Mjomba anawachukia watoto wangu?

Mjomba anawachukia watoto wangu?

Nilizingatia sana mpaka nilipofikisha 31 ndipo nikamleta Mtanganyika mpya nikiwa na utulivu kiakili na kiuchumi.
Hawa vijana wanadhani kuleta mtoto duniani ni kama kuangua embe mtini.

Wanazaa hovyo hovyo tu, Halafu wanaanza kutia huruma na kusumbua watu kutaka ushauri na msaada.

Ngoja maisha yawatwange kisawasawa mpaka pale akili zitakapo funguka.
 
Pole mkuu! Hapo dawa ni kuondoka hapo nyumbani japo hujafafanua ni nyumbani kwa nani hadi mjomba naye awepo!

Usijefanya makosa ukahama wewe bila watoto na mke!
Kweli mkuu
Pole mkuu! Hapo dawa ni kuondoka hapo nyumbani japo hujafafanua ni nyumbani kwa nani hadi mjomba naye awepo!

Usijefanya makosa ukahama wewe bila watoto na mke!
Mkuu itakua yupo kwa shemeji yake ndiyo ila vijana tukioa mambo yakiwa magumu ukitaka kurudisha majeshi tunatakiwa turudishe majeshi kambini kwetu kwa Baba na Mama wao hawata Wachukia mke na wajukuu wao.
 
Ilikuwaje hadi ukawa mpumbavu kuhamia upande wa mama yako? HAPO SIO KWENU HAMA HARAKA SANA.
Mkuu Tamaduni zinatofautiana jamii na jamii kwa jamii za watu wa pwani wao kwa mfano wewe unaweza kwenda kuishi kwao mke wako yani ukweni mkaishi pamoja kama kwenu au kwako.
 
Huko sio kwenu man!!?

Hakuna urithi wako huko ndio Maana jamaa kakunja ndita!!!

Nenda kwa baba mwambie nimekuletea wajukuu halafu Ganda hapo hapo Hanna kuondoka!!

Pole sana man!
Kweli Mkuu uko siyo kwao mara mia pangekua kwa Kaka yake au mdo wake .
 
Daah, Mkuu naona hujamuelewa Mkuu Etugrul Bey


Kimsingi maisha Kama maisha Ni fumbo Yana Siri Sana.


Unaposema ulifanikiwa Bila kusaidiwa na mtu na ukatoboa hiyo isiwe assumptions yako kuwa kila mtu anaweza kupambana Bila kushikwa mkono na akafanikiwa.


Huyo mtoa mada kabla hayajamkuta alikuwa yupo vizuri that's why akaona ajenge familia. Kilichomkuta Ni sehemu ya maisha ambayo hata ww yanaweza kukuta muda wowote na wakati wowote.

Kumtukana na kum,beza sio busara Zaidi ilibidi umtie moyo WA kupambana Zaidi ili atoke apo alipo sasa.


Kuwa Kwenye wakati mzuri Kwa sasa kiuchumi haimaanishi utakuwa ivyo miaka yote hata Kama unafanya juhudi za makusudi kuepuka kuanguka kiuchumi badae.

Maisha Ni fumbo Mkuu, punguza kubeza walioanguka sababu Kwenye maisha Kuna kukosea, kujifunza na kunyanyuka upya.


Ww kuwa na nguvu ya kiuchumi Kwa sasa sio sababu ya kuwabeza wengine na Sina hakika Kama utaweza kujua kila kitu na kila mbinu ya kuendelea kuwa ulipo hapo Leo.


Zaidi Sana muombe Mungu Mkuu, binadamu pekee yake hawezi kufanikiwa Kwa kila kitu na hata kujua yajayo.
Nimeipenda hii
 
Maisha si fumbo.

Hizi ni mentality mlizo jiwekea kichwani zisizo na uhalisia wowote ule

Kwa hiyo unasubiri uje ushikwe mkono ndipo ufanikiwe?

Kwamba usiposhikwa mkono hautafanikiwa?

Kama alikuwa yupo vizuri, Kwa nini arudishe mpira kwa kipa?

Hauhitaji kutiwa moyo ili upambane.
Kichwa chako lazima kijiwekee mentality ya kupambana muda wote ili usianguke kiuchumi.

Sikweli. Sio matajiri wote wana anguka.

Matajiri wengi tu wanazidi kuwa matajiri na maskini wengi tu wanazidi kuwa maskini.

Baadhi ya matajiri wananguka na vivyo hivyo na maskini wanazidi kuanguka kwenye umaskini wao.

Maisha sio fumbo. Maisha ni mikakati na mipango.

Hakuna mtu aliyebezwa. Hapa tuna elezana uhalisia wa maisha ulivyo.

Huyo Mungu hayupo na hajawahi kuwepo kusaidia kitu chochote kile.

Ndio maana hata mleta mada licha ya kumuomba sana huyo Mungu amsaidie,

Mungu huyo Kashindwa kumsaidia mpaka amefikia hatua ya kuja kwetu sisi binadamu wenzie tumsaidie ushauri na mawazo.
Watu msio mwamini mungu huwa mnadhani mambo yanafanikiwa kwa jitihada zenu tu basi

ila naamini kauli ya mwamba mmoja aliwahi sema wasio mwamini mungu iko shida pahala
 
Huyo mjamba wako anafuata nini kwenu,
Kati yako na yeye nani yupo kwao?
Kweli uandishi nao ni kipaji! Jamaa hata halijaeleza vizuri kama hapo linapoishi ni kwa wazazi wa lenyewe au linaishi kwa mjomba wake!
 
Ni upande wa ujombani mkuu kwao na mama
Na wewe huko umeenda kufanya nini? Huna upande wa baba yenu? Wasukuma na sisi tumezidi yaani mtu una mke na watoto unataka uendelee kuishi kwa bibi yako mpaka sasa hivi? Halafu na huyo uncle wako naye takataka tu, yaani na uzee wote huo bado anafugwa kwa mamake? Au dish limeyumba nini?
 
huyo mkeo hana kwao? aende kwao wewe endelea kujitafuta kawe muwazi kwao kwamba hali yako ya kuchum sio nzur akae hapo kwa usalama wake na watoto ukianza kujipata unachukua familia yako,hivi na mama ako mzaz anaishi hapohapo?
Kwamba?!?

Na bado mnapiga kelele hakuna family imara siku hizi!?

Huyo mwanamke hawezi kuwa na mumewe bega Kwa bega kuhakikisha jamaa anarejea katika shughuli za kiuchumi na kushirikiana nae kutengeneza Kwa ajili ya Watoto wao?

Hao Watoto Ndio wakupelekwa Kwa bibi yao/zao then baba na mama wapambane kuhakikisha wanarejesha family yao chini ya paa moja.

Family
Family
Family
 
Habari za Jumapili ndugu zangu kaka/dada zangu wote kwa ujumla Natumaini mmeamka vema, Mimi pia mzima,

Sawa Mimi sio mwandishi mzuri Wala mwandikaji ila lengo la Uzi ni kwamba kuna situation naipitia. Nina watoto kadhaa nipo pia na mama yao, hapa nyumbani baada ya maisha kuwa sio sawa kidogo nikarudisha Mpira Nyumbani.

Changamoto zipo hazikosekani ila ndogo ndogo ila kubwa ni hii mjomba anachukia watoto wangu na hiki kinaniuma sana!

Watoto wanaweza kuwa wanacheza nje ya uwanjani wakimuona basi wanakimbia ndani kuja kwangu au kwa mama yao, yani muda wote amekasirika amenuna nuna tu mimi tukionana namsalimia tu basi imetoka maana huwezi kuchukia watoto mimi pia nikakuthamini.

Hali yangu ni mbaya sana hasa kiuchumi ni kazi ndogo ndogo za kubangaiza namuomba sana Mungu kila siku angalau nipate kwangu nitoke hapa naumia sana naona yani anafanya yote kwa sababu anajua sina pa kwenda, ndugu zangu mnisaidie mawazo, ushauri ata kama kazi nifanye.

Niwatakie Jumapili njema Ndugu zangu.
Mungu akusaidie. Siku moja mjomba atamani kucheza na wanao
 
Unaishi kwa mjomba wako ama na mjomba nae anaeishi kwa mama yake, umerudisha mpira kwenye nyumba ya urithi ya mama yako.
 
Wew unamlaumu na kumchukia wakati wewe ndio umeyasababisha chanzo ni wewe huwezi laumu choo kinanuka wakati wewe ndie umekunya huko
 
Watu msio mwamini mungu huwa mnadhani mambo yanafanikiwa kwa jitihada zenu tu basi
Hata wewe umefanikiwa kwa juhudi zako wala si Mungu.

Kama Mungu ndio anakusaidia kufanikiwa, Acha kazi yako au biashara yako uone kama huyo Mungu atakuwa na uwezo wa kukusaidia yeye kama yeye.
ila naamini kauli ya mwamba mmoja aliwahi sema wasio mwamini mungu iko shida pahala
Kuamini unaweza kuamini hata uongo na wala hukatazwi kuamini hivyo.

Ila sihitaji kuamini uwepo wa huyo Mungu, Nahitaji kujua kwa uthibitisho na uhakika.
 
Kwamba?!?

Na bado mnapiga kelele hakuna family imara siku hizi!?

Huyo mwanamke hawezi kuwa na mumewe bega Kwa bega kuhakikisha jamaa anarejea katika shughuli za kiuchumi na kushirikiana nae kutengeneza Kwa ajili ya Watoto wao?

Hao Watoto Ndio wakupelekwa Kwa bibi yao/zao then baba na mama wapambane kuhakikisha wanarejesha family yao chini ya paa moja.

Family
Family
Family
ina make sense
 
Mkuu Tamaduni zinatofautiana jamii na jamii kwa jamii za watu wa pwani wao kwa mfano wewe unaweza kwenda kuishi kwao mke wako yani ukweni mkaishi pamoja kama kwenu au kwako.
Huo ni utamaduni wa kishenzi sana.
 
Usukumani mama hana urithi kwao. Kwa ufupi huyo mwamba hapo alipo anafugwa kwa bibi yake maana hapo siyo kwao! Hapo ni kwenye makazi ya mjomba wake maana ndiye mrithi wa hapo!
Unaishi kwa mjomba wako ama na mjomba nae anaeishi kwa mama yake, umerudisha mpira kwenye nyumba ya urithi ya mama yako
 
Kwamba?!?

Na bado mnapiga kelele hakuna family imara siku hizi!?

Huyo mwanamke hawezi kuwa na mumewe bega Kwa bega kuhakikisha jamaa anarejea katika shughuli za kiuchumi na kushirikiana nae kutengeneza Kwa ajili ya Watoto wao?

Hao Watoto Ndio wakupelekwa Kwa bibi yao/zao then baba na mama wapambane kuhakikisha wanarejesha family yao chini ya paa moja.

Family
Family
Family
Inategemea na mazingira mkuu! Huenda jamaa huko atakoenda itamlazimu kuishi mazingira yenye utata hasa kwa mwanamke! Mfano kwenye madini au kwenye zege ambapo anaweza kujikuta analala site kwenye mahema ambapo wanaume wamejaa!
 
Back
Top Bottom