Mjue gwiji wa sheria nchini Dkt. Lamwai

Shida ya nchi hii haijalishi una hoja una vifungu vya sheria kama inagusa maslahi ya wakubwa utaangukia pua.
Hao wakubwa wanajiona miungu watu...ila mwamba kwa namna flan alikuwa very bright katika kusema ukwel
 
Huyu Dr masumbuko kuna muda alikuwa anawatesa Sana hata lytonga nae kuna kipindi alitoka kabisa kwenye reli

Walid Aman huyu nilikuwa namskia Tu

Ilikuwa ubabe na undava Sana
 

Mara nyingi watu walioko serikalini huwa mbumbumbu sana kifikra, hivyo utumia nguvu sana kufanya mambo yao, akitokea mtu kumupinga huyo mtu huwa Ni adui number moja. Yuko tayari kuuwa ,kuumiza aonekane yuko right, mpaka leo ukipinga hoja za watawala basi wako tayari kupoteza kabisa. Mfano akina Dr Nshala, Mwambukusi etc.
 
Yote mema ya Lamwai yalifutika baada ya kuamua kuwa mwanaCCM, Lamwai akawa mjinga, mpumbavu na mnafiki.
CCM iko kuharibu akili za watu tu.

Poor Lamwai.
 
hivi alikuwa na watoto twenty ngapi? pesa na umaarufu ni shetani wa kwanza wa wanawake hakika.
 
Upo sahihi huwa hawataki wakosolewe kabisa
 
Mwaka 1995 aligombea ubunge wa Ubungo kupitia chama cha NCCR Mageuzi na kupata uungwaji mkono mkubwa sana. Siku moja kabla ya kupiga kura ilikuwa siku ya kufunga kampeni kwa wagombea.

Lamwai alichagua kufungia kampeni zake viwanja vya Mwembechai wakati huohuo mgombea Urais wa CCM alikuwa akifunga kampeni zake viwanja vya Jangwani. Baada ya kumaliza mkutano wake Lamwai akaondoka kupitia barabara ya Kawawa, akisindikizwa na maelfu ya watu na gari yake ikisukumwa. Hayakuwa mapenzi bali mahaba. Barabara ya Morogoro na ile ya Kawawa zilitapika watu.

Walipofika mataa ya Magomeni wakakutana na msafara wa mgombea Urais wa CCM ukiwa na ving’ora na polisi kibao. Msafara wa Ben na polisi wake ukatulizwa na wafuasi wa Lamwai waliokuwa wengi kiasi cha kufurika barabara. CCM na wafuasi wao wakataka kutumia nguvu ili mgombea wao apite kwanza.

Polisi kama kawaida yao wakataka kuingilia kati kwa kupiga mabomu lakini baada ya kushauriana wakaamua kutumia busara kwa kuwaomba wafuasi wa Lamwai wapishe njia ili msafara wa Ben upite.

Kwa mara ya kwanza katika historia ya siasa za taifa hili, msafara wa mgombea Urais wa chama tawala ukaomba ruhusa ya kupita katikati ya mafuriko ya wafuasi wa mgombea ubunge. Bila shaka kitendo hiki kilimuuma sana Ben, ila bahati mbaya hajaelezea kwenye kitabu chake cha MY LIFE, MY PURPOSE. Labda alisahau au anaweza kuelezea wakati mwingine akipata fursa ya kufanya hivyo.

Anyway, tuyaache hayo. Lamwai akashinda na kuwa Mbunge machachari sana mwenye nguvu ya ushawishi na aliyeshiba hoja. Pia akaendelea na taaluma yake ya sheria akiwasaidia watu mbalimbali na chama chake mahakamani kama Wakili. Moja ya kesi zilizompa umaarufu mkubwa ni ile ya Kihiyo. Leo ‘kihiyo’ ni neno lisilo rasmi linalomaanisha mtu mjinga, zwazwa, au goigoi lakini asili ya neno hilo ni Dr.Masumbuko Lamwai.

Mwaka 1995 Ramadhani Kihiyo alichaguliwa kuwa Mbunge wa Temeke kupitia chama cha mapinduzi (CCM). Katika Uchaguzi huo Kihiyo alipata kura 37,303 kati ya kura zote 57,152 zilizopigwa........itaendelea
 
Chama cha NCCR Mageuzi kupitia Mwanasheria mkuu wa chama hicho Dr.Masumbuko Lamwai kiliweka pingamizi mahakamani kudai kuwa Kihiyo alivunja sheria ya uchaguzi Na.1 ya mwaka 1985 kwa kufanya vitendo visivyokua vya uadilifu wakati wa kampeni zake.

NCCR Mageuzi ilimtuhumu Kihiyo kudanganya kuhusu Elimu yake wakati wa kampeni kama njia ya kushawishi wananchi kumpigie kura. Lamwai, aliiambia Mahakama kuwa Kihiyo alidanganya wananchi wa Temeke kuwa yeye ni Mhandisi wa maji aliyehitimu Chuo cha Ufundi DIT wakati huo kikiitwa Dar Tecnical College, jambo ambalo halikuwa kweli.

Kihiyo anadaiwa kujiita Mhandisi wa maji alipopeleka gari la maji wilayani Temeke na kugawa maji safi bure kwa wananchi siku mbili kabla ya uchaguzi. Lamwai alidai mahakamani hapo kuwa hiyo ilikuwa rushwa.

Sehemu ya Mahojiano kati ya Kihiyo na Wakili Lamwai kama yalivyochapishwa na gazeti la "Daily News" la May mwaka 1996 ilikua kama ifuatavyo;

Lamwai: Unasema ulihitimu chuo cha ufundi DIT mwaka 1986?
Kihiyo: Ndio.
Lamwai: Unajua foundry? (mashine ya kuyeyusha vyuma)
Kihiyo: Hapana, simjui mtu huyo (vicheko).
Lamwai: Kuna idara ngapi ndogo katika idara ya uhandisi mitambo (mechanical engineering department)?
Kihiyo: Zipo tatu. Chumba cha injini, chumba cha pampu na chumba cha matengenezo (vicheko).
Lamwai: Unamfahamu aliyekuwa mkuu wa chuo wakati ukisoma?
Kihiyo: Hapana simjui.
Lamwai: Nani aliyekua Afisa Usajili?
Kihiyo: Kuhanga.
Lamwai: Hapana, Kuhanga alikua Makamu mkuu wa chuo kikuu cha Dar es Salaam.
Lamwai: Lini ulianza masomo yako DIT?
Kihiyo: Sikumbuki (vicheko).
Lamwai: Nini kirefu cha VTC (Vocational Training Centre)?
Kihiyo: National Committee Centre (vicheko).
Lamwai: Unaweza kudhibitisha elimu yako mbele ya mahakama hii kwa kuleta vyeti vyako vya taaluma?
Kihiyo: Ndio.

Lamwai aliomba Mahakama imuagize Kihiyo kuleta vyeti vyake vya taaluma. Kihiyo alipewa siku 7 lakini alishindwa kufanya hivyo. Siku ya kesi ilipofika Kihiyo aliiomba Mahakama imuongezee siku mbili zaidi aendelee kuvitafuta kwa sababu hakumbuki alipoviweka. Pamoja na kuongezewa siku mbili bado alishindwa kuviwasilisha.
 
Yote mema ya Lamwai yalifutika baada ya kuamua kuwa mwanaCCM, Lamwai akawa mjinga, mpumbavu na mnafiki.
CCM iko kuharibu akili za watu tu.

Poor Lamwai.
Wapo wanaomjua Dr Masumbuko kama Mhadhiri Mwandamizi wa Sheria na alifundisha na kuwawezesha wengi kuwa Wanasheria na Mawakili na wengine hadi wamefikia kuwa Majaji

kuna watu walionewa kwny kesi na mashauri mbalimbali akawasaidia wakashinda

kwangu alikuwa Mtu anaenihamasisha kwny uwekezaji kwny kilimo akinipeleka kwa gari lake mwenyewe hadi Shambani kwake Bagamoyo na kuona mafanikio kwny uwekezaji wake

Mjinga ni yule anaetaka watu wote wamtazame mtu katika angel moja anayotaka yeye
 
ukweli ni kwamba, lamwai ni mtu aliyewafanya watu wengi sana wasomee sheria kutokana na umahiri wake, watu waliipenda sheria kwa kumwangalia yeye. hilo ameacha kama legacy.
 
we ni wale wachaga wapumbavu siyo? Mkoa adhimu maana yake nini. Kima we
 
wewe umezaliwa juzi, ni manguli wachache sana walishawahi kutokea Tanzania waliomzidi Lamwai, hao siwajui. hata Tundu Lisu na wote uliowataja walijifunza na kupata moyo na uzoefu toka kwa Lamwai. huyu jamaa alikuwa noma.
 
Kwa hiyo Lipumba hajaelimika?
 
Huyu Dr masumbuko kuna muda alikuwa anawatesa Sana hata lytonga nae kuna kipindi alitoka kabisa kwenye reli

Walid Aman huyu nilikuwa namskia Tu

Ilikuwa ubabe na undava Sana
Dr Walid Aman Walid Kabourow ana record yake

1) Katibu Mkuu wa Chadema
2) Makamu Mwenyekiti wa Chadema Taifa
3) Mbunge wa kwanza wa Jimbo wa Chadema
4) Mbunge wa Kwanza wa kutokea Upinzani baada ya kufanyika uchaguzi mdogo 1994
5) Kijana aliefungwa na kufukuzwa shule kwa kuchana kadi ya TANU na ya Baba wa Taifa, wa pili akiwa Hayati Mchungaji Christopher Mtikila
6) Kiongozi wa Kitaifa wa kwanza kutoka Chadema kuunga mkono juhudi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…