Mji wa Goma (mashariki mwa DRC) watanda giza

25 January 2025
WAKATI WA KUKATA TAMAA: Jean-Pierre Bemba Awaomba Vijana Kujiunga na Jeshi katika Mapambano dhidi ya M23


Machafuko yametokea katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambapo waasi wa M23 wako mbioni kuchukua udhibiti wa taifa hilo huku wakiendelea kusonga mbele.

Vikosi vya Jeshi la Ulinzi la Kongo (FARDC), ambavyo tayari havina vifaa na vinalipwa kidogo, vimezidiwa nguvu na haviwezi tena kudhibiti vikosi vya M23 vilivyojiimarisha katika mkoa wa Kivu Kaskazini.

Aliyepata kuwa Naibu Waziri Mkuu (2023 - 2024) ambaye sasa naibu waziri wa Uchukuzi na aliyepata kutuhumiwa kwa uhalifu wa kivita akahukumiwa kuwa mfungwa mheshimiwa Jean-Pierre anawaomba vijana na raia wengine wa Kongo wajiunge na jeshi la taifa FARDC kwenye safu za vita.

Bemba aliwaalika vijana wa Kongo kujiunga na kuimarisha safu ya FARDC ambayo imepata hasara kubwa, akisisitiza kuwa ulinzi wa nchi ni jukumu la kawaida.

"Jiunge na FARDC ili kuchangia kikamilifu katika kuhifadhi usalama na sovereignty la eneo letu na ujenzi wa mustakabali thabiti na wenye mafanikio kwa nchi yetu," waziri Bemba alisema.

Hivi majuzi M23 walimpiga risasi Gavana wa Kijeshi wa FARDC wa Mkoa wa Kivu Kaskazini Meja Jenerali Peter Cirimwami walipokuwa kwenye uwanja wa mapambano kuashiria kuimarika kwao mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
 
25 January 2025

HALI YA HOFU IMESAMBAA: Tshisekedi Awaita Jeshi, Wakuu wa Polisi kwa Mkutano wa Mgogoro Kuhusu Hali Ya Kutisha ya Mashariki

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo mheshimowa Félix Tshisekedi amefanya mkutano wa dharura na wakuu wa Jeshi la Ulinzi (FARDC) na Polisi wa Kitaifa (PNC) kuhusu hali ya usalama inayotia wasiwasi katika jimbo la Kivu Kaskazini.

Mkutano huo ambao ulifanyika Alhamisi hii jioni , ulihudhuriwa pia na Waziri Mkuu Judith Suminwa Tuluka pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani na yule wa Ulinzi.

Tshisekedi ataongoza zaidi Baraza Kuu la Ulinzi na mkutano wa kila wiki wa Baraza la Mawaziri kesho huku maendeleo ya waasi wa M23 yakiwekwa kuwa jambo kuu katika ajenda.

Waasi wa M23 wamedhibiti karibu eneo lote la Kivu Kaskazini na sehemu ya Mkoa wa Kivu Kusini kufuatia mapigano makali yaliyoripotiwa wiki hii iliyopita
 
09 January 2025
Rais Kagame: "Viongozi wa M23 na wapiganaji wao wengi walitoka Uganda"


View: https://m.youtube.com/watch?v=BPrC8hSfPko

Rais Kagame ameeleza kuwa makundi yanayopigana mashariki mwa Congo DR hayana uhusiano wowote na Rwanda,.

Rais Kageme asisitiza kuwa sababu pekee ya Rwanda kuingizwa katika picha hiyo ni kwa sababu wapiganaji hao wanazungumza Kinyarwanda.

"Hawakutoka Rwanda...viongozi hawa wa M23 na wapiganaji wao wengi walitoka Uganda ambako walikuwa wakimbizi,"
 
Basi hakuna jeshi hapo kuna wahuni tu humo jeshini.
 
Maiti yake ilikuwa inapambaniwa kwa sababu gani mkuu?
Duh! Vitani kuna watu hasa wa vyeo vikubwa, wanakuwa wanted deal or alive(akiwa mzima au amekufa). Chirimwami alikuwa level nyingine. Na anahusishwa na kuwa daraja kati ya FDLR na Serikali ya Congo. Vitani kama hali inaruhusu, maiti za wenzenu hazitakiwi kuangukia mikononi mwa adui. Nadhani kukamatwa kwa maiti kunadhihilisha uzembe kwa team yake(mwenye uelewa zaidi anaweza tusaidia).
 
Naona Kagame anazunguka zunguka tu hatoi majibu
 
Hali ni tete.....Hao wenye njaa ndio wakapambane na M23?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…