Huyu Mjane alikua anaishi kwenye nyumba ya serekali. Baada ya mumewe kufariki alipewa notisi ya kuhama.
Alifanya jitihada kubwa ya kuiomba Serikali imfikirie na imuachie akae katika nyumba hio ambayo inaonekana walitumia gharama kubwa kuiremba na kuitia mapambo ya kila aina. Hata hivyo ombi lake lilitupiliwa mbali.
Kwa hasira na yeye akang'oa kila kitu kuanzia tiles, gypsum, switch za umeme na hata rangi za ukutani.
Hivyo sasa hivi anatafutwa ili awajibike.
Wito wangu kwa serekali, imuonee huruma mjane huyu na si vizuri kuwanyanyasa wajane na mayatima.
Kabla mke wa aliyekuwa jaji mkuu wa Zanzibar, marehemu Mkusa Isack Sepetu, Salma Mkusa alitoa malalamiko akidai kwamba shirika la nyumba Zanzibar lilimtaka kuhama na kukabidhi funguo za nyumba waliyokuwa wakiishi na marehemu mume wake maeneo ya michenzani block namba 9.
Aliiomba serikali na shirika la nyumba kutafuta utaratibu sahihi na wa haki juu ya hilo. Alisema hakuwa na deni na mume wake hakua nalo. Anadai majungu mengi yalipikwa kwamba nyumba inatakiwa na serikali na ni mtu mkubwa anahitaji nyumba hiyo.
Duu walikuwa na hasira kweli maana si kwakuvunja kule, hapo ni funzo kwa viongozi ukipewa nyumba ya serikali unajenga na yako siku haupo familia isipate shida kama hizo
Katika msiba ukiacha wa Nyerere ambao nimeona Tanzania ikilia sana ni wa Omar Juma,ilituuma sana ila behind the scene huyu baba hakutendewa haki ya uhai wake[emoji29]
Aliyekuwa makamu wa Raisi awamu ya Mkapa (Omar Ali Juma), baada ya kufariki familia yake ilitolewa kwenye nyumba Oysterbay.
Serikali hailei wajane, inawahifadhi watumishi wake tuu. Utumishi ukiisha huduma zinakatwa in exception to President, Jaji mkuu na Spika.
Jaji Mkusa Sepetu(1974-2020) hakuwa Jaji Mkuu wa Zanzibar licha ya kuwa aliwahi mara kadhaa kukaimu nafasi ya Jaji Mkuu.
Hadi mauti yanamkuta mwezi february mwaka huu,Jaji Sepetu alikuwa jaji wa Mahakama kuu ya Zanzibar.
Jaji mkuu wa Zanzibar ni Jaji Othman Makungu.
Je aliyefanya uharibifu huu ni Mke mkubwa ama Mdogo Manake Marehemu Jaji Sepetu aliacha Wajane wawili.
Jaji Mkuu Ramadhani aliwahi kukalamika baada ya kustaafu miaka kadhaa iliyofuata ulinzi wa serikali uliondolewa nyumbani kwake mpaka ikabidi yeye mwenyewe kwa pesa zake mfukoni awe anamlipa mlinzi wa Co. Binafsi.