Mjane aolewa na wanaume watatu kwa pamoja akiwemo shemeji yake

Mjane aolewa na wanaume watatu kwa pamoja akiwemo shemeji yake

Oldmantz

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2023
Posts
704
Reaction score
1,457
mjane-pic.jpg


Nellie akiwa na waume zake watatu

Ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni’, Nellie kutoka Nigeria ameitoa ile dhana ya mwanaume kuoa wake wengi bali mwanamke pia anaweza kuolewa na wanaume wengi baada ya kuolewa na wanaume watatu.
Jimmy, Hassan na Danny ndio waume wapya wa Nellie na wameamua kuwa marafiki baada ya kumuoa na kuishi naye kwa pamoja.

Kati ya wanaume hao Hassan ni ndugu wa marehemu mume wake ambaye alibahatika kuzaa naye watoto wawili. Mume wa Nellie alifariki dunia kwa ajali ya gari, hata hivyo mdogo wake huyo alikuwa akiishi nyumbani hapo kama mwanafamilia.

Baadaye alimpata mume wake wa pili na wa tatu katika nyakati tofauti na ambao wote wanaishi nyumba moja na alisema anawahudumia wote na pia imani kwamba hawatamuacha.

Nellie ambaye anafanya biashara ya kuuza magari amesema, "Naitwa Nellie, na mimi ndiye nimeweka rekodi katika kijiji hiki nikiwa na wanaume watatu. Nimeishi na wanaume hawa watatu kama waume wangu kwa miaka mitatu. Nilikuwa na mume ambaye tulikuwa pamoja kwa miaka minane ambaye alikufa katika ajali ya gari,” amesema.

“Baada ya kufariki niliachwa na kaka yake Hassan na tuliendelea kuishi nyumba moja kama ilivyokuwa kabla ya marehemu mume wangu kufariki, hata hivyo alinionyesha upendo na mwishowe nikampenda,” aliiambia Afrimax English.

Akimzungumzia Danny anasema alikuwa amemaliza tu elimu yake na hakuwa amepata ajira alipokutana naye alimwonyesha upendo na kumpeleka nyumbani kwake, ambapo wanaume wengine wawili walimkaribisha.

Nellie alimpata Jimmy akiwa ameketi pekee yake huku akionekana akiwa mpweke, kisha alimuomba wazungumze kwani aliona kama mtu mwenye mawazo mengi.

“Nilihitaji mtu wa kunifariji na kuniambia maneno mazuri, na pia nilihitaji mtu wa kuzungumza naye, aliniambia maisha yake, siku hiyo kila mtu alienda njia yake, lakini tuliendelea kuwa marafiki. Tulikubaliana na historia yetu ya maisha na kuishi kama mume na mke," Jimmy alisema.

Nellie anajivunia kukidhi mahitaji ya waume zake na kujigamba kuwa hawawezi kumdanganya kwa sababu anawapenda wote sawa.

"Kuishi na wanaume watatu kunanifanya nijisikie furaha sana, na ninaweza kuthibitisha kuwa wanaume wangu pia wana furaha kwa sababu wana kila kitu wanachotaka, na nina hakika hawatanidanganya kwa sababu naamini ninakidhi mahitaji yao," Nellie alisema.

Mwananchi​

 
Huyu bingwa wa mizagamuano. Lazima ladha ni sawa nachai ya rangi isiyo na sukati
 
Niliona hii YouTube nikajua masihara😳 mikuyenge mitatu yote inakukojolea tu? Aisee... Foursome hiyo
Haya ndio maendeleo ya masuper woman bwana...dah anaburrudika vilivyo anachichagulia tuu leo nitaka threesome foursoume au two some🤣🤣🤣
 
Duh! Huyu mwanamama amefanya kufuru kubwa Sana itabidi tumjengee sanamu la heshima zake.
 
Nilitegemea nione picha za watu fulani hivi local (waporipori) sana wakiwa ndani ya mavazi ya magome ya miti hivi (kama wale wanaosalimiana kwa kutoa mashuzi), kumbe hao watu wanaonekana ni wajanja kabisa (kutokana na mavazi na muonekano wao) sasa kimewakuta nini?!!!!!!
 
Back
Top Bottom