Mjane wa Mrema atoswa, familia yapinga wosia uliachwa na Mrema. Mjane apokonywa nyumba ya Salasala

Watanzania wenzangu je mmejiuliza kwa nini hawa wazee husainishwa mikataba ya mirathi mara tu baada ya kuoa?

Mbona Vijana wakioa ama kuolewa hakunaga mambo ya makaratasi ya mirathi endapo mmoja atandoka ??
 
kutokana na hali ya Mzee ilivyokuwa kuna haja ya review ya huo wosia kwa kweli. Yaani kumpa mtori Marehemu siku mbili tatu unataka nyumba ya mil 500+ aisee hilo suala ni gumu mno.

Kama ni makochi, TV mashuka yote kila kitu apewe mjane ila Nyumba aiwache kama alivyoikuta, hiyo ni mali ya watoto hata kama ni watu wazima hakuna sheria inazuia.
 

Sasa wewe unataka kutoka kwenye msingi wa hoja. Hapa tupo kisheria zaidi tukiweka pembeni mambo ya hisia, utu uzima na busara.
 
Sasa wewe unataka kutoka kwenye msingi wa hoja. Hapa tupo kisheria zaidi tukiweka pembeni mambo ya hisia, utu uzima na busara.
kisheria vipi kaka, yaani uolewe wiki 4, afu unataka ukombe haki za Marehemu alizochuma miaka yote ya uhai wake - kisa tu umemwogesha na kumtunza akiwa mgonjwa...hilo hapana.

Babu yangu Mzaa mama alifiwa na bibi yetu (mkewe); sisi wajukuu nikiwemo na mimi nilitaka Babu yetu aoe ili apete wa kumtunza...tulipewa kazi ya kumtafutia mchumba - cha ajabu kila tunayemleta home anasema ana jicho kubwa, kichogo krefu, mfupi - yaani tukachemka kumbe anasongesha muda mbele - hakutaka.

Alivyochoka sana alikuja mama mmoja kuishi naye kwa hiari ili amtunze ila Babu alimwambia kabisa akifa atapewa kitanda na mshuka tu, vingine vyote mali ya watoto, yule bibi akakubali - Baada ya miezi kadhaa babu akafariki dunia.

Siku ya kikao cha familia yule mama akasema hivyo hivyo alivyoambiwa na Babu, Balaza la familia kwa kuheshimu maneno ya Marehemu ambayo hayakuandikwa popote wakamzawadia nyumba hiyo hiyo na mashamba... akawa bibi yetu. (ila condition hawezi kuitoa urithi ama kuiuza)

So wajane jishusheni, utakachopewa na familia ndicho hicho hicho, usianzishe ligi kwenye mali za wenyewe !! Mke huwa ni mke wa Kwanza tu wengine wanaofuata ni vimada tu.
 

Huo ni utashi wa familia yenu. Nasijui kama umefuatilia wakati una ninukuu nilikua namjibu kitu Gani huyo jamaa kuhusu hii hoja.

Unaelewa Nini unapoambiwa Mke? Si unaona huyo Mama unaemwita Bibi alikuja kumtunza Babu yenu bila hata kuwa na cheti Cha ndoa na Bado akaambulia vitu vingi kuzidi hata wanaoachiwa urithi Kwa wosia na kuwa na vyeti vya ndoa?

Mie sitetei mjane Wala Marehem, nnachokiona ni hicho kichochoro Cha watu kusema wosia wa marehem iliandikwa wakati akiwa hayuko vizuri wakati hapo hapo mtu huyo huyo alipofanya maamuzi ya ndoa hawakumzuia kwamba hayuko sawa kichwani.
 
bi mkubwa anataka nyumba na Prodo la Mzee !! yaho mengine ya kwenu.
Ila dunia ya leo robo tatu ya binaadam wameshakatika mishipa ya aibu. Inapokuja suala la mali au fedha hakuna aibu tena. Unaona jinsi hata wanasiasa wanavyojishusha hadhi na kujiita ''chawa wa fulani'' ili tu wapate kula. Huko nyumba za ibada ndiyo kabisaa, viongozi wake wameshapagawa na fedha.
 
Mkibioshohajawahi kuaminika kokote.....haamilki
Ndo yamemkuta Sasa ilikuwa timing tuu
 
Kukbe hamjui yule dada hana mpango wa mali alikuja kwa nia moja nayo ni umaarufu sasa mrema anamali gani hana kitu .
Atarudi kwake na ataendelea na maisha yake .
 
Sasa hao nao wanadhani hizo mali zitawafikisha wapi? Maana mali za marehemu huwa hazikai labd kama aliwashirikisha kuzitunza na kuziendeleza toka mwanzo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…