Mjomba wangu anataka kuchomwa akifa, familia yake imekataa kaja kwangu, Nichukue uamuzi upi??

Ni uamuzi wa mtu, nami nimeamua nikifa nizikwe kimila, sitaki mambo ya Biblia au Koran, utumike utamaduni wangu wa asili na sio Wazungu au Waarabu.
 
Waafrika huwa hatuheshimu kabisa maamuzi ya watu. Mwambie anunue kabisa kuni na aandae eneo la kuchomea.
 
Yeye ndiye kataka mwili wake uchomwe nyie shida nini? Mwambieni yeye anunue magogo kabisa yawepo hapo, msipo mchoma atakuwa anawaijia na kuni begani ukoo mzima [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapana usimdanganye, mwambie ajaribu kufutilia Mahakamani ajue kama linafaa kisheria
 
Msipomchoma maiti take itagoma kuzikwa. Yani hamtafanikiwa kumzika hadi mtakapomchoma
 
Msikilize na mkubaliane mapema.. Akidondoka leo hamjaweka sawa itakula kwenyu
 
Achomwe tu hakuna namna,mpeleke kwa wahindi wenye utamaduni hio wawape maelekezo
 
Cha msingi mwambie ukweli Ili ajue hutaweza kumtekelezea jambo lake.
 
Kama nyie hamuwezi akatafute hekalu la wahindu au wabudha awaachie huo wosia.
 
pagumu mkuu.

ila nchi za wenzetu huo ni uamuzi wa mtu binafsi, na wengine wanagawa kabisa viungo vyao kwa ajili ya research za spitali au kuwasaidia watu wengine.
ni nchi za wenzetu wenye tamaduni zao.

Hii ni Tz
 
Suala rahisi sana. Mshauri uncle aende kule Jamatini yoyote ya Wahindi, ambako ndipo wanaporatbu hatua za mwisho za watu wao.

Awataarifu kwamba, japo yeye sio kabacholi, lakini anakuballiana sana na utaratibu wao wa kumalizia hatua ya mwisho ya mwanadamu. Na kwamba angependelea wamfanyie hivyo (cremate) atakapofariki

Wadosi wapo vizuri sana kwenye kuchanganya biashara na Imani. Kitakachofuata, ni uncle kuambia gharama za hiyo shughuli ili alipe na awe kwenye orodha.

Mtihani alionao mjomba wako ni kwamba, kwa vile anaishi katika jamii ambayo haikubaliani na hilo suala; kifo kikimtokea kijijini, basi familia yake watamzika tu. Akifia nje ya hapo anapoishi, au nje ya nchi, lazma afukiwe na maiti iliwe na funza. Utamaduni huo haupo na haukubaliki na walio wengi.

Binadamu wa siku hizi tupo mguu na njia sana. Huwezi kujua umauti utakukuta wapi. Hivyo basi, uncle awe muangalifu asipoteze pesa zake kwa wadosi. Akubali tu kufukiwa na kuliwa na funza.
 
ana kichaa kwani yeye baniani. kama kwake kuchomwa muhimu mwambie ajichome ndo afe kuondoa utata
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…