Mjomba anawachukia watoto wangu?

Mjomba anawachukia watoto wangu?

Habari za Jumapili ndugu zangu kaka/dada zangu wote kwa ujumla Natumaini mmeamka vema, Mimi pia mzima,

Sawa Mimi sio mwandishi mzuri Wala mwandikaji ila lengo la Uzi ni kwamba kuna situation naipitia. Nina watoto kadhaa nipo pia na mama yao, hapa nyumbani baada ya maisha kuwa sio sawa kidogo nikarudisha Mpira Nyumbani.

Changamoto zipo hazikosekani ila ndogo ndogo ila kubwa ni hii mjomba anachukia watoto wangu na hiki kinaniuma sana!

Watoto wanaweza kuwa wanacheza nje ya uwanjani wakimuona basi wanakimbia ndani kuja kwangu au kwa mama yao, yani muda wote amekasirika amenuna nuna tu mimi tukionana namsalimia tu basi imetoka maana huwezi kuchukia watoto mimi pia nikakuthamini.

Hali yangu ni mbaya sana hasa kiuchumi ni kazi ndogo ndogo za kubangaiza namuomba sana Mungu kila siku angalau nipate kwangu nitoke hapa naumia sana naona yani anafanya yote kwa sababu anajua sina pa kwenda, ndugu zangu mnisaidie mawazo, ushauri ata kama kazi nifanye.

Niwatakie Jumapili njema Ndugu zangu.
Pole sana !
Hapo shida ni kipato tu Mwenyezi Mungu akubariki upate kipato na kwako kwa mara nyingine, mjomba/shangazi/cousin watawapaenda wewe na familia yako

Mtu kitu !
 
Inategemea na mazingira mkuu! Huenda jamaa huko atakoenda itamlazimu kuishi mazingira yenye utata hasa kwa mwanamke! Mfano kwenye madini au kwenye zege ambapo anaweza kujikuta analala site kwenye mahema ambapo wanaume wamejaa!
Aende na mkewe nae mkewe ataungana na wamama wengine wa huko mgodini na kwenye kubeba zege kwenye kazi za kutoa huduma Kwa wafanyakazi Kama chakula, vinjwaji, sigara, sweets na mahitaji mengi tu ya binaadam.

Wakati umefika wa watu kutambua hizi sio nyakati za lelemama!!

Family inajengwa uimara wake Kwa ushirikiano wa wote baba na mama.

Siafiki Kwa family kutengana kisa changamoto za kiuchumi Kwa maana nafasi hiyo Ndio hutumika kuvunja family na pia hii umjengea picha mbaya mwenza wako Kwa kuona kwamba wewe baba/mzazi umeshindwa majukumu yako mpaka uyatelekezee Kwa wazazi wa mwenza wako.

Kiapo cha “katika shida na raha” ni muhimu sana kikaelezewa umuhimu wake na maana yake halisi Kwa kila wanandoa wapya na wale wanandoa wakongwe wakumbushwe kila mwaka kuhusu hicho kiapo.
 
Usukumani mama hana urithi kwao. Kwa ufupi huyo mwamba hapo alipo anafugwa kwa bibi yake maana hapo siyo kwao! Hapo ni kwenye makazi ya mjomba wake maana ndiye mrithi wa hapo!
Duh,kwa maoni yangu, mila mbovu hii.
 
Hawa vijana umaskini wana utafutaga wenyewe.

Mtu anajua kabisa yeye ni maskini na hali ya nyumbani kwao kiuchumi ni mbaya, Badala ya kujijenga yeye kwanza anakimbilia kuzaa watoto na kuwa na familia.

Hapo lazima umaskini umtwange kisawasawa mpaka pale akili zitakapo mkaa sawasawa.
Huu ni ukweli mchungu watu wengi wasiotaka kuukubali.

Mjomba kama nae elimu hana ni lazima atajenga chuki kwako na kwa wanao kwa sababu anawaza inawezekana umerudi kujiandalia mazingira ya kujichotea vya urithi.
 
Nyie huwa mkifanikiwa mna maneno sana, ohoo tuliteswa, tulinyanyaswa. Wewe Ulirudisha mpira golini kwa sababu ya matatizo ya kiuchumi, ukaona ni sawa kabisa.

Mjomba wako unaweza kuta naye ana matatizo yake na hana pa kuyapeleka. Na mtu kuwa kimya au serious haina maana kwamaba anamchukia mtu yeyote, achilia mbali wanao. Kuna watu wako kimya wanatafakari, ila wewe unaanza kuji hisi kwa sababu uko kwake au kwao.

Tizama kila mtu ana handle shida zake tofauti, mpo nyie mnao lia lia na wapo watu wako kimya kimya kivyao vyao.
Acha kujihisi utagombana na watu bila sababu.

Hujawahi kuongea na huyo mjomba wako akakwambia anawachukia wanao, au wewe na mkeo. lakini unahisi tu anawachukia wanao.

Nakwambia siku ukiwa na kwako nyie ndio huwa mnaanza kulipiza visasi hata bila kuelewa unamlipizia nani, yani mis directed hunger.

Acha fikra hasi, ongea na watu kwanza ndio uwe na conclusion ya mawazo yako.
 
Unavyo tafsiri maisha usidhani kila mtu anaya tafsiri hivyo hivyo.

Nilisha kwama katika maisha na nili hustle kivyangu nikatoboa.

Sikutegemea mtu yeyote aje anipe msaada na wala sitegemei msaada wa kiumbe chochote kile.

Nakwambia hivi, matatizo mengi maishani na umaskini huletwa na uzembe na ujinga.

Wewe kama unajijua bado huna uwezo wa kuhudumia watoto, Kwa nini uzae?

Au unazaa ukitegemea uje usaidiwe?

Maisha yanakupa unachotaka cha msingi uwe na mipango madhubuti na imara.

Sasa wewe unazaa watoto halafu wewe mwenyewe hali yako ya kiuchumi ni mbaya, Halafu utegemee maisha yatakuwa marahisi kweli?
Ndio maana mseven alisema mtu mpumbavu, mvivu ni ngumu kuishi nchi zilizoendelea, lazima utakufa tu, lkn kwa africa waweza kuishi kwa vizinga maishani yako yote.
 
Pole mzee.... mwanaume kushindwa kulinda familia yake ni stress kubwa sana
 
Sina ujuzi ila kazi yoyote naweza Fanya ikiwa sijui ukinipa maelekezo nafanya
Mkuu sikupangii cha kujibu lakini, hili jibu ni jepesi sana kwa mtu alie kwenye hali kama yako.

Hii inaleta tafsiri kuaa hiyo hali unayopitia pengine wewe ndo sababu...huwezi niambia una mke na watoto eti huna ujuzi wowote.

Mwanzo ulikua unafanya kazi gani? Jieleze mkuu watu wanataka kukusaidia, halafu wewe unasema sina ujuzi wowote. Kweli?

Jiongeze hapo kamanda.
 
Back
Top Bottom