Mji wa Goma (mashariki mwa DRC) watanda giza

Mji wa Goma (mashariki mwa DRC) watanda giza

Ndio maana tunasema isaidiwe Kwa kuvunja Jeshi na Idada za usalama Ili Nchi zingine za Kizalendo ndio zishike hatuma Ili recruitment ianze upya na waasi wasakwe waporwe silaha kokote waliko.
Sasa unasaidiaje kunavunjaje jenshi la nchi nyingine.Maana hili ni jambo la ndani la nchi.Taratibu za kimataifa haziko hivyo.kinachoweza fanyika ni kuweka vikwazo tuu kwa nchi. sababu mfumo wote uko corrupted na unanufaika na hali inavyoendelea.Jeshi lingekuwa safi ndiyo lingetumika kupindua serikali.lakini kwa DR Congo inaonekana serikali na jeshi vyote ni corupted.

Ndiyo maana ukichagua raisi wa hovyo akafanikiwa kuunda jeshi la hovyo basi nchi itapambana na hali yake.Labda wananchi waamue kuingia barabarani
 
Tanzania
Burundi
Burkifaso
South Africa
Namibia
Zimbabwe
Algeria
Guinea
Ethiopia
Kikubwa hapo ni intelligence hata ulete jeshi la vipi.....na kwa upepo ulivyo kwa sasa M23 anaonekana yupo vizuri sana kwenye intelligence kuliko vikosi anavyopigana navyo,, sasa jiulize anapata wapi huo uwezo wakati ni kikundi tu cha waasi ila anawapiga gap hadi majeshi ya serikali za nchi zinazosaidia hapo
 
Sasa unasaidiaje kunavunjaje jenshi la nchi nyingine.Maana hili ni jambo la ndani la nchi.Taratibu za kimataifa haziko hivyo.kinachoweza fanyika ni kuweka vikwazo tuu kwa nchi. sababu mfumo wote uko corrupted na unanufaika na hali inavyoendelea.Jeshi lingekuwa safi ndiyo lingetumika kupindua serikali.lakini kwa DR Congo inaonekana serikali na jeshi vyote ni corupted.

Ndiyo maana ukichagua raisi wa hovyo akafanikiwa kuunda jeshi la hovyo basi nchi itapambana na hali yake.Labda wananchi waamue kuingia barabarani
Wao kama DRC ndio wakubali kuanza upya kama hawataki basi wajue Nchi itaanza kugawanyika Moja baada ya nyingine.

Kivu itakuwa Nchi inayojitegemea ambapo mwisho wa siku itaungana na Rwanda.

Baadae majimbo mengine yatafuata.
 
Polisee huyo siyo Mjeda .....ila kesho mutu asianze kulia lia hakuna kusimamisha Mapigano ni mwendo wa BM na mvua ya MASASE
Upo Drc? Au unasimuliwa kuhusu Drc? Unataka useme majeshi ya FARDC yana nidhamu sana sio? Upo Congo kweli wewe? Kuna mengi hujayajua nakuuliza kitu kimoja tu unijibu directly ..,


WAKATI ZILE BM ZINAUNGURUMA KWA WAASI ILIKUAJE WAKAACHA KUPIGA TENA? Ukishapata majibu ya hapo tu tulia kula samaki zako subiri urudi baa za Kawe wakukome na subaru yako mpya.

NB, niliweka video ya police ikiakisi tabia ya jumla ya majeshi ya Congo hilo nalo hukuelewa ,
Ni mara ngapi umesikia hao hao majeshi ya serikali kubaka ,kuua na kupora mali kwa raia?
 
Upo Drc? Au unasimuliwa kuhusu Drc? Unataka useme majeshi ya FDLC yana nidhamu sana sio? Upo Congo kweli wewe? Kuna mengi hujayajua nakuuliza kitu kimoja tu unijibu directly ..,


WAKATI ZILE BM ZINAUNGURUMA KWA WAASI ILIKUAJE WAKAACHA KUPIGA TENA? Ukishapata majibu ya hapo tu tulia kula samaki zako subiri urudi baa za Kawe wakukome na subaru yako mpya
Kwaa Taarifa yako hao Nyamurenge wameanza kula kifinyo na lile daraja limesha vunjwa mwingine mkubwa wao yupo hapa LEBA anajifunguwa Masase
 
kifo cha aliekuwa mkuu wa mkoa wa Kivu kasikazini Mejor General Chirimwami. Leo subuhi, maji,umeme na huduma za mitandao havikupatikana kabisa,jambo lililozua hofu kwa wakazi wa mji huo.

HABARI ZA KINA NA ZA NDANI
Meja jenerali huyo inasemekana amepoteza maisha kutokana na majeraha vitani


View: https://m.youtube.com/watch?v=hAb9ctrgVdc
Habari Uasi wa M23: DRC Yathibitisha Kuuawa kwa Gavana wa Kivu Kaskazini, Jenerali Peter Cirimwami Licha ya kukimbizwa mji mkuu wa Kinshasa kwa matibabu, alifariki kutokana na majeraha yake anaripoti Claver Ndushabandi Januari 24, 2025

5842703c-a2b9-4c3f-acb5-9efe1f79d76e-780x405.jpeg
Picha maktaba : Meja Jenerali Chirimwami kwenye mstari wa mbele siku ya Alhamisi

Goma - Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imethibitisha kifo cha Meja Jenerali Peter Chirimwami, gavana wa kijeshi wa Kivu Kaskazini, ambaye alikufa kutokana na majeraha aliyopata karibu na mstari wa mbele kati ya Goma na Sake.

Tangazo hilo, lililotolewa katika taarifa ya Jeshi la Kongo (FARDC) siku ya Ijumaa mjini Kinshasa, linakuja wakati waasi wa M23 wakizidisha mashambulizi yao kuelekea Goma, na hivyo kuzidisha hofu ya kuongezeka kwa eneo hilo.


Meja Jenerali Cirimwami, ambaye alikuwa akiratibu operesheni za ulinzi dhidi ya M23, alijeruhiwa vibaya siku ya Alhamisi alipokuwa akiwatembelea wanajeshi.
Licha ya kukimbizwa Kinshasa kwa matibabu, alifariki dunia kutokana na majeraha yake.

"Alianguka kishujaa na silaha mikononi mwake,akiwa mstari wa mbele " taarifa ya FARDC ilisoma, ikisisitiza jukumu lake kubwa kwenye uwanja wa vita.
Kifo chake kinaashiria pigo kubwa kwa juhudi za kijeshi za DRC katika wakati muhimu katika mapambano ya kulinda Goma.

Maendeleo ya M23
Kifo cha Cirimwami kinakuja huku kukiwa na mapigano makali huko Sake, mji muhimu ulio kilomita 20 tu kutoka Goma ambao unatumika kama eneo kuu la mwisho la ulinzi mbele ya jiji hilo.
Waasi wa M23, wanaodai kuwa wanasonga mbele "kuikomboa" Goma, wamevuka maeneo makubwa, na kulazimisha vikosi vya Kongo na washirika wao wa kikanda kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) kuweka ulinzi mkali.

FARDC, ikiungwa mkono na wanajeshi wa SADC, wakiwemo wanajeshi wa Jeshi la Ulinzi la Kitaifa la Afrika Kusini (SANDF), wametuma helikopta, silaha nzito nzito, na vikosi maalum kusimamisha M23.

Kukamatwa kwa eneo hilo la Sake na waasi hao M23 kumeongeza hatari ya kushambuliwa Goma, kitovu cha kimkakati cha mashariki mwa DRC.

Mkuu wa Umoja wa Mataifa Aonya

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ameonyesha hofu juu ya mashambulizi mapya ya M23, akionya kuhusu "adhabu mbaya" kwa raia na uwezekano wa kuongezeka kwa vita vya kikanda.
"Kukamatwa kwa Sake kunaongeza tishio kwa Goma na kuongeza hatari ya kuongezeka kwa eneo," Guterres alisema katika taarifa siku ya Alhamisi.
Alitoa wito kwa M23 kusitisha mara moja mashambulizi yake, kujiondoa katika maeneo yote yanayokaliwa, na kutii makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyotiwa saini Julai 31, 2024.

Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa pia alitoa wasiwasi juu ya madai ya Rwanda kuunga mkono M23, akinukuu matokeo ya ripoti ya Kundi la Wataalamu wa Umoja wa Mataifa iliyoandika kuwepo kwa wanajeshi wa Rwanda katika ardhi ya Kongo. Rwanda inakanusha shutuma hizo, lakini suala hilo linaendelea kuzorotesha uhusiano katika eneo hilo.
 
Kwaa Taarifa yako hao Nyamurenge wameanza kula kifinyo na lile daraja limesha vunjwa mwingine mkubwa wao yupo hapa LEBA anajifunguwa Masase
Tatizo lako u mgeni wa hayo mambo unaongea kishabiki nimekuuliza mwanzo walipigwa BM ikawaje ikasitishwa ?
 
Meja jenerali huyo inasemekana amepoteza maisha kutokana na majeraha vitani


View: https://m.youtube.com/watch?v=hAb9ctrgVdc

Hapa kikubwa tu ni kwamba amekufa,uhakika wa nani kamuua ndo bado, ila kwa vyanzo vya habali, walimchola muda mrefu na kumuwekea mtego. Sasa jiulize kwenye sekeseke la kuipambania maiti yake walikufa watu wangapi! Na inasemekani alikufa na ma kanali 3
 
Huko kwenye jeshi la FARDC kuna mapandikizi ya M23 kama yote.kila kinachopangwa FARDC kinafika M23 kama kilivyo.hivyo hakuna chochote cha siri ndani ya jeshi ambacho m23 hawakijui.
Unawaitaje pandikizi wakati ni wazawa?
 
Huko kwenye jeshi la FARDC kuna mapandikizi ya M23 kama yote.kila kinachopangwa FARDC kinafika M23 kama kilivyo.hivyo hakuna chochote cha siri ndani ya jeshi ambacho m23 hawakijui.
Hapo kikubwa ni ma Godfather wa eneo hilo wana influence kiasi gani.......kwa kule unaweza ukawa rais ila kuna upande ma godfather ndo wananguvu juu ya wanachi kuliko wewe rais.......jamaa watakuchezea hadi ikulu maana wanakua na watu wao kwenye kila idara ndani ya nchi....na ogopa sana kwenye jeshi yakiingia makundi ambayo yanakua loyal kwa mkubwa wao fulani tu hata kama sio rais wa hio nchi.........serikali ya DRC ina nguvu pande za Kinshasa tu ila wakija mashariki lazima kuna namna wakubaliane na wababe wa eneo hilo ndo unakuta kuna vikundi vya waasi vimeingizwa jeshini, shida sasa hivyo vikundi vya waasi kuna kipindi vinakua na watu waliowahi kua M23 maana wengi wa wapiganaji ni watu wa maeneo hayohayo inategemea sasa hilo eneo kalichukua mbabe gani,,,sasa serikali ukija kuchukua kikundi fulani kiingie jeshini basi jua hadi watu wa lile kundi hasimu utawaingiza jeshini.....ndo kinachoendelea huko
 
Tatizo lako u mgeni wa hayo mambo unaongea kishabiki nimekuuliza mwanzo walipigwa BM ikawaje ikasitishwa ?
Huku ndo nimekulia labda Kisangani Kaskazini Magharibi kwenye Misitu minene naweza potea

Tatizo ni asili ya Roho mbaya iweje ukaribishwe uwanze kutowa AMRI ...kama wewe ni Mzoefu wa hayo Mambo ulishafika Mwese na Ikola Mpanda....kama umefika tupe kidogo uzoefu

Habari ya BM muda huu ndo ZINASOSELA mpaka kesho saa sita mchana MAJIBU utayapata HAPA HAPA
 
Namfahamu kiasi huyu mzee alikua mtu wa tungi hivi,

Apumzike kwa amani

Kivu, Congo DR

Pia alisititiza maendeleo ya jimbo kama gavana, habari maktaba za meja jenerali Peter Chirimwami akisimamia ujenzi wa miundomsingi


View: https://m.youtube.com/watch?v=1pK3r6nR1VE
Wananchi nao waongea kuhusu usimamizi na kutumika (kazi) za maendeleo ambazo gavana alisimamia ...27 Machi 2024.. VoA ilipofika Goma kushuhudia kazi za maendeleo ... vifaa kazi kama matingatinga yakipasua miamba na majabali kutengeneza barabara, kiwanja cha ndege, bandari kuunganisha maeneo mbalimbali ya jimbo huku gavana akiwatembeza kuonesha ... Goma inaenda kuwa Paradiso wakaazi wakisifia kazi za gavana hadi sasa

Serikali ya jimbo la Kivu Kaskazini Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo inayo ongozwa na wanajeshi imeanzisha miradi ya maendeleo hasa ujenzi wa barabara muhimu katika Miji ya Goma, Beni na Butembo, lengo kuu kupunguza athari za usafiri kwa wakaazi wa maeneo hayo.
 
Huku ndo nimekulia labda Kisangani Kaskazini Magharibi kwenye Misitu minene naweza potea

Tatizo ni asili ya Roho mbaya iweje ukaribishwe uwanze kutowa AMRI ...kama wewe ni Mzoefu wa hayo Mambo ulishafika Mwese na Ikola Mpanda....kama umefika tupe kidogo uzoefu

Habari ya BM muda huu ndo ZINASOSELA mpaka kesho saa sita mchana MAJIBU utayapata HAPA HAPA
Sawa kesho saa sita mchana ntakucheki hapa
 
Back
Top Bottom