kuna mawakili kama Lamwai, watu walikuwa wakisikia tarehe atakayokuwepo mahakamani, wanaenda tu kumwangalia kujifunza hata anavyoargue tu, wanafunzi na mawakili wachanga tulikuwa tunaenda kujifunza anavyopangilia hoja na kupangua mashambulizi. alikuwa shule kabisa enzi zake, though alipokuja kuzeeka na mambo mengi ya sheria yakabadilika hakuwa na uwezo wa kujisomea mambo mapya vijana damu mbichi ambao ni digitali wakawa wanampiga sana za uso, yeye anakuja na mauzoefu na misimamo yake ile ya zamani,kijana anamsubiria tu amalize afu anaongea kidogo tu kwa misimamo ya sasa. hapo ndio tulikuwa tunamchakaza.
sheria ni dynamic alafu ukiwa mwanasheria wewe ni mwanafunzi, utasoma maisha yako yote. kuna misimamo ya sheria inabadilika kila kukicha, zamani walikuwa wanasoma hardcopy, digitali ikaja na electronic, sheria na kesi law tunapat aelectronic, tukasumbua sana wazee wasiopenda computer na wengi wakaamua kustaafu au kukimbilia kwenye vyuo kufundisha.