Mjini hakuna rafiki wa uhakika wote ni 'deal maker'

Mjini hakuna rafiki wa uhakika wote ni 'deal maker'

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
33,679
Reaction score
49,841
Na hii imetokea kwa vijana wengi, wakiwa mikoani kelele ni nyingi sana mara watakwambia ukija mjini tutafutane angalau tubadilishe mawazo, mazingira, na tupeane fursa.

Sasa ukifika mjini, ukiomba muonane naye, chenga zinakuwa nyingi; mara leo niko bize nimetingwa na kazi, mara nimesafiri niko nje ya jiji,mara nitakuwa studio n.k wakati mwingine hata simu yako hawapokei wakishajua umewafuata mjini, sasa unajiuliza akiwa mkoani mbwembwe ni nyingi, ila ukifika mjini na kuanza kumtafuta anakupa sababu nyingi ili msiweze kuonana.

kwa mazingira hayo, kweli mjini hakuna urafiki, urafiki ni huko mikoani na vijijini ambapo mnaweza kuombana chumvi, vitunguu, majembe n.k
 
Ni kama unavyoambiwa karibu tule alafu mtu ana sahani moja! jiongeze .....na Tanzania tulianza mapema hayo mambo...mtoto anaambiwa nenda kavae twende akirudi wazazi wamemkimbia!
Ha ha ha ha kwa hiyo mkuu hii tabia imetokana na wazazi?
 
Vijana shida mnafeki sana maisha.

Yaan mkiongea najamaa zenu. Mnawatambia sanaaaaa

Ila sasa Jamaa wanapokuja kuwatembelea

Mnaanza kuwaza, jamaa atajua ukweli[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

mkiwa wakweli wa kila kitu. Huwez mpiga chenga jamaa yako tena Mwana mliyemisiana muda mrefu
 
Watu wa Dar hao.
Hakikisha ukienda Dar uwe financially enough hao marafiki ukikutana nao tumia bila mawazo Kama wanakula Gambe wape mpka wapoteane.. next time ukirudi mbona mda wote utakua unapigiwa sim kuuliza umefika wapi..!
Tafuta hela kijana namba yako Haijafutwa.
 
hii kufeki maisha nadhani ndio tatizo kubwa
 
Watu wa Dar hao.
Hakikisha ukienda Dar uwe financially enough hao marafiki ukikutana nao tumia bila mawazo Kama wanakula Gambe wape mpka wapoteane.. next time ukirudi mbona mda wote utakua unapigiwa sim kuuliza umefika wapi..!
Tafuta hela kijana namba yako Haijafutwa.
Urafiki wa mpaka uwe na hela huo sio urafiki bora, bali hapo unakuwa umegeuzwa kuwa fursa.
 
Kumbe wewe hukumuelewa mhenga aliyesema mtegemea cha ndugu hufa maskini?

Inasemekana yeye alkuwa anazungushwa na kaka yake mkubwa, ndio akatuachia msemo huo
 
Kumbe wewe hukumuelewa mhenga aliyesema mtegemea cha ndugu hufa maskini?

Inasemekana yeye alkuwa anazungushwa na kaka yake mkubwa, ndio akatuachia msemo huo
Uko sahihi,kwa mazingira hayo inamaana kwamba unatakiwa ujipange ukiwa na shida au raha, utatue changamoto zako mwenyewe.
 
Na hii imetokea kwa vijana wengi, wakiwa mikoani kelele ni nyingi sana mara watakwambia ukija mjini tutafutane angalau tubadilishe mawazo, mazingira, na tupeane fursa. Sasa ukifika mjini, ukiomba muonane naye, chenga zinakuwa nyingi; mara leo niko bize nimetingwa na kazi, mara nimesafiri niko nje ya jiji,mara nitakuwa studio n.k wakati mwingine hata simu yako hawapokei wakishajua umewafuata mjini, sasa unajiuliza akiwa mkoani mbwembwe ni nyingi, ila ukifika mjini na kuanza kumtafuta anakupa sababu nyingi ili msiweze kuonana.

kwa mazingira hayo, kweli mjini hakuna urafiki, urafiki ni huko mikoani na vijijini ambapo mnaweza kuombana chumvi, vitunguu, majembe n.k
Maisha ya sasa hivi bro RAFIKI WA KWELI NI KIVULI CHAKO TUU...MAANA KITAKUWA NAWE MPAKA KABURINI...TAKE CARE MKUU
 
Back
Top Bottom