Mjomba wangu anataka kuchomwa akifa, familia yake imekataa kaja kwangu, Nichukue uamuzi upi??

Mjomba wangu anataka kuchomwa akifa, familia yake imekataa kaja kwangu, Nichukue uamuzi upi??

Ni uamuzi wa mtu, nami nimeamua nikifa nizikwe kimila, sitaki mambo ya Biblia au Koran, utumike utamaduni wangu wa asili na sio Wazungu au Waarabu.
 
Waafrika huwa hatuheshimu kabisa maamuzi ya watu. Mwambie anunue kabisa kuni na aandae eneo la kuchomea.
 
Yeye ndiye kataka mwili wake uchomwe nyie shida nini? Mwambieni yeye anunue magogo kabisa yawepo hapo, msipo mchoma atakuwa anawaijia na kuni begani ukoo mzima [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni uncle wangu yupo kwenye 50 huko.

Kwa kipindi kama cha miaka mitatu amekuwa akiwa na msimamo wa kutaka kuchomwa akifa.

Familia yake ilikataa kwa hio kaja kwangu maana tupo karibu.

nami sio muumini wa hizi ishu, huwa nampa tu sapoti ya kinafki 😁.

Je nimwambie ukweli sitaweza kutekeleza anachotaka au nimdanganye tu ili kumfurahisha ila kama kawaida maafa yakimkuta atazikwa tu kwa utaratibu wa kawaida.
Hapana usimdanganye, mwambie ajaribu kufutilia Mahakamani ajue kama linafaa kisheria
 
Msipomchoma maiti take itagoma kuzikwa. Yani hamtafanikiwa kumzika hadi mtakapomchoma
 
Ni uncle wangu yupo kwenye 50 huko.

Kwa kipindi kama cha miaka mitatu amekuwa akiwa na msimamo wa kutaka kuchomwa akifa.

Familia yake ilikataa kwa hio kaja kwangu maana tupo karibu.

nami sio muumini wa hizi ishu, huwa nampa tu sapoti ya kinafki [emoji16].

Je nimwambie ukweli sitaweza kutekeleza anachotaka au nimdanganye tu ili kumfurahisha ila kama kawaida maafa yakimkuta atazikwa tu kwa utaratibu wa kawaida.
Msikilize na mkubaliane mapema.. Akidondoka leo hamjaweka sawa itakula kwenyu
 
Achomwe tu hakuna namna,mpeleke kwa wahindi wenye utamaduni hio wawape maelekezo
 
View attachment 2028494

Kwa kipindi kama cha miaka mitatu amekuwa akiwa na msimamo wa kutaka kufanyiwa mazshi kwa kuchomwa mauti yakimkta na niende kupeperusha majivu yake kijijini, sehemu aliyokuwa akiipenda.

Familia yake ilikataa kwa hio kaja kwangu maana tupo karibu.

Huduma hii ya mazishi natambua kwamba ipo hata hapa nchini, inaitwa cremation, lakini imezoeleka kwa kiasi kikubwa kutumika na wahindi wanaofata mila na tamaduni zao.

Kwa tamaduni zetu hizi za hapa kwetu na hata kwa dini, huu utaratibu haujazoeleka kiukweli, kwa hiyo hata mimi siwezi kumtekelezea anachotaka, pia hata familia yake nayo imekataa, sipendi kuanzisha taharuki.

Huwa nampaga tu sapoti ya kinafki [emoji16] maana ni mjomba tuliezoeana sana.

Je nimwambie ukweli kwamba sitaweza kutekeleza anachotaka au nimdanganye tu ili kumfurahisha ila kama kawaida maafa yakimkuta atazikwa tu kwa utaratibu wa kawaida.
Cha msingi mwambie ukweli Ili ajue hutaweza kumtekelezea jambo lake.
 
Kama nyie hamuwezi akatafute hekalu la wahindu au wabudha awaachie huo wosia.
 
pagumu mkuu.

ila nchi za wenzetu huo ni uamuzi wa mtu binafsi, na wengine wanagawa kabisa viungo vyao kwa ajili ya research za spitali au kuwasaidia watu wengine.
ni nchi za wenzetu wenye tamaduni zao.

Hii ni Tz
 
Suala rahisi sana. Mshauri uncle aende kule Jamatini yoyote ya Wahindi, ambako ndipo wanaporatbu hatua za mwisho za watu wao.

Awataarifu kwamba, japo yeye sio kabacholi, lakini anakuballiana sana na utaratibu wao wa kumalizia hatua ya mwisho ya mwanadamu. Na kwamba angependelea wamfanyie hivyo (cremate) atakapofariki

Wadosi wapo vizuri sana kwenye kuchanganya biashara na Imani. Kitakachofuata, ni uncle kuambia gharama za hiyo shughuli ili alipe na awe kwenye orodha.

Mtihani alionao mjomba wako ni kwamba, kwa vile anaishi katika jamii ambayo haikubaliani na hilo suala; kifo kikimtokea kijijini, basi familia yake watamzika tu. Akifia nje ya hapo anapoishi, au nje ya nchi, lazma afukiwe na maiti iliwe na funza. Utamaduni huo haupo na haukubaliki na walio wengi.

Binadamu wa siku hizi tupo mguu na njia sana. Huwezi kujua umauti utakukuta wapi. Hivyo basi, uncle awe muangalifu asipoteze pesa zake kwa wadosi. Akubali tu kufukiwa na kuliwa na funza.
 
View attachment 2028527

Kwa kipindi kama cha miaka mitatu amekuwa akiwa na msimamo wa kutaka kufanyiwa mazshi kwa kuchomwa mauti yakimkuta

Sababu zake mpaka sasa hazijaniingia akilini, yeye hataki mwili wake uoze taratibu, sijui mambo ya mwili kutumika msukule, kuhofia kwamba ataamka akizikwa 😂 😂 n.k.

Familia yake ilikataa kwa hio kaja kwangu, kaniomba nimsaidie hio ishu na pia niende kupeperusha majivu yake kijijini sehemu aliyokuwa akiipenda utotoni.

Huduma hii ya mazishi natambua kwamba ipo hata hapa nchini, inaitwa cremation, lakini imezoeleka kwa kiasi kikubwa kutumika na wahindi wanaofata mila na tamaduni zao.

Kwa tamaduni zetu hizi za hapa kwetu na hata kwa dini, huu utaratibu haujazoeleka kiukweli, kwa hiyo hata mimi siwezi kumtekelezea anachotaka, pia hata familia yake nayo imekataa, sipendi kuanzisha taharuki.

Huwa nampaga tu sapoti ya kinafki 😁 maana ni mjomba tuliezoeana sana.

Je nimwambie ukweli kwamba sitaweza kutekeleza anachotaka au nimdanganye tu ili kumfurahisha ila kama kawaida maafa yakimkuta atazikwa tu kwa utaratibu wa kawaida.
ana kichaa kwani yeye baniani. kama kwake kuchomwa muhimu mwambie ajichome ndo afe kuondoa utata
 
Back
Top Bottom