kisheria vipi kaka, yaani uolewe wiki 4, afu unataka ukombe haki za Marehemu alizochuma miaka yote ya uhai wake - kisa tu umemwogesha na kumtunza akiwa mgonjwa...hilo hapana.
Babu yangu Mzaa mama alifiwa na bibi yetu (mkewe); sisi wajukuu nikiwemo na mimi nilitaka Babu yetu aoe ili apete wa kumtunza...tulipewa kazi ya kumtafutia mchumba - cha ajabu kila tunayemleta home anasema ana jicho kubwa, kichogo krefu, mfupi - yaani tukachemka kumbe anasongesha muda mbele - hakutaka.
Alivyochoka sana alikuja mama mmoja kuishi naye kwa hiari ili amtunze ila Babu alimwambia kabisa akifa atapewa kitanda na mshuka tu, vingine vyote mali ya watoto, yule bibi akakubali - Baada ya miezi kadhaa babu akafariki dunia.
Siku ya kikao cha familia yule mama akasema hivyo hivyo alivyoambiwa na Babu, Balaza la familia kwa kuheshimu maneno ya Marehemu ambayo hayakuandikwa popote wakamzawadia nyumba hiyo hiyo na mashamba... akawa bibi yetu. (ila condition hawezi kuitoa urithi ama kuiuza)
So wajane jishusheni, utakachopewa na familia ndicho hicho hicho, usianzishe ligi kwenye mali za wenyewe !! Mke huwa ni mke wa Kwanza tu wengine wanaofuata ni vimada tu.