Mji wa Ifakara ni mzuri kuliko Njombe mjini

Mji wa Ifakara ni mzuri kuliko Njombe mjini

Unaesema makambako ipo wilaya ya ludewa hebu angalia na ramani hiyo ulinganishe na vitu unavo viongea
FB_IMG_16419032754961153.jpg
 
Na ukienda Ifakara msimu wa kung'olelea mpunga (march mpaka Mei) aisee huwa kunapooza sana!

Yaani mishe mishe na kuchangamka ni wakati wa mavuno na kiangazi (Juni mpaka Disemba)! Mfano ukienda leo Ifakara, ni lazima utafurahia zile mishe mishe za watu. Ila baada ya hapo, kunadorora tena!
Nikifikiria week ilopita nimekaa Iragua siku nane kisa daraja limekatika pale stand ya nyanya,daah wabunge wa hayo maeneo miyeyusho sana.By the way nimeishi huko kiukwel mkoa wa Morogoro unahitaji kugawanywa ili kusogeza huduma za kijamii karibu sijui lini hilo bonde watalifanya kuwa mkoa
 
Yan jamaa Kama hujui tulia tukueleweshe ambao tuko eneo husika wilaya ya njombe Ina wakurugenzi watatu Kuna wa mji njombe ,wa mji makambako na wawilaya na hizi ndizo zinazo unda makao makuu ya mkoa wa njombe na ludewa inajitegemea haina mji ile ko Ina onekana hata njombe hujawai fika huwezi sema makambako ipo ludewa hata kijiografia Ni tofauti mno
Ni kweli makambako iko nyuma huku kabla ya kufika Njombe, ukifika Njombe km unaelemea Songea unakata kuli pale ndiyo unapata uelekeo wa Ludewa (Monilii)
 
Nikifikiria week ilopita nimekaa Iragua siku nane kisa daraja limekatika pale stand ya nyanya,daah wabunge wa hayo maeneo miyeyusho sana.By the way nimeishi huko kiukwel mkoa wa Morogoro unahitaji kugawanywa ili kusogeza huduma za kijamii karibu sijui lini hilo bonde watalifanya kuwa mkoa

Dah! Nimepita sana hayo maeneo ya Lupilo, Iragua, Itete, Mtimbira, Sofi, mapaka Malinyi! Miaka hiyo ya 90, unapanda basi saa 9 za usiku!
Ukilichelewa tu, itakulazimu kusafiri tena kesho yake, au ubahatike kupanda gari la wamisheni wa Kikatoliki!

Hilo Bonde la Kilombero miaka nenda halijawahi kuwa na unafuu wa miundombinu! Ingawa kuna wasomi wengi tu wanatokea huko. Ukienda ule upande wa Mlimba, nako ni shida tu wakati wa masika. Barabara ni mbovu mpaka basi.
 
Yan jamaa Kama hujui tulia tukueleweshe ambao tuko eneo husika wilaya ya njombe Ina wakurugenzi watatu Kuna wa mji njombe ,wa mji makambako na wawilaya na hizi ndizo zinazo unda makao makuu ya mkoa wa njombe na ludewa inajitegemea haina mji ile ko Ina onekana hata njombe hujawai fika huwezi sema makambako ipo ludewa hata kijiografia Ni tofauti mno
Mkuu, makambako si wilaya ya wanging'ombe?
 
Makambako haipo wilaya ya wanging'ombe ipo wilaya ya njombe wilaya ya njombe Ina halmashauri tatu na mkuu wa wilaya Ni mmoja. Watu wengi huwa wanajua hivyo no ingawa kwa Sasa makambako imeomba kujitegemea kuwa wilaya
Mkuu, makambako si wilaya ya wanging'ombe?
 
Huu upumbafu wa ku compare maeneo sijui Nan kauanzisha humu JF imekuwa kero yaan
 
Labda anaiongelea Ifakara ya Katindiuka, Mwembetogwa, Mlabani, Silent Inn, Minepa, Viwanja 60, Lipangalala, Lumemo, Michenga, Ihanga, au Kihogosi!

Ifakara ni mji wa zamani na wa kihistoria. Ila kuulinganisha na Njombe, kiukweli ni uonevu. Labda Ifakara uilinganishe na Kilosa. Hapo sawa. Ufupi tu Njombe iko juu zaidi ya Ifakara. Kuanzia kwenye kipato na pia majengo.
Mkuu nakubaliana nawe, vile vile maumbile ya kijografia yapo tofauti: Njombe mandhari (view) yake iko vizuri sana iliyopangwa kwa mitelemko na miinuko iliyojipanga, tofauti na Ifakara bonde la mpunga na ndio maana hata nyumba za Serikali wameanua kuzijenga Kibaoni. Ifakara hata kwa Makambako haipati.
 
Njombe nimeishi miaka 3,nakujua hadi Lupembe,ukalawa,made kesho,kifanya,ikondo.

Njombe mjini ni sehemu ndogo sana,toka pale Hospital ya wilaya hadi uwanja wa ndege mji umeisha

Mji wa Ifakara, unaweza kuwa sawa kabisa kwa ukubwa na Mji wa Njombe. Ni moja ya makao makuu ya Wilaya ambazo ni kubwa. Zingine ni Masasi, Tarime, Korogwe, Nzega na kipekee mji wa Tunduma
 
Niongezee tu kwa TZ wilaya ambazo zinavibe ni pamoja Masasi, Mbinga,Kahama, Ifakara na Tunduma hizi sehemu huduma zote muhimu zipo

Daa, ndo nimoena hii post, utafikiri tulikua pamoja. Wilaya au miji hii ina compete na Manispaa nyingi tu hapa Tanzania: Masasi, Tunduma, Kahama hiyo tayari, Tarime, Ifakara ni ya pili baada ya Morogoro, Korogwe ingawa naona kama inashuka sasa, lakini Makambako nayo siyo kubwa ila inajitahidi
 
Mkoa wa Morogoro umekosa watetezi. Viongozi wengi wamependa kupata na kuhidhi Ardhi wanahofu au maslahi binafsi kutokuugawa Mkoa wa Morogoro. Mkoa una vigezo vyote vya kuzaa Mikoa Mingine - Ukubwa Wa Eneo, Idadi yq Watu na Shughuli za Kiuchumi tangu pale Mikoa ya Rukwa, Iringa, Mbeya, Mwanza na Shinyanga ilipokuwa inagawanywa kuzaa Mikoa Mingine. Mikoa mingine ilikuwa Upendeleo Tu wa Wazi kuvutia Uwekezaji wa Raslimali za Taifa kwa Makao Makuu ya Mikoa. Mji wa Mpanda na Kilosa kihistoria inafanana na Wilaya ya Kilosa ina Idadi kubwa ya Watu na Uchumi Mkonge iliufanya Maarufu lakini haukufanywa kuwa Mkoa- kulikoni kama sio Upendeleo wa aliekuwa WM Mhe MPP. Mkoa wa Morogoro sasa iwe na isiwe uzae Mikoa Mitatu (1) Morogoro - Makao Makuu Morogoro (2) Rubeho au Wami Makao Makuu Kilosa na (3) Kilombero au Ruaha au Ulanga - Makao Makuu Malinyi au Ifakara.

Mikoa 3 hapana, mikoa miwili ni halali kabisa, makao makuu yawe Ifakara na siyo Malinyi. Ifakara ni katikati na Centre kubwa, njia panda ya kwenda Njombe kupitia Lupembe na njia ya kwenda Songea kupitia Malinyi huko. Pia njia ya kwenda Ulanga! Kiuhalisia Ifakara ile lami inayotokea Mikumi ikikamilika, Njombe ikae mguu sawa, kwanza wana mazao mengi sana. Siyo sehemu ya kubeza hata kidogo!
 
Sasa mkuu huo Mji si unachangamshwa kibiashara na wageni! Hasa Wasukuma. Ila ukija kwa wenyeji, mambo siyo mepesi hata kidogo.

Nimeishi miaka mingi sana Ifakara. Ila ukiilinganisha na Njombe, naona kama Njombe iko juu zaidi ya Ifakara. Ifakara ingelinganishwa na Mji kama Kilosa vile, hakika Ifakara ingetisha mbaya.

Hayo mambo ya Wenyeji hayana maana yoyote! Wenyeji wa Dar wana impact yoyote? Wenyeji wa US red Indians wana issue? Issue ni shughuli za uzalishaji na biashara ya sehemu husika!
 
Back
Top Bottom