View attachment 2795908
Nenda, pita pote, mji kwa mji, kijiji kwa kijiji. Uliza nani mwamba wa sheria, Tena usisahau kupita kwa
Wanazuoni wa kizazi cha 21 *uliza hilo swali, Pita *Udom, Udsm, Mzumbe, Saut, Tudarco mpaka,
Ruco kwa wakatoliki. Wote watakujibu Gwiji wa sheria ni
Kibatala na
Tundu lissu, wakienda mbali watamtaja Mnyakusa
wakili Mwabukusi wa Mwanjelwa.
Sasa acha hao wote, kuna huyu mwamba ambaye kawapiku wote,
Rekodi yake haijawahi kuvunjwa na wote hao. Ubaya ni kuwa Hakufanya kazi zake kipindi Watoto wa Mkapa na JK tunazaliwa.
Huyu Mwamba
alizitesa mahakama za Taifa hili Mpaka zikakubali, Hayati Jaji kisanga na Nyalali waliukubali mtikiso wa Mwamba huyu haijawahi kutokea.
Huyu Ndiyo
Dr Masumbuko Mahunga Selasini Lamwai. almarufu
Dr Lamwai, mzaliwa wa mkoa adhimu wa kilimajaro aliyezikataa zile mbichi na kuiheshimisha tasnia ya uwakili nchini.
Kwanza ni
Genius vibaya mno, Alipoenda kusoma
Chuo kikuu Cha Oxford- Uingereza aliwapiga na kitu kizito wazungu, aliwaambia yeye anao uwezo wa kusoma miaka miwili kozi ya miaka minne. Wakamjaribu, Mwamba akagraduate na kuwaacha wazungu wakomae na miaka minne.
Alihitimu PhD ya
Criminal & Procedural law kwa miaka miwili tu badala ya minne. huu utaratibu ulikuwepo pale chuoni.
Mpaka sasa anatajwa kuwa ndiye
Mwanafunzi pekee kutoka afrika aliyewahi kuhitimu hiyo fani kwa Miaka miwili.
Dr Lamwai alikuwa wakili matata Sana. Aliingia Bungeni kama
Mbunge wa jimbo la ubungo mwaka 1995. Akiwa Bungeni aligoma kuapa kiapo cha
utii kwa Rais. Akatoa hoja kuwa Bunge ni muhimili unaojitegemea, hivyo, sio Sawa mbunge kuapa kiapo cha utii kwa Rais, mwamba akamfundisha Spika dhana ya
Separation of power, akampa vifungu konki
Spika Pius Msekwa.
Spika Msekwa, akaamuru
sheria ya kiapo cha utii irekebishwe na
kufuta kipengele cha wabunge kuapa utii kwa Rais, wabunge wote walirudia kuapa upya mwaka huo na mpaka sasa wabunge hawaapi kiapo cha utii kwa Rais kwasababu ya ufundi wa Dr lamwai.
Dr Lamwai aliwahi kumshikisha adabu
waziri mmoja aliye kuwa mwanamama. Alimpiga
cross examination ya kichokozi kinoma, alimuuliza;
"Inaonekana wewe ni Malaya Sana?", waziri akachukia, akaanza kutukana hovyo hovyo mahakamani.
Mwamba akatoa picha za Watoto wanne wa yule waziri akamuuliza;
"Hawa ni wanao?", Waziri akakubali. Wakili lamwai akatoa picha za wanaume wanne akamwambia;
iambie mahakama Hawa ni Akina nani?. Waziri akainamisha kichwa kwa aibu. Basi umalaya ukathibitishwa na wakili lamwai, kwani kila mtoto alikuwa na Baba yake kwenye zile picha. Yaani waziri alizaa na wanamume wanne tofauti. Huu ni utundu wa Dr lamwai.
Dr lamwai aliwahi Kusimamia kesi maarufu ya kupinga ushindi wa
ubunge jimbo la temeke mwaka
1996 Ambapo alishinda na kumng'oa kitini mh
Ramadhan kihiyo kwa tuhuma za kudanganya elimu yake.
Dr lamwai alikuwa kivutio kikubwa kwa vijana enzi za
miaka ya 90. Inasemekana watu walilala kwenye stesheni za treni kumsubili lamwai.
Lamwai alikuwa mbunge wa kwanza wa chama cha upinzani
NCCR-mageuzi katika jimbo la ubungo, aliitumia Taaluma ya sheria kushinikiza mambo nyeti na muhimu Bungeni.
Baada ya kuitesa serikali kwa muda mrefu, kisasi kikamfikia. Dr lamwai
alifukuzwa kazi pale Udsm alipokuwa akifundisha
sheria, akafanyiwa figisu
akapoteza ubunge, akaporwa
leseni ya uwakili, Mali zake
zikataifishwa. akabaki yeye na nguo zake tu. Akaishi kwa dhiki muda mrefu hadi alipoamua kujiunga na chama tawala-CCM ndipo akarudishiwa leseni ya uwakili na mali zake.
Dr lamwai ametoa vipanga wa sheria nchini. Mfano mzuri ni wakili Msomi
John Malya. Hiki kichwa kiliandaliwa na Dr lamwai pale chuo kikuu Cha
Tumaini - dar es salaam.
Dr lamwai alifariki mwaka 2020 kwa maradhi.