TUSHIRIKISHANE Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Nzega

TUSHIRIKISHANE Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Nzega

Safari moja huanzisha nyingine ndugu step, na penye nia basi hakuna linaloshindikana na imani watu wa nzega tukiungana kwa pamoja basi upo uwezekano wa kupatikana shule nyingine ya kidato cha tano na cha sita zaidi ya hii Bulunde.
 
Usemacho bwana sanga nia kweli kinachoitajika bwana bashe atafute wakazi wa nzega waliopo nje ya nzega mfano waliopo dar wakae chini wajadili mambo yao ni aje watafanikisha maendeleo ya nzega kama hivyo kuongeza shule za kidato cha tano na cha wakazi wa nzega wakichangia walicho nacho basi shule zitakiwepo
 
Thread #88 ina Changamoto.Utajuaje kuna wizi wa Dawa za serikali?Nami katika wale waliokwenda Dukani ana utaalam wa kuzitofautisha dawa za umma na zile za kibiashara?
Alafu kama Mbunge anatoa Pesa za Umeme kwa Sungusungu,accounting yake inakuwaje?Kwa Nini zisiingie kwenye Mfumo rasmi?Ndani Zahanati ina account benki,Halmashauri ina account pia--haamini mfumo?
 
Thread #88 ina Changamoto.Utajuaje kuna wizi wa Dawa za serikali?Nami katika wale waliokwenda Dukani ana utaalam wa kuzitofautisha dawa za umma na zile za kibiashara?
Alafu kama Mbunge anatoa Pesa za Umeme kwa Sungusungu,accounting yake inakuwaje?Kwa Nini zisiingie kwenye Mfumo rasmi?Ndani Zahanati ina account benki,Halmashauri ina account pia--haamini mfumo?
kiongozi pengine tuwekane sawa tu katika suala la madawa, dawa zote zinazoletwa na serikali ziende katika vituo vya afya zina alama zake si mpaka uwe mtaalam ndio uweze tofautisha hata wewe ukielekezwa tu utajua alama ya MSD huwa ipo hiyo moja,

Kingine suala la sungusungu, vikundi vingi vya sungusungu, vina mfumo wao wa kuhifadhi pesa si vikundi vyote vya sungusungu vina account bank , vipo vikundi vya sungusungu ambavyo pesa yao wanaitunza kwa mtindo wa kukopeshana hawaipeleki bank

Nazani nimeondoa utata uliokuwa nao kiongozi.
 
IMG_20161108_172503.jpg
IMG_20161108_172503.jpg
IMG_20161108_170654.jpg
IMG_20161108_173403_1.jpg
mpango wa muda mfupi wa upatikanaji wa Maji safi na salama-Nzega kwa kuongeza mita za ujazo 1300

MAENDELEO YA MPANGO

Leo tarehe 08/11/2016 machujio ya maji wawili yaliyokuwa yana karabatiwa katika chanzo cha maji bwawa la Uchama ukarabati wake umekamilika

Machujio hayo yana uwezo wakuchukua lita za maji milioni moja na laki mbili , Siku ya kesho tarehe 09/11/2016 yatafanyiwa majaribio

Vile vile mashine za kusukuma maji nazo Siku ya leo zimefanyiwa marekebisho lengo ni kuwezesha mashine zote tatu zinazopatikana kati chanzo cha maji bwawa la Uchama ziweze kufanya kazi

Ikumbukwe hapo awali mashine mbili tu ndio zilikuwa zinafanya kazi.
 
IMG_20161108_173644.jpg
IMG_20161108_173728.jpg
hili ni bwawa la Uchama ambalo ndio litaanza kutumika sasa kuhudumia wakazi wa nzega baada ya bwawa la kilimi lilikuwa likitumika awali kusimama tumiwa

Picha hapo juu ni muonekano tofauti tofauti wa bwawa la Uchama ambalo sasa linafanyiwa usafi wa kuondoa uchafu ambao unaonekana katika picha
 
Miye nauliza tu hayo marekebisho yenu ya mashine za maji bado tu haziajakamika tunaitaji maji jamani Siku ya pili leo mji wote wa nzega hatuna maji
 
Miye nauliza tu hayo marekebisho yenu ya mashine za maji bado tu haziajakamika tunaitaji maji jamani Siku ya pili leo mji wote wa nzega hatuna maji
IMG_20161109_170449.jpg
IMG_20161109_170449.jpg
Nazi embe ukarabati uliokuwa unafanyika Jana umekamilika na leo hii machujio mawili ya maji katika bwawa la Uchama yameanza majaribio vile vile mashine zilizokuwa zinafanyiwa matengenezo zimekamika hivyo Kuna baadhi ya maeneo leo hii yameanza kupata maji

Tunaomba mrejesho wako tu kipindi maji yakianza kutoka uje utuambie je maji yanayotoka sasa yana utofauti na yale ya awali ikiwa wingi wake, kasi yake pamoja na ubora wake yani usafi wa Maji
 
IMG-20161110-WA0023.jpg
ujenzi wa nyumba ya Daktari katika kituo cha afya Nhobola

MAENDELEO YA MPANGO HUU
Jengo limekamilika kama linavyoonekana katika picha hatua ilnayofuatia ni upauaji.
 

Attachments

  • IMG_20160918_180544.jpg
    IMG_20160918_180544.jpg
    230.5 KB · Views: 45
IMG_20161113_085334.jpg
ujenzi wa kituo kipya cha mabasi-Nzega

MAENDELEO YA MPANGO HUU

uchimbaji wa kisima cha maji, umekamilika kama picha inavyoonekana hatua iliyobakia nikufunga pampu ili kisima kianze kufanya kazi .
 
Kwa hatua ya maji niwapongeze maji yanatoka masafi ila bado maeneo mengine maji bado mgao haueleweki ingekuwa vizuri bwana josephat sanga ukawa unatuwekea na ratiba ya mgao wa Maji hapa ili tuweze kujua zaidi yote kwa yote nikupongeze kwa ufuatiliaji mzuri na kutupa tarifa kwa wakati
 
Thread #88 ina Changamoto.Utajuaje kuna wizi wa Dawa za serikali?Nami katika wale waliokwenda Dukani ana utaalam wa kuzitofautisha dawa za umma na zile za kibiashara?
Alafu kama Mbunge anatoa Pesa za Umeme kwa Sungusungu,accounting yake inakuwaje?Kwa Nini zisiingie kwenye Mfumo rasmi?Ndani Zahanati ina account benki,Halmashauri ina account pia--haamini mfumo?
Mara nyingi mifumo rasmi ya Serikali ina gharama kubwa kitu cha Tsh 1 kinakuwa mara mbili ama tatu ya gharama halisi.

Jamii zetu zina mifumo ya asili na mara nyingi mifumo hiyo imekua ya manufaa sana kuliko rasmi ya kiserikali.
 
Hapo juu Mbunge yupo sahihi ni vyema kuangalia f fursa zote, hii ni pamoja na mifumo iliyopo ili lengo litimie kwa haraka zaidi. Napenda kuwapongeza kwa swala la maji, natumaini upatikanaji wake utawezesha kubadili mazingira. Hamasisheni upandaji miti na usafi wa makazi kama anavyofanya RC Makonda Dar, uboreshaji mazingira utasaidia sana jamii hata kuwa na mitazamo yenye afya. Ni lazima idara ya misitu ibadilike hapa.
 
TARIFA FUPI YA MWEZI NOVEMBA 2016 KUHUSU MAENDELEO YA MRADI WA TUSHIRIKIANE KATIKA JIMBO LA NZEGA MJINI


A) ukamilishaji wa ujenzi wa kituo kipya cha mabasi Nzega

Kazi ambayo inaendelea kwa sasa ni uchimbaji wa kisima, kisima kimekwisha chimbwa tayali, hatua iliyobakia kwa sasa nikufunga pampu, ili kisima kianze kufanya kazi, vile vile mchakato wa kutangaza washindi wa zabuni ajili ya ujenzi wa vibanda vya biashara unaendelea na mda wowote kuanzia sasa washindi watatangazwa ili waweze kuanza ujenzi wa mabanda ya biashara.


B) Ujenzi wa nyumba ya Daktari katika kituo cha afya Nhobola

mradi huu kwa sasa upo katika hatua ya upauaji wa jengo, hii ilikuwa ni hatua inayofuatia baada ya ujenzi wa boma ukiwa umekwisha kamilika, kama tarifa picha ya maendeleo ya mpango kazi huu inavyoonyesha, kwaiyo hatua iliyopo sasa na inayosubiliwa ni upauaji wa jengo hilo, kamati ya ujenzi pamoja na uongozi wa kijiji ulishakaa na kujadili makadirio ya pesa inayoitajika kwa ajiri ya kazi ya upauaji wakakubaliana hivyo basi mda wowote kuanzia sasa kazi ya upauaji inaanza.

C) Kukamilisha mpango wa muda mfupi wa upatikanaji wa Maji safi na salama-Nzega kwa kuongeza mita za ujazo 1300

Hatua iliyopo sasa ni majaribio na urekebishaji wa miundombinu ya maji, ikiwa ni mabomba, matanki kazi inayofanyika ili kuweza kuangalia ufanisi unaokuwepo baada ya kazi ya ukamilishaji wa matengenezo ya machujio mawili ya maji kukamilika, vile vile uongezaji wa mashine mbili za kumpampu maji kuongezewa, na kuwa mashine tatu, zitakazo fanya kazi kwa pamoja

tofauti na awali ambapo chujio lilikuwa moja na mashine iliyokuwa ikifanya kazi ya kupampu maji ilikuwa moja, vile vile baadhi ya matanki ya maji yalikuwa hayafanyi kazi, hivyo sasa zoezi lililopo ni kukarabati miundombinu hiyo ya maji ili zoezi la majaribio liweze kuendelea na kuendelea kukarabati maeneo ambayo ya taonekana bado yana tatizo ili badae zoezi likamilike na wakati wa nzega waweze kupata maji kwa uhakika zaidi.


D) Kukamilisha mabweni na madarasa ya kidato cha 5&6-Sekondari ya Bulunde

Mradi huu kwa sasa umesimama hii ikiwa ni hatua ya awali ya ukamilishaji wa kuinua jengo kukamilika , hivyo hatua inayosubiliwa kwa sasa ni upauaji wa mabweni hayo ambayo ujenzi wake wa boma umekamilika kama habari picha za maendeleo ya mpango kazi huu zinavyoonyesha.

hivyo basi wahusika wa ujenzi kwa sasa wapo katika zoezi la kuanza kazi ya upauaji wa mabweni hayo, kwaiyo kazi ya upauaji ikianza tutakuja wapatia mrejesho wa maendeleo hayo.


Imetolewa

Afisa mawasiliano Nzega.
 
Back
Top Bottom