Mji wa Goma (mashariki mwa DRC) watanda giza

Mji wa Goma (mashariki mwa DRC) watanda giza

Toka jana tarehe 23 Januari 2025, mida ya saa mbili usiku, mji wa Goma uligubikwa na giza.

Ni baada ya taarifa za kifo cha aliekuwa mkuu wa mkoa wa Kivu kasikazini Mejor General Chirimwami. Leo subuhi, maji,umeme na huduma za mitandao havikupatikana kabisa,jambo lililozua hofu kwa wakazi wa mji huo.

Wengi wenye uwezo, kwa kuhofia kuporwa mali zao na jeshi la FARDC na wazalendo, wamepanda ndege na kuelekea mikoa mingine ikiwemo Kinshasa. Uongozi wa serikali umewataka wananchi kuwa watulivu na kuliamini na kuliunga mkono jeshi lao, ila wanaonekana kukosa imani, baada ya kukosa huduma hizo za msingi.

Pamoja na hali hiyo, inasemekana pia eneo la tambalale lililopo umbali wa km 20 kutoka mji wa Goma, tayari lipo mikononi mwa M23,maana kwa sasa wanapigana kutoka pande tofauti tofauti(kwa makundi),na inaonekana FARDC hawajui waanzie wapi.

Kwa wanaojaribu kudadavua mambo, wanahisi lengo la M23 ni kuifunga mipaka ya DRC na Rwanda, jambo litakalosababisha waliozingilwa wasiweze kutoka. Na hali ikiwa hivi kweli, kuna dalili sa majeshi ya Tanzania,Malawi na South Africa kudhalilika,maana kwa hali iliyopo, M23 bado imaendelea kuwaomba wakae mbali na jeshi lipigane lenyewe, vinginevyo na wao watashughulikiwa.

Ikumbukwe, kwa kuzingilwa kwa mji huo, sababu ni kwamba jeshi hilo lisiweze kupata msaada wa kijeshi kutoka nje. Na baada ya kuona hali si shwali, FARDC iliamua kusafirisha badhi ya siraha zake kupitia njia ya maji kuelekea Bukavu. Picha, ni hali ya Goma kwa sasa.

View attachment 3213045View attachment 3213046

Huko kwenye jeshi la FARDC kuna mapandikizi ya M23 kama yote.kila kinachopangwa FARDC kinafika M23 kama kilivyo.hivyo hakuna chochote cha siri ndani ya jeshi ambacho m23 hawakijui.
 
Tena bora hata Israel.....DRC ni nchi moja ila ndani yake ina watu wenye misimamo tofauti na kuna maeneo watu tokea wazaliwe wanajua vikundi vya waasi ndo serikali yenyewe........DRC kwa mashariki ni kama hakuna serikali kabisa bali tu ni makundi yanaji organise yanatawala eneo fulani
Ukweli ni kwamba DRC inasumbuliwa na Wasiojulikana, M23 wanasingiziwa tu.

Wasiojulikana DRC ni majeshi yao wenyewe. Wanatajirika kuba mali nyingi humo.
 
Tena bora hata Israel.....DRC ni nchi moja ila ndani yake ina watu wenye misimamo tofauti na kuna maeneo watu tokea wazaliwe wanajua vikundi vya waasi ndo serikali yenyewe........DRC kwa mashariki ni kama hakuna serikali kabisa bali tu ni makundi yanaji organise yanatawala eneo fulani
Watu wanarahisisha,bila DRC kusaidiwa na mataifa mengine ya Africa yenye Uzalendo itasambaratika Kila Jimbo liwe kivyake.

Ndio Maana Huwa nasema hata Sgr yetu Haina maana yeyote kama tunakopanga ifike hakuna amani
 
Huko kwenye jeshi la FARDC kuna mapandikizi ya M23 kama yote.kila kinachopangwa FARDC kinafika M23 kama kilivyo.hivyo hakuna chochote cha siri ndani ya jeshi ambacho m23 hawakijui.
Yaani DRC inahitaji Msaada wa Nchi za Kizalendo.

Hata hapa Tanzania tabia ya kuingiza ingiza watu jeshini na usalama kinyemela Kuna siku itakuja kutu cost.

Mara 100 💯 watu wa mipakani wasiwe kwenye vyombo nyeti
 
Yaani DRC inahitaji Msaada wa Nchi za Kizalendo

Kwa hali ilivyo sasa ni kama haiwezekani tena.Labda Mungu mwenyewe aingilie kati.mpaka rasilimali zote zitakapoisha congo ndiyo itatulia. iko hiv,jesh la congo linaongozwa na waasi bila watu kujua.kuna watu walishaingizwa jeshini na wako kwenye nafasi za juu kabisa kwa maslahi ya mataifa mengine
 
Watu wanarahisisha,bila DRC kusaidiwa na mataifa mengine ya Africa yenye Uzalendo itasambaratika Kila Jimbo liwe kivyake.

Ndio Maana Huwa nasema hata Sgr yetu Haina maana yeyote kama tunakopanga ifike hakuna amani
DRC kuna mambo inabidi wayabadili kutokea ndani ,wasipobadilika hata wakisaidiwa vipi mambo yatarudi vilevile....
..ile nchi kuanzia serikali hadi vikundi vya waasi kuna makundi/nchi za wazungu wanakula nao mema ya nchi ndo maana ukisema uisaidie serikali ,mulemule ndani ya nchi kuna watu tayari watakuona unawasaidia watu fulani na vibaraka wao,,, na wao unakuta wanaamua kuliamsha huku wakipewa support na wenzao wa nje waiangushe serikali..........kikubwa zile rasilimali wangekubali kwanza ziwanufaishe wote kwenye ile nchi ndo mengine yaendelee ila kwa jinsi hali ilivyo sasa akishinda mmoja lazima ampe mwenzie shida,,kwahio wakishatambua hilo vita hazitaisha kule
 
JW hapo kama mgeni mualikwa tu hana nguvu kiasi hiko shida ni serikali ya DRC yenyewe kujielewa ....maana anataka kucheza kete za kusaidiwa na nchi jirani huku pia anataka kuendelea na matajiri wake wa ufaransa na ubelgiji.......kule kuna conflict of interest kikubwa jamaa wakishtuka bora wajitoe tu maana kushinda kule ni ngumu
Hata Tized in Maslahi huku na tukijitowa yule Nyoka wa Nile atatumeza wacha tuanze kutafuta KICHWA
 
Kwa hali ilivyo sasa ni kama haiwezekani tena.Labda Mungu mwenyewe aingilie kati.mpaka rasilimali zote zitakapoisha congo ndiyo itatulia. iko hiv,jesh la congo linaongozwa na waasi bila watu kujua.kuna watu walishaingizwa jeshini na wako kwenye nafasi za juu kabisa kwa maslahi ya mataifa mengine
Na waasi wengi waliopo kwenye jeshi la DRC ni wale wanaotaka kuwafuta banyamulenge na jamii nyingine zenye asili ya kitutsi,,,kwahio na wao lazima Rwanda aingilie kati na hata Uganda ana mkono wake pale sema main ni Rwanda,,,kikubwa labda makundi yote yangekubaliwa kuingia jeshini na kwenye serikali
 
Yaani DRC inahitaji Msaada wa Nchi za Kizalendo.

Hata hapa Tanzania tabia ya kuingiza ingiza watu jeshini na usalama kinyemela Kuna siku itakuja kutu cost.

Mara 100 💯 watu wa mipakani wasiwe kwenye vyombo nyeti
Wanapitia ule Mlango kuna wakati nahisi tupo open kwa maadui zetu haswa huko JIKONI
 
Kwa hali ilivyo sasa ni kama haiwezekani tena.Labda Mungu mwenyewe aingilie kati.mpaka rasilimali zote zitakapoisha congo ndiyo itatulia. iko hiv,jesh la congo linaongozwa na waasi bila watu kujua.kuna watu walishaingizwa jeshini na wako kwenye nafasi za juu kabisa kwa maslahi ya mataifa mengine
Ndio maana tunasema isaidiwe Kwa kuvunja Jeshi na Idada za usalama Ili Nchi zingine za Kizalendo ndio zishike hatuma Ili recruitment ianze upya na waasi wasakwe waporwe silaha kokote waliko.
 
Haha Tz kuna kitu.....part ipo na Rwanda na part ipo na Drc......kuna mambo mengi.....wacha tuishie hapo
Hahaha haya Mkuu hapa Lubumbashi enzi ya Boing 737 Serengeti na Kilimanjaro zinapishanà angani kama daradara...
 
Sasa vijana wetu wachache wa jwtz ambao wapo hapo goma tunawasaidiaje jamani hatutaki watoto yatima kwa sababu za vita ya congo..
Wangerudi tu jamani.
Wanarudije labda? Hapa ni uwanja wa aibu na kejeri kwa sasa mkuu. Ulisikia waliokataa kupigana Burundi kilichowakuta? haya,imagine misifa inayomwagiwa JWTZ, na watu hao hawajiwezi mbele ya M23,na ikitokea wataonekana wasaliti. Haya yote ni makosa ya viongozi wanaotanguliza matumbo yao na familia zao.

Hakuna kazi ya kinafiki kama siasa. Hivi, unajua hilo jeshi na dhana zao walipita wapi? Hii vita ina mitego mingi, DRC na washilika wake hawaiwezi. Wanajeshi wanapukutika tu lakini kiuhalisia mshindi anajulikana.
 
Ndio maana tunasema isaidiwe Kwa kuvunja Jeshi na Idada za usalama Ili Nchi zingine za Kizalendo ndio zishike hatuma Ili recruitment ianze upya na waasi wasakwe waporwe silaha kokote waliko.
Hapo sasa nchi za kizalendo ni zipi? Maana kwa sasa ukimuweka Tanzania na Uganda😀😀☻☻, Burundi ndo hivyo......Afrika kusini sijajua kama ana uzoefu sana na yale maeneo,,,,,,,,,,,
 
Hahaha haya Mkuu hapa Lubumbashi enzi ya Boing 737 Serengeti na Kilimanjaro zinapishanà angani kama daradara...
Kuna sababu kwanini ule muungano wa majeshi ya nje na serikali kwa sasa haufui dafu kwa M23...........kuna kamanda wa Kenya alikuaga kwenye hivyo vikosi vya UN alitokaga nduki kabisa kurudi Nairobi 🤣🤣jamaa walimtishia tu, pale mziki wake ni mkubwa na kuna wachezaji wengi na wakubwa
Screenshot_20250125-145638_Chrome.jpg

Ukiona hadi kamanda anatoka nduki kwenye mission area na sababu ni kutishiwa tu tena na watu ambao hawajui....jua tu hapo sio sehemu ya kawaida
 
Hapo sasa nchi za kizalendo ni zipi? Maana kwa sasa ukimuweka Tanzania na Uganda😀😀☻☻, Burundi ndo hivyo......Afrika kusini sijajua kama ana uzoefu sana na yale maeneo,,,,,,,,,,,
Tanzania
Burundi
Burkifaso
South Africa
Namibia
Zimbabwe
Algeria
Guinea
Ethiopia
 
Back
Top Bottom