Mjema: Ziara ya Chongolo na Ujumbe wake nchini China italeta Wawekezaji na faida nyingi sana kwa Taifa

Mjema: Ziara ya Chongolo na Ujumbe wake nchini China italeta Wawekezaji na faida nyingi sana kwa Taifa

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2019
Posts
377
Reaction score
435
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa wamefanya ziara ya takribani siku 10 nchini China iliyoanza Aprili 17, 2023 na kutamatika Jana Aprili 28, 2023. Chongolo aliambatana na Katibu wa Itikadi na Uenezi Ndugu Sophia Mjema, Katibu wa Oganaizesheni Ndugu Issa Gavu na Wajumbe wengine wa Halmashauri Kuu ya CCM.



Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Ndugu Sophia Mjema Jana Ijumaa Aprili 28, 2023 katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba Jijini Dar es Salaam baada tu ya msafara kurudi nchini, ameeleza mafanikio makubwa ya ziara hiyo nchini China.

Mjema amesema ziara hiyo ilikuwa ya kikazi na mafunzo ya kubadilishana uzoefu mbalimbali kati ya CCM na Chama Tawala cha China CPC na kutembelea majimbo matatu ya Beijing, Hebei na Guangzhou.

Ziara hiyo ilijikita kubadilishana uzoefu na China katika maeneo ya elimu na ufundi stadi, kilimo, afya, viwanda, habari na mawasiliano.


Ziara hiyo imewafikisha kwa Viongozi wakubwa wa CPC na masuala ya Nje akiwemo na Mkurugenzi wa Kamisheni ya Mambo ya Nje wa Kamati Kuu ya CPC Bwana Wang Yi, Waziri wa Idara ya Mambo ya Nje ya CPC Bwana Liu Jianchao na wengine wakubwa kwenye majimbo ya Hebei na Guangzhou ambapo wamebadilishana uzoefu namna walivyoweza kubadilisha uchumi wao na kuwa moja ya Mataifa yaliyofanikiwa sana duniani.

Mjema amesema ziara hii itashusha sana Wawekezaji wengi kutoka China watakaokuja nchini kuwekeza kwenye elimu stadi, kilimo, afya na kubadilishana uzoefu namna China walivyoweza kuondoa umaskini na kuinua uchumi wao.

Kwa mujibu wa Mjema amesema ziara hii ni matunda ya ziara za Rais Samia nje ya nchi na uboreshaji wake wa diplomasia ambao sasa umefanya Tanzania kufunguliwa milango ya kiuchumi na uwekezaji kote duniani.
 
Ni jambo jema

Mbowe naye kaahidi kuleta Wawekezaji wengi kutoka Africa Kusini
 
Back
Top Bottom