Mjane wa aliyekuwa Jaji wa Zanzibar, Marehemu Mkusa Isack Sepetu anatafutwa baada ya kuharibu nyumba ya shirika la nyumba Zanzibar

Nikisema kurithi sio mali ya familia hiyo ni kwamba mnapewa priority by default kuendelea na mkataba. Sio Tanzania tu ipo ivyo duniani kote.
Mkataba wowote wa kupanga duniani kote huji ona kipengele chochote kinachotamka kwamba utaendelea kuwa mpangaji by default mkataba ukiisha!!! Hakipo na hakitakuwepo

mpangaji unatakiwa uusome mkataba uuelewe.USIANGALIE SIJUI TAMKO LA WAZIRI ohh sijui mila na desturi zilizozoeleka !!! soma mkataba wa kupanga unasema nini

Huo mkataba wa kupanga sio wa huyo mama wala sio wa familia.ALIYEINGIA MKATABA NI JUDGE SEPETU full stop.Hao wengine hauwahusu wawe wake wawe watoto.Wakihitaji wanaomba tu kama watu wengine wakikubaliwa sawa wakikataliwa sawa sio nyumba yao ya urithi hiyo.Kwanza hata sina uhakika kama mirathi ilishafunguliwa au bado .Lkini hata kama mirathi ilishafunguliwa hiyo nyumba haimo kwenye vitu vya mirathi kuwa watarithi nyumba ya kupanga ya Jaji Sepetu!!!

Frustration sio sababu ya kuvunja mkataba au kuharibu mali za serikali hasira zake alitakiwa akazimalizie kwingine sio kwenye mali ya serikali.

kama kufiwa wanawake wazanzibari wengi tu mbona wanafiwa yeye sio wa kwanza na mikataba ya nyumba ikiisha hufunga virago au wao kuomba upya kuwa wapangaji ziwe za serikali au za watu binafsi hawafanyi uharibifu kwenye hizo nyumba.

No way adakwe tu na aonyeshwe cha mtema kuni
 
Uko sahihi .Tatizo baadhi ya hizi famnilia kubwa hudhani maisha yanatakiwa yabaki vile vile mhusika akistaafu au kufariki .Waendelee kuishi maeneo maarufu ya watu wazito yenye hadhi kubwa nk

Tanzania bara viongozi wetu wengi wakubwa wanajielewa na wanalielewa sana hili wengi hawasumbui kabisa isipokuwa wachache

Raisi Nyerere alipostaafu alitimka Dar es salaam akatimkia zake kijijini Butiama kuishi mkoa wa Mara

Raisi Mkapa alikuwa akiishi ikulu Dar es salaam alipostaafu akatimkia zake kijijini Lushoto Tanga

Raisi Kikwete alikuwa akiishi ikulu Dar esa salaam baada ya kustaafu akatimkia zake kijini Msoga Bagamoyo mkoa wa Pwani

Hao ni maraisi wanatimkia vijijini kuwa ya mjini yaishe sembuse huyo mjane na hao watoto wake

Si vizuri kukomaa tu ohh mimi nilikuwa mke wa marehemu jaji so what akifariki wewe sio jaji wala wanao biashara imeshafungwa hiyo
 
Jaji mpaka anafariki hana hata kibanda cha kujisitiri huwa wanajisahau sana na kota za serikali
 


☝ Hiyo ni sehemu ya mkataba wa hapa ninapoishi soma unavyosema nikifa nini kitatokea ni shirika la nyumba la serikali.

Nenda katembelee maeneo ambayo kuna nyumba nyingi za NHC uone wajane waliobaki kwenye nyumba ambazo mikataba waliingia waume zao ni common practice ata Tanzania.

Acha kubisha kutokana na hisia zako deal with the facts.

Good Day
 
-baada ya mapangaji kufariki mkataba unarithiwa na mke(level 1) ,naamini sheria za upangaji ZHC pia kipengele hiki kipo.
-la msingi nini kilichopelekea ZHC kuisitisha mkataba na kumnyima mjane haki ya kuendelaea kupanga miezi michache baada ya kufiwa na mume?
 

Apparently not kwa mujibu wa ZHC wao wanamtambua mumewe tu. Story kamili hiyo hapo ☝️ you be the judge.
 
Baba yake wema alikua na familia ingine( mama wa kambo wa wema) na ndio alikua mke mkubwa ...hiyo familia ingine ndio marehem Mkusa (anashare baba na wema) alikua mmoja wa watoto .....so mvunja nyumba ni mke wa mkusa ( wifi ya wema)
 
mkataba mbona uko wazi. Unasema MAY BE INHERITED hausemi SHALL BE INHERITED maana yake sio lazima urithiwe ndio maana limetumika neno MAY na sio SHALL

Ungesema SHALL BE INHERITED ungemaanisha lazima urithiwe na hao waliotajwa

Huo mkataba haukupi haki ya kisheria kuwa lazima urithiwe unasema MAY BE!!! Rudia kuusoma!!! Usije ukapata shida mbeleni
 
inachekesha km yule mtoto mkubwa kabisa wa kiume analialia eti ooh sie tutaenda wapi,bwege sana hama kwenu wewe katafute kwako
Hata mimi nilishangaa kabisa, yule si ni Baba mzima anakuwa na maisha yake? Ndiyo yale matoto yakulelewa kwenye hotpot
 
Atakuwa mdogo tu kwa mbwembwe na kelele hizo za mitoto mijitu mizima inayolilia nyumba za serikali
Anaonekana kabisa ni mdogo [emoji23][emoji23][emoji23] maana ukiiona video anavyoongea nikama kuna mashemela wamemtenga
 
Sasa huo ukarabati wa nini nyumba ya shirika? Kwanini hizo pesa asijengea yake? Tatizo wengi wakipanga humo wanajisahau, tunaopanga kwa watu zile kashikashi zinatuzibua akili tunajenga hata mabanda na kuishi humo
 
CCM zenji vipi? mbona manyanyaso ..sawa ahame lakini mpeni basi walau mwaka ajipange!!
 
Huyo mtu mkubwa wa serikali mwenye haki kuliko huyo mama nafikiri atarekebisha tu mambo madog madogo hayo kwake...
 
Naam, kama hauna nyumba, basi weka TZS za kutosha benki. Ukiondoka, TZS zinanunua nyumba chapuchapu. Mfanyakazi wa serikali akifariki, nafasi yake inachukuliwa na mwingine. Na huyo mwingine anahitaji nyumba ya serikali. Inaumiza kwa walioachwa lakini ndio utaratibu huo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…