTO ZILIZOPO ZA UTEKELEZAJI WA MIPANGO KAZI

Changamoto zilizopo katika kusimamia Mpango-Kazi unaoongoza utekelezaji wa ahadi nne

zilizochaguliwa na wana-Tushirikishane na kuridhiwa na Mbunge Mh. Hussein Bashe ni

muingiliano wa kiutendaji kati ya Serikali Kuu na Halmashauri kiasi cha kuvuluga na kusitisha

ratiba ya shughuli za Halmashauri. Mathalani Watendaji wakuu wa Halmashauri wanapokuwa

katika majukumu mengine kama kuratibu mbio za mwenge, kwa namna moja au nyingine

inaathiri utejelezaji wa ahadi za Tushirikishane kama vile stendi. Pia suala la Mtendaji wa kijiji

cha Nhobola kusimishwa kazi liliathiriki maendeleo ya ujenzi wa nyumba ya Daktari.

Imeandaliwa:

Joseph Sanga

Afisa mawasiliano wa mradi-Nzega
 
OK. Nawapongeza kwa hill. Ila inatakiwa jitihada zaidi ya kuongeza High school zifikie at least 6 kwa wilaya nzima pia vyuo 2. Hii itasaidia kuongeza wigo wa elimu kwa wananzega pia uchumi utakua. Tusisahau kukaribisha wawekezaji wa viwanda wengi zaidi
 
Tarifa ipo vizuri hongera afisa Mawasiliano, katibu wa Mbunge, na Mbunge ushirikiano wenu unaonekana mzuri sana endeleeni hivyo hivyo kwa kasi i hii naimani miradi yote mtatekeleza kwa wakati, na hata sisi wadau tunakosa maswali safi sana
 
IMG_20161105_105321.jpg
IMG_20161105_105425.jpg
ujenzi wa nyumba ya Daktari katika kituo cha Afya Nhobora

MAENDELEO YA MPANGO HUU

ujenzi uliokuwa umesimama kutokana na changamoto zilizojitokeza ambazo zimeelezewa katika katika tarifa ya mwezi Agosti mpaka Septemba, na mwezi Octoba zishatatuliwa na sasa ujenzi unaoendelea kama picha inavyoonekana .
 
IMG_20161105_101235.jpg
IMG_20161105_102102.jpg

Ukamilishaji wa ujenzi wa kituo kipya cha mabasi Nzega

MAENDELEO YA MPANGO HUU


Leo tarehe 05/11/2016, umeanza uchimbaji wa kisima cha maji katika kituo kipya cha mabasi Nzega hii ni hatua ya awali ya kuhakikisha upatikanaji wa Maji safi na salama katika eneo la kituo kipya cha mabasi, kipindi wakisubilia unganishaji wa Maji ya mbomba ambayo miundombinu yake bado kufika katika eneo la kituo hiki kipya cha mabasi sagara nzega.

Pichani ni baadhi ya Watalamu wataohusika na uchimbaji wa kisima hicho.
 
IMG_20161105_112540.jpg
IMG_20161105_112711.jpg
Kukamilisha mabweni na madarasa ya kidato cha 5&6- katika shule ya Sekondari Bulunde

MAENDELEO YA MPANGO HUU

Uinuaji wa boma la mabweni hayo umekwisha kamilika kama picha inavyoonyesha , hatua inayosubiliwa kwa sasa ni upauaji wa majengo hayo.
 
Back
Top Bottom