Mji wa Ifakara ni mzuri kuliko Njombe mjini

Unaesema makambako ipo wilaya ya ludewa hebu angalia na ramani hiyo ulinganishe na vitu unavo viongea
 
Makambako haiundi wilaya ya njombe inawilaya yake inaitwa ludewa ila inaunda mkoa wa njombe wilaya ya njombe inaundwa na njombe mji na njombe vijijini

makambako iko wilaya ya wanging'ombe

ludewa ni wilaya inajitegemea
 
Nikifikiria week ilopita nimekaa Iragua siku nane kisa daraja limekatika pale stand ya nyanya,daah wabunge wa hayo maeneo miyeyusho sana.By the way nimeishi huko kiukwel mkoa wa Morogoro unahitaji kugawanywa ili kusogeza huduma za kijamii karibu sijui lini hilo bonde watalifanya kuwa mkoa
 
Ni kweli makambako iko nyuma huku kabla ya kufika Njombe, ukifika Njombe km unaelemea Songea unakata kuli pale ndiyo unapata uelekeo wa Ludewa (Monilii)
 

Dah! Nimepita sana hayo maeneo ya Lupilo, Iragua, Itete, Mtimbira, Sofi, mapaka Malinyi! Miaka hiyo ya 90, unapanda basi saa 9 za usiku!
Ukilichelewa tu, itakulazimu kusafiri tena kesho yake, au ubahatike kupanda gari la wamisheni wa Kikatoliki!

Hilo Bonde la Kilombero miaka nenda halijawahi kuwa na unafuu wa miundombinu! Ingawa kuna wasomi wengi tu wanatokea huko. Ukienda ule upande wa Mlimba, nako ni shida tu wakati wa masika. Barabara ni mbovu mpaka basi.
 
Mkuu, makambako si wilaya ya wanging'ombe?
 
Makambako haipo wilaya ya wanging'ombe ipo wilaya ya njombe wilaya ya njombe Ina halmashauri tatu na mkuu wa wilaya Ni mmoja. Watu wengi huwa wanajua hivyo no ingawa kwa Sasa makambako imeomba kujitegemea kuwa wilaya
Mkuu, makambako si wilaya ya wanging'ombe?
 
Huu upumbafu wa ku compare maeneo sijui Nan kauanzisha humu JF imekuwa kero yaan
 
Mkuu nakubaliana nawe, vile vile maumbile ya kijografia yapo tofauti: Njombe mandhari (view) yake iko vizuri sana iliyopangwa kwa mitelemko na miinuko iliyojipanga, tofauti na Ifakara bonde la mpunga na ndio maana hata nyumba za Serikali wameanua kuzijenga Kibaoni. Ifakara hata kwa Makambako haipati.
 
Njombe nimeishi miaka 3,nakujua hadi Lupembe,ukalawa,made kesho,kifanya,ikondo.

Njombe mjini ni sehemu ndogo sana,toka pale Hospital ya wilaya hadi uwanja wa ndege mji umeisha

Mji wa Ifakara, unaweza kuwa sawa kabisa kwa ukubwa na Mji wa Njombe. Ni moja ya makao makuu ya Wilaya ambazo ni kubwa. Zingine ni Masasi, Tarime, Korogwe, Nzega na kipekee mji wa Tunduma
 
Niongezee tu kwa TZ wilaya ambazo zinavibe ni pamoja Masasi, Mbinga,Kahama, Ifakara na Tunduma hizi sehemu huduma zote muhimu zipo

Daa, ndo nimoena hii post, utafikiri tulikua pamoja. Wilaya au miji hii ina compete na Manispaa nyingi tu hapa Tanzania: Masasi, Tunduma, Kahama hiyo tayari, Tarime, Ifakara ni ya pili baada ya Morogoro, Korogwe ingawa naona kama inashuka sasa, lakini Makambako nayo siyo kubwa ila inajitahidi
 

Mikoa 3 hapana, mikoa miwili ni halali kabisa, makao makuu yawe Ifakara na siyo Malinyi. Ifakara ni katikati na Centre kubwa, njia panda ya kwenda Njombe kupitia Lupembe na njia ya kwenda Songea kupitia Malinyi huko. Pia njia ya kwenda Ulanga! Kiuhalisia Ifakara ile lami inayotokea Mikumi ikikamilika, Njombe ikae mguu sawa, kwanza wana mazao mengi sana. Siyo sehemu ya kubeza hata kidogo!
 

Hayo mambo ya Wenyeji hayana maana yoyote! Wenyeji wa Dar wana impact yoyote? Wenyeji wa US red Indians wana issue? Issue ni shughuli za uzalishaji na biashara ya sehemu husika!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…