Mji wa Goma (mashariki mwa DRC) watanda giza

Twin_Kids

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2016
Posts
3,692
Reaction score
5,647
Toka jana tarehe 23 Januari 2025, mida ya saa mbili usiku, mji wa Goma uligubikwa na giza.

Ni baada ya taarifa za kifo cha aliekuwa mkuu wa mkoa wa Kivu kasikazini Mejor General Chirimwami. Leo subuhi, maji,umeme na huduma za mitandao havikupatikana kabisa,jambo lililozua hofu kwa wakazi wa mji huo.

Wengi wenye uwezo, kwa kuhofia kuporwa mali zao na jeshi la FARDC na wazalendo, wamepanda ndege na kuelekea mikoa mingine ikiwemo Kinshasa. Uongozi wa serikali umewataka wananchi kuwa watulivu na kuliamini na kuliunga mkono jeshi lao, ila wanaonekana kukosa imani, baada ya kukosa huduma hizo za msingi.

Pamoja na hali hiyo, inasemekana pia eneo la tambalale lililopo umbali wa km 20 kutoka mji wa Goma, tayari lipo mikononi mwa M23,maana kwa sasa wanapigana kutoka pande tofauti tofauti(kwa makundi),na inaonekana FARDC hawajui waanzie wapi.

Kwa wanaojaribu kudadavua mambo, wanahisi lengo la M23 ni kuifunga mipaka ya DRC na Rwanda, jambo litakalosababisha waliozingilwa wasiweze kutoka. Na hali ikiwa hivi kweli, kuna dalili sa majeshi ya Tanzania,Malawi na South Africa kudhalilika,maana kwa hali iliyopo, M23 bado imaendelea kuwaomba wakae mbali na jeshi lipigane lenyewe, vinginevyo na wao watashughulikiwa.

Ikumbukwe, kwa kuzingilwa kwa mji huo, sababu ni kwamba jeshi hilo lisiweze kupata msaada wa kijeshi kutoka nje. Na baada ya kuona hali si shwali, FARDC iliamua kusafirisha badhi ya siraha zake kupitia njia ya maji kuelekea Bukavu. Picha, ni hali ya Goma kwa sasa.

Goma1.jpg
Goma2.jpg
 
Attachments

  • Goma3.jpg
    Goma3.jpg
    19.4 KB · Views: 4
Tangu nijue DRC iko kimkakati na UN inaratibu. Sina cha kusema.
Poor Africa inaangamia kwa kukosa viongozi waadilifu. Shame on us
Na wameiruhusu Rwanda kuichukua mazima Goma yote ili iwe chini yake.

Sababu ni kwamba tayari Rwanda ni emerging economy na stable country.

Hivyo ni kuichukua Goma na kuifanya iwe safe itainufaisha Rwanda wenyewe na wakubwa wa Dunia.

Tukumbuke magari ya dizeli na petroli huko kwa wakubwa mwisho ni 2030 hivyo malighafi ni lazima ianze kuandaliwa sasa.

M23 ni proxy tu ila nyuma yake yapo majeshi ya Rwanda.

Akili ni nywele.
 
Tukumbuke magari ya dizeli na petroli huko kwa wakubwa mwisho ni 2023 hivyo malighafi ni lazima ianze kuandaliwa sasa.

M23 ni proxy tu ila nyuma yake yapo majeshi ya Rwanda.

Akili ni nywele.
Hii maneno iseme kwa sauti ya chini sana. Nadhani umenielewa.
Huu ni mchezo kama michezo mingine.
Shame on us African na viobgozi wetu
 
Na wameiruhusu Rwanda kuichukua mazima Goma yote ili iwe chini yake.

Sababu ni kwamba tayari Rwanda ni emerging economy na stable country.

Hivyo ni kuichukua Goma na kuifanya iwe safe itainufaisha Rwanda wenyewe na wakubwa wa Dunia.

Tukumbuke magari ya dizeli na petroli huko kwa wakubwa mwisho ni 2030 hivyo malighafi ni lazima ianze kuandaliwa sasa.

M23 ni proxy tu ila nyuma yake yapo majeshi ya Rwanda.

Akili ni nywele.
Wamarekani ni Wapumbavu sana...
America wako na Kagame..
Wao ndo wanawawezesha hao M23..
Ni ujinga viongozi Wa Africa kukubali huu uhayawani...
 
Hii maneno iseme kwa sauti ya chini sana. Nadhani umenielewa.
Huu ni mchezo kama michezo mingine.
Shame on us African na viobgozi wetu
Mkuu, ni kweli hii michezo saa hii yachezwa kwa uwazi na umeona Gaza pale Israeli mawakala wa wakubwa wa Dunia wameichakaza na sasa Qatar atapewa kazi ya reconstruction ya Gaza mpya kwa kutumia resources zilizopo palepale Gaza.

Tunaona Russia/ Ukraine war ambayo pia ni kugombea rasilimali.

Na Rwanda pia ni same case.

Ndo Dunia ilipofika saa hii jomba.
 
Zipo falsafa za kisiri zinaendesha mambo
 
Toka jana tarehe 23 Januari 2025, mida ya saa mbili usiku, mji wa Goma uligubikwa na giza.

Ni baada ya taarifa za kifo cha aliekuwa mkuu wa mkoa wa Kivu kasikazini Mejor General Chirimwami. Leo subuhi, maji,umeme na huduma za mitandao havikupatikana kabisa,jambo lililozua hofu kwa wakazi wa mji huo.

Wengi wenye uwezo, kwa kuhofia kuporwa mali zao na jeshi la FARDC na wazalendo, wamepanda ndege na kuelekea mikoa mingine ikiwemo Kinshasa. Uongozi wa serikali umewataka wananchi kuwa watulivu na kuliamini na kuliunga mkono jeshi lao, ila wanaonekana kukosa imani, baada ya kukosa huduma hizo za msingi.

Pamoja na hali hiyo, inasemekana pia eneo la tambalale lililopo umbali wa km 20 kutoka mji wa Goma, tayari lipo mikononi mwa M23,maana kwa sasa wanapigana kutoka pande tofauti tofauti(kwa makundi),na inaonekana FARDC hawajui waanzie wapi.

Kwa wanaojaribu kudadavua mambo, wanahisi lengo la M23 ni kuifunga mipaka ya DRC na Rwanda, jambo litakalosababisha waliozingilwa wasiweze kutoka. Na hali ikiwa hivi kweli, kuna dalili sa majeshi ya Tanzania,Malawi na South Africa kudhalilika,maana kwa hali iliyopo, M23 bado imaendelea kuwaomba wakae mbali na jeshi lipigane lenyewe, vinginevyo na wao watashughulikiwa.

Ikumbukwe, kwa kuzingilwa kwa mji huo, sababu ni kwamba jeshi hilo lisiweze kupata msaada wa kijeshi kutoka nje. Na baada ya kuona hali si shwali, FARDC iliamua kusafirisha badhi ya siraha zake kupitia njia ya maji kuelekea Bukavu. Picha, ni hali ya Goma kwa sasa.

View attachment 3213045View attachment 3213046
Wamarekani ni Wapumbavu sana...
America wako na Kagame..
Wao ndo wanawawezesha hao M23..
Ni ujinga viongozi Wa Africa kukubali huu uhayawani...
Tangu nijue DRC iko kimkakati na UN inaratibu. Sina cha kusema.
Poor Africa inaangamia kwa kukosa viongozi waadilifu. Shame on us
Africa my continent

"Let us agreed that Black people cannot rule themselves, Whites are born in order to rule and Blacks are born to be ruled."

Pieter W. Botha, a former President of South Africa during the Apartheid era.
 
Back
Top Bottom