Mjane wa aliyekuwa Jaji wa Zanzibar, Marehemu Mkusa Isack Sepetu anatafutwa baada ya kuharibu nyumba ya shirika la nyumba Zanzibar

Mjane wa aliyekuwa Jaji wa Zanzibar, Marehemu Mkusa Isack Sepetu anatafutwa baada ya kuharibu nyumba ya shirika la nyumba Zanzibar

Sasa nae alishindwa nini kujenga nyumba yake mpaka jengo la serikali aweke tyles? hicho ni kiranga chake alipe tu
Halafu hao watoto ni watu wazima nao wanangángánia nyumba ya serikali sasa wanadhani aliyeteuliwa akakae wapi?

Kwanza nyumba za serikali zinakarabatiwa na serikali si ajabu huyu mama alitaka kuipora kiujanja nyumba hiyo ya serikali.

Kama kweli kafanya hivyo halali yake kunyea debe ili liwe fundisho na kwa wengine.

Huyu mama alijisahau na sidhani kama kweli alikuwa mke wake huyo Sepetu labda alikuwa nyumba ndogo, na ni makosa yake alisahau kumshauri huyo mume wake wajenge nyumba,wauza mchicha tu wana nyumba uweje yeye asiwe na nyumba hadi mauti yanamkuta,mimi namlaumu huyo mama pamoja na wanaojiita watoto wa sepetu
 
Jaji Mkusa Sepetu(1974-2020) hakuwa Jaji Mkuu wa Zanzibar licha ya kuwa aliwahi mara kadhaa kukaimu nafasi ya Jaji Mkuu.
Hadi mauti yanamkuta mwezi february mwaka huu,Jaji Sepetu alikuwa jaji wa Mahakama kuu ya Zanzibar.

Jaji mkuu wa Zanzibar ni Jaji Othman Makungu.

Je aliyefanya uharibifu huu ni Mke mkubwa ama Mdogo Manake Marehemu Jaji Sepetu aliacha Wajane wawili.
Atakuwa mdogo tu kwa mbwembwe na kelele hizo za mitoto mijitu mizima inayolilia nyumba za serikali
 
Inachekesha sana, makamu wa rais, na jaji wa mahakama kuu hawajajenga nyumba!!!


Angekuwa mjane wa mwl mada ingekuwa na wachangiaji 10,000 wakiwaponda walifeli na wanalipwa laki 2.


Inawezekanaje ukafika ujaji na umakam wa rais hauna kighorofa hata kimoja?

Wafukuzwe kabisa ili wengine akili zao zijiseti kuwa wanathaminika wakiwa kazini tu.
 
Sio nyumba ya serikali per se, ni nyumba ya shirika la nyumba la zanzibar kama vile NHC kwa upande wa bara.

Wao walikuwa wapangaji tu inaonekana mkataba ulikuwa kwa jina la marehemu ila wamekuwa wakilipa kodi kama kawaida.

Huu ni unyanyasaji ata bara NHC wakati wa Nehemia kuna watu walianza mtindo huo wakiona kuna nyumba ipo maeneo mazuri na mzazi amefariki kuna watu wanawafuata mameneja wamaeneo husika wanatoa ongo wanafamilia wanaanzishiwa mizengwe kwenye ku renew mkataba au wataongezewa kodi hata kwa zaidi ya 150% in one go unashangaa mtu analipa double ya jirani zake.

Nehemia alikuja stuka baadae naona akapiga mkwara hizo tabia zikapungua hila bado zipo kiasi fulani ni mameneja tu wenye tamaa.

Ndio kilichomkuta huyo mjane sio nyumba ya serikali maalum ya kuweka viongozi ambapo kazi ikiisha unatakiwa umpishe anaekuja ingekuwa ivyo sawa na sidhani kama wangebisha ni nyumba ya kupanga ndio maana akasema kodi wanalipa.

Hii nchi ina watu wenye tamaa, wivu na wenye kutumia nafasi zao kupokonya haki za wengine ni unyanyasaji tu.
 
inachekesha km yule mtoto mkubwa kabisa wa kiume analialia eti ooh sie tutaenda wapi,bwege sana hama kwenu wewe katafute kwako
hata mimi kanishangaza na mama kasema ohh mimi na watoto tutaenda wapi mitoto mijitu mizima ile hata haya haina loo

huyo mama gaidi huwezi haribu nyumba ya serikali hivyo akamatwe atandikwe na viboko.Mumewe ndie alikuwa mfanyakazi wa serikali na akifariki nyumba anatakiwa apewe mfanyakazi mwingine wa serikali .Sio mali binafsi hiyo
 
Mtu amefikia vyeo cha ujaji mkuu, hakuweza kujenga miaka yote hiyo?
uongo huyo mama atakuwa ama alikuwa akipangisha hiyo nyumba ya NHC AU ATAKUWA ALIJENGA HALAFU KULE ALIKOJENGA AKAWA ANAPANGISHA

Huyo muongo mkubwa kaharibu mali ya serikali
 
FAE51678-4668-42D7-AF5C-2D336DAEF270.jpeg


Inawezekana kama taifa tuna tatizo la selective listening au tumejazwa na bias za majungu. Watu wengi tuna tabia ku interpret kile tulichotaka kusikia tofauti kabisa na kinachoongelewa.

Nyumba ni mali ya ZHC (Zanzibar Housing Corporation) ni ya kupanga sio ya serikali ambayo mfanyakazi anapewa.

Wao ni wapangaji hapo, kupata lazima uombe ZHC alieingia nao mkataba kafariki (pichani). Kuna kigogo anaitaka ndio sababu ya kuvunjiwa contract na kutolewa lakini si kwa sababu ni nyumba maalum ya wafanyakazi wa serikali tu.
 
Jaji Mkuu Ramadhani aliwahi kukalamika baada ya kustaafu miaka kadhaa iliyofuata ulinzi wa serikali uliondolewa nyumbani kwake mpk ikabidi yeye mwenyewe kwa pesa zake mfukoni awe anamlipa mlinzi wa Co. Binafsi.


Aiseeeh.....!
 
Sio nyumba ya serikali per se, ni nyumba ya shirika la nyumba la zanzibar kama vile NHC kwa upande wa bara.

Wao walikuwa wapangaji tu inaonekana mkataba ulikuwa kwa jina la marehemu ila wamekuwa wakilipa kodi kama kawaida.

Huu ni unyanyasaji ata bara NHC wakati wa Nehemia kuna watu walianza mtindo huo wakiona kuna nyumba ipo maeneo mazuri na mzazi amefariki kuna watu wanawafuata mameneja wamaeneo husika wanatoa ongo wanafamilia wanaanzishiwa mizengwe kwenye ku renew mkataba au wataongezewa kodi hata kwa zaidi ya 150% in one go unashangaa mtu analipa double ya jirani zake.

Nehemia alikuja stuka baadae naona akapiga mkwara hizo tabia zikapungua hila bado zipo kiasi fulani ni mameneja tu wenye tamaa.

Ndio kilichomkuta huyo mjane sio nyumba ya serikali maalum ya kuweka viongozi ambapo kazi ikiisha unatakiwa umpishe anaekuja ingekuwa ivyo sawa na sidhani kama wangebisha ni nyumba ya kupanga ndio maana akasema kodi wanalipa.

Hii nchi ina watu wenye tamaa, wivu na wenye kutumia nafasi zao kupokonya haki za wengine ni unyanyasaji tu.
Kama ni kweli huyo mama basi hajatendewa haki lakini vip kuhusu kuifanyia marekebisho?

Lakini inakuwaje mtu ana nafasi kubwa kwenye serikali anashindwa kujenga nyumba za kawaida za kustiri familia yake?

Mambo mengine watumishi wa umma wanapaswa kujitambua mapema. Mtumishi wa umma unapaswa kujua kazi hairithishwi ukianza kazi jaribu kuona kama vile kesho hutakuwepo hivyo unatengeneza misingi ambayo hata kama hutakuwepo itasaidia wategemezi wako....
 
Ukiwa Kwako Heshma Ipo Hata Ukijenga Banda Tu
Ndiyo Maana Viongozi Wa Sasa Hivi Hata Akiteuliwa Hataki Nyumba Ya Serikali
Bora Aendelee Na Maisha Yake Uswazi
 
Kiswahili kinanitesa, Wens Sepetu anaingiaje hapa?? Ninapata taabu Kaka WA Wema halafu mjane. Hey unamaanisha nini au ulitaka kusema huyu ni mjane wa kaka yake Isaac Sepetu aliyekuwa baba yake Wema iwe kwenye mabano Hakika nimetabika kupata manana yako. Sada kisheria amefanya kosa name akipelekwa mahakamani atapatwa name hatia ya uharibifu wa Mali y'all shirika au serikali . Charge hiyo kwa kumuonea huruma other wise atakuwa na kesi ya uvunjaji
 
Kama ni kweli huyo mama basi hajatendewa haki lakini vip kuhusu kuifanyia marekebisho? Lakini inakuwaje mtu ana nafasi kubwa kwenye serikali anashindwa kujenga nyumba za kawaida za kustiri familia yake?...
Hayo ni mambo ya kawaida NHC/ZHC wanaruhusu wateja kutengeneza nyumba zao jinsi wapendavyo (mikataba yao sio kama private) au hata kufanya extension nje unaruhusiwa kama serikali ya mtaa wakikupa kibali.

Kikubwa kwao unachotakiwa ni kulipa kodi yako tu na kutoa extension ya mkataba sio tatizo kwa familia ata kama mkataba waliingia wazazi washakufa watoto mnatumbaliwa kama warithi wa mkataba kama mmekulia humo ndani.

Alichofanyiwa huyo mjane ni uonevu hata bara huu mchezo ulitaka kukithiri Nehemia akastuliwa wafanyakazi wa chini wakaanza uoga, hila bado upo upo unakuta mtu anapigwa kodi kubwa hatari ukiona ivyo kuna mtu anataka nyumba.

Halafu kwa sasa NHC kama familia imekalia nyumba kwa muda mrefu sasa hivi wanaruhusu kuinunua kabisa na Lukuvi anatilia mkazo hilo jambo wapate hela wajenge nyingine watu wapate makazi.

Kujenga ni swala la mtu binafsi kutokana na mazingira yake.
 
Wakuu naomba tujadili suala hili kwa kina.

Huyu mjane alikua anaishi kwenye nyumba ya serekali. Baada ya mumewe kufariki alipewa notisi ya kuhama..
Nimecheka sana nilikuwa sijamuelewa awali jamaa aliyelalamikia MB 16, sijui Simu yake itakatika vipande[emoji3] [emoji1]
YULE MJANE ANA HATIA YA KUTENDA KOSA, KAZI NI KWAKE AJIANDAE TU HUKUMU
 
Back
Top Bottom