Mje mtushauri vijana wa miaka 25 hadi 40

Mje mtushauri vijana wa miaka 25 hadi 40

Shida yenu ubishi! Tukiwaambiaga mnasema tunawaonea gere sababu mnapendwa na mishangazi!

Tulieni vijana! Tuheshimuni tuwashauri yaliyo mema.

Mnahisi nyie ndio wa kwanza kupitia hizo stage kweli? Au mnadhani nyie ndio mmegundua utamu wa pombe na utamu wa lile tendo? Tumepita humo humo na sisi vijana, tukiwashauri kitu ni kwa kuwa tunakijua! Shida mnaona sisi tumelost kwahiyo hatuwezi waambia kitu.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Habari.

Nimekuja na mada hii kwa wazoefu wa maisha mnaweza kutusaidia sisi vijana wadogo ambao tuko kwenye miaka 23 hadi 40.

Maisha yetu yamekuwa ni ya matarajio mengi sana lakini uhalisia wa hayo matarajio ni tofauti na tunavyofikiria au tulivyoahidi.

Umri umefika tumejikuta tuna wake ,watoto na kazi au vitu vya kawaida ambavyo hatukuwa na mipango navyo labda tuseme tunaona tumefeli .

Tuliwaza kumiliki Nyumba Kali,Gari nzuri ,kuwa na kazi yenye mshahara wa kutosheleza mahitaji maishani na ndugu lakini haijawa hivyo.

Kwa wazoefu wa maisha.

Tunaomba mtushauri kitu gani cha ziada tufanye hili tuweze kufikia lengo la maisha wakuu
Mkipata fedha pigeni maji kwa kwenda mbele. Mambo ya nyumba na viwanja achaneni navyo, tena vipo siku zote. Biblia inatumbia nyumbani ni mbinguni, hivyo kujenga hapa duniani ni sawa na kujenga njiani.
Aidha, wala tusikubali kuhama nyumbani kwa ajili ya kujitegemea. Yani hizi familia zetu kijana akifikisha miaka 25 tayari wanataka ahame nyumbani akajitegemee. Naona utaratibu huu unakiuka hata vitabu vya dini, Yesu yupo kwa Baba yake zaidi ya miaka elfu 2 iliyopita na maisha unaendelea.
 
pombe ni kwa masikini hata biblia inalitambua hilo

wapeni pombe masikini...
Mkuu kuna pombe hata maskini kijijini kwenu wote wakijiunga hawawezi nunua, biblia ni hadithi tu zenye mkanganyiko , daudi alilewa akacheza na nuhu walilewa pia kina suleiman na kina yesu kwa mujibu wa hiyo hadithi kumbe ni makanjanja tu😁
 
Tokea nilipo jifahamu niliacha kujifananisha na yeyote...Mimi unique kwa hivi hivi nilivyo pesa zitakuja tuuu...!

Sitamani kuwa yeyote yule kwani naamini Kila mwenye pumzi anapambana na vita ya nafasi yake ambayo wengine vita hizi ni za siri awajapenda yeyote ajue.

Ndio linapo kuja ule msemo "Kila mtu anao ukrasa kwenye maisha yake ambao hapendi usomwe na yeyote"😭​
 
Nidhamu ya pesa
Usiishi maisha ya watu wengine ridhika na ulichonacho
Malengo ya muda mrefu yatakusaidia kujua wapi upo na nn ufanye usitak kilakitu leoleo

Starehe sio kitu Cha maana sana ukiniona haziendani na malengoyako acha
 
Back
Top Bottom