Habari za Jumapili ndugu zangu kaka/dada zangu wote kwa ujumla Natumaini mmeamka vema, Mimi pia mzima,
Sawa Mimi sio mwandishi mzuri Wala mwandikaji ila lengo la Uzi ni kwamba kuna situation naipitia. Nina watoto kadhaa nipo pia na mama yao, hapa nyumbani baada ya maisha kuwa sio sawa kidogo nikarudisha Mpira Nyumbani.
Changamoto zipo hazikosekani ila ndogo ndogo ila kubwa ni hii mjomba anachukia watoto wangu na hiki kinaniuma sana!
Watoto wanaweza kuwa wanacheza nje ya uwanjani wakimuona basi wanakimbia ndani kuja kwangu au kwa mama yao, yani muda wote amekasirika amenuna nuna tu mimi tukionana namsalimia tu basi imetoka maana huwezi kuchukia watoto mimi pia nikakuthamini.
Hali yangu ni mbaya sana hasa kiuchumi ni kazi ndogo ndogo za kubangaiza namuomba sana Mungu kila siku angalau nipate kwangu nitoke hapa naumia sana naona yani anafanya yote kwa sababu anajua sina pa kwenda, ndugu zangu mnisaidie mawazo, ushauri ata kama kazi nifanye.
Niwatakie Jumapili njema Ndugu zangu.