Mjadala: Waziri wa mambo ya nje ya Marekani anamkuta Paul Makonda na hatia ya kuua watu! Kwanini anakumbatiwa sana na Rais Magufuli?

Huyo waziri wa mambo ya nje ya Marekani anaongea kama nani?. na ni nani kampa hayo mamlaka wakati ni waziri tu wa nchi moja mwanachama wa UN?.

Nani kamkuhumu au anatarajia kumhukumu Donald Trump kwa kutuma wanajeshi wamuue General Kassim kule Iraq?, tujitahidi tuachane na huu utumwa wa mawazo.

Marekani haijawa ni nchi ambayo mwanadamu kapewa na Mungu kwa kuambiwa kwamba wao ni wasamehewa dhambi na wenye sifa maalum ya kuhumu dunia nzima.
 
Mike Pompeo Boss wa taasisi wa Kijasusi Marekani amekuja na hoja nzito ya zuio la RC Makonda kuingia Marekani bila kuweka wazi sababu.

Pengine, Pompeo na watetezi wa Pompeo hapa Tanzania watusaidie kuwa fair.

Taarifa ya CiA chini na Gina Hispel ilithibitisha pasi chembe ya mashaka mwana wa Mfalme wa Saudia alihusika na kutoa order ya kuuwawa Jamal Khashoggi.

Pompeo mbona hajawahi kutoa zuio la Mohamed bin Salam aka MBS kuingia Marekani? Au kutaka ICJ ichukue mkondo wa jambo hili, ili baada ya hapo, awe na moral authority katazo la kwa Paul Christian Makonda.??


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Marekani wanatuonea wivu
Wajinga wengi nchi hii pamoja na huyu eti nchi ya kwanza duniani kwa kila kitu inaionea wivu nchi ya mwisho duniani kwa kila kitu, sawa na Mo Dewji (anisamehe) amwonee wivu Matonya kwa style yake ya kupata fedha.
 
Watetezi wa muuaji hamkai mbali!
 
Je,ni kweli makonda ni muuaji?Kama ndiyo basi hata hiyo kupigwa ban kuingia US ni kidogo mno,waje wamchukue wakampoteze wajuako!
 
CHADEMA sema poo! Makonda amewashinda! mmemchongea wee, mmesaidiwa na Gwajima mpaka yeye akaita poo, nyinyi mpo tu! Mmemshindwa sasa mnafikiri ya marekani itawasaidia! Marekani walichunguza wakakuta ushahidi wenu unapwaya wameyaacha!
Makonda miaka inakwenda bado anachapa kazi! Na anazidi kupendwa! Ita poo! Mmemshindwa.
 
Makonda: a big disgrace for this country and the fact that he is being protected by the regime shows that he is a mere front man.
 
Je kama alitumwa kuuwa na Mamlaka za juu ?
 
Magufuli ni wazi alikuwa anamkingia kifua Makonda kwa sababu yeye ndiye alikuwa akimtuma kwenda kuua watu aliyokuwa akiwaona kama maadui zake.

Kwa mantiki hiyo basi, Magufuli na Makonda wote walihusika katika uhalifu wa kuua watu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…