Mjue Jini Mahaba: Fahamu mengi kuhusu jini mahaba

Wewe huna hoja tena heri ukae kimya tu!
 
Wewe huna hoja tena heri ukae kimya tu!


Wewe ndiyo huna hoja, kwani unanipinga halafu unashindwa kutoa hoja mbadala zinazokuunga mkono katika kile unachoamini,, umebaki tu kupiga kelele.😜😜.

Mungu akikupa ufahamu wa Qur'an ni raha sana.


Ewe Rakims, fanya swala ya Istikhara au Hajja ili Allah akupe heri ya kujua maana za aya za kitabu chake Qur'an.
 
Good.iyo elimu ya kuwaona ina itwaje? Na je ukimuona akajua umemuona!
 
Sasa ni kwambie hiyo gaibu imefichwa na wanadamu wenzako sio mungu psychic abilities to compress human to the maximum is a big secret for humanity. Most important thing is an "EYE"
 
Sikuwaumba wanadamu na majini ila waniabudu?
wewe unaelewa vipi hii aya?
 
Mkuu kama wewe ni muislam basi unatakiwa urudi darasani ukasome vema uislamu wako kwa maana umepotoka kuamini kuwa maelezo ya Qur.an kuhusu majini ni wageni na kama umesali istikhara ndio ukaambiwa hivyo basi wewe umemzidi hata mtume kwa maana yeye mwenyewe kwenye hadithi yake kuhusu majini anasema:
Allah kaumba aina tofauti za majini. Miongoni mwao wapo wale wanaoweza kujibadili katika maumbile tofauti kama mbwa na nyoka; na baadhi yao hupaa kama upepo na wengine wanaweza kusafiri na kupumzika.
Abu Tha`labah al-Khushni pia alisema kwamba Mtume (swala llahu aleyhi wasalam) alisema:
:“Majini wapo wa aina tatu: Aina moja wapo ni ya upepo wanaweza kupaa kama upepo; aina nyingine huonekana kama mbwa au nyoka; na aina nyingine ni wale ambao hupumzika na kuendelea na safari zao.”(Ilipokelewa na At-Tahawi katika Mushkil Al-’Athar)

Sasa kama mkuu umeoteshwa hivyo huna tofauti na manabii wa uongo waliopo hivi sasa

Rakims
 
Good.iyo elimu ya kuwaona ina itwaje? Na je ukimuona akajua umemuona!
Kuna elimu nyingi za kuwaona lakini zote kati ya hizo zipo zinazoishia katika kushukuru au kukufuru itategemea na uliyojifunza au kufundishwa aina ya kwanza na ambayo wengi hutumia ni Mandal hii unaweza kutumia kwa kioo au macho ya kawaida lakini aina zingine si salama na pia ikiwa una imani thabiti na kinga ya mwenyezi Mungu wakikuona hawawezi kukufanya chochote sema ikiwa unawaita na huna uhakika unachofanya basi ni sawa na kumuita mwanajeshi au jambazi kwa ghadhabu na vishindo halafu akija unacheka cheka. atakacho kufanya mtajuana nyinyi wawili,

Rakims
 
Sasa ni kwambie hiyo gaibu imefichwa na wanadamu wenzako sio mungu psychic abilities to compress human to the maximum is a big secret for humanity. Most important thing is an "EYE"
how can a young man like him know this kind of stuff mkuu?
 
Umehama tena kutoka guest kwenda foreigners/strangers?

unaizungumzia vipi Surat Asabaa aya ya 15

"Na Tulipomkidhia kifo chake
(Suleimani) hakuna kilichowabainishia
kwamba yeye amekwisha kufa
isipokuwa mnyoo wa ardhini ambaye
alikula fimbo yake (Suleimani). Basi
alipoanguka wale majini walitambua
waziwazi kwamba kama wangaliyajua
yasiyoonekana, wasingalibakia katika
hali ya mateso ya kufedhehesha"

Sasa wewe unang'ang'ania uongo wako ili hapo ubadirishe mada baina yangu na wewe rejea kwenye mada yako ulivyoileta hapa:

Ulisema huo ni uongo mtupu na hakuna viumbe wa aina hiyo na kanusho lako ni kuwa hakuna majini na hapa sikuambii kuwa Qur.an ni kitabu cha majini au ni ngano za majini hapana isipokuwa nakuelimisha kuhusu usilofahamu kuhusu majini na usifanye watu wanielewe kuwa natetea mada za majini kwa msaada wa kitabu kitukufu hapana!

Rakims
 
REJEA PIA DAI LAKO HILI KUHUSU MAJINI UJUE NAZUNGUMZA NINI!?

Ndio maana nakwambia huna hoja wewe kaa kimya umeshashindwa huna la kusema zaidi ya uzushi tu na uongo na kawaida ya muongo huona wengine ni waongo pia usisahau kichaa huhisi anaakili kuliko watu wenye timamu lau kama angejua angebadilika!?
wacha kuzalisha mada ndani ya mada

Rakims
 
“Malaika waliumbwa kutokana na mwanga na MAJINI waliumbwa kutokana na moto”
(Saheeh Muslim)
Kitabu wanachokubaliana nacho waislamu wote
Hivi unaumwa mkuu au hujasoma? basi soma. au kama hujui kaa kimya

Kipande hiki kinaelezea mambo mengi sana kuhusu majini sasa kama hawa majini ni bacteria mwanasayansi yupi kwenu alithibitisha maumbile yao kwa moto. Kwa sababu wao waliumbwa kwa moto, na mahusiano yao na wanadamu yamejengwa juu ya hili. kama wanadamu, wao pia wanatakiwa kumuabudu Mungu na kufuata dini ya haki na kuabudu kama wanadamu na malaika. wao jambo waliloumbiwa ni sawa na sisi kama vile mwenyezi Mungu aliposema,.

“Sikuwaumba wanadamu na majini ila waniabudu.” (Quran 51:56)

Majini pia wanaweza kuwa waislamu au sio waislamu vyovyote vile kwa asili yao ya moto wengi wao pia sio waislamu kwa nafasi kubwa sana Wote hawa majini wasiokuwa na dini wengi wao hufuata yale waliopelekewa na Jini maarufu zaidi kuliko wote ambaye ni shetani, sasa kwa hakika hawa majini wote wanaopinga na wasiokuwa na dini huitwa mashetani, Majini pia wengi hubadili na kuingia katika dini ya Uislamu kwa utajo au kauli nzito zenye ukumbusho mkubwa ambayo ni maneno au aya za Qur.an ambazo ni ukumbusho kwa wenye akili na wenye kujua. na pia hawajabadili dini katika kipindi hiki tu isipokuwa hata zama za Mtume Mtukufu wa Uislamu walibadiri na kuingia katika uislamu kwa kusikiliza Qur.an ya Ajabu yenye kusema kweli na iliyokamilika na Mwenyezi mungu akamuamuru mtu kusimulia hiki kisa. Cha majini

Na hii ndio maana ya hiyo aya unayong'ang'ania kuwa majini ni watu wakuu au funza na bacteria zako wewe na walimu wako:

“Sema (Ewe’ Muhammad): Imefunuliwa kwangu ya kuwa kundi la majini lilisikika kwa kusikiliza na kusema; Tumesikiliza Qur.an ya ajabu Kabisa. Ambayo ni muongozo wenye kuongoza kwenye haki na sisi tumeiamini na hatumshirikishi Mola wetu na chochote’.”(Quran 72:1-2)

katika mategemeo ya ulimwengu wanaoishi pia majini ni viumbe wenye ufanano kabisa na sisi: kwa maana wao wanakula na kunywa wanaoa na kuzaa pia wanakufa. Maisha na hadithi yao pia itaisha kama vile yetu na watahukumiwa siku ya malipo kama sisi na pia wataingia motoni na peponi kama sisi.
Mwenyezi Mungu Atuepushe na moto.
Kama bado hadi hapa hujajua majini wapo basi mwenyezi Mungu atakuongoza kupata elimu au kujua pindi atakapo hitaji na sisi ni wenye kukumbusha na sio wenye kuongozana kama Mwenyezi Mungu kakubadilishia wewe maana ya majini tunayoifahamu sisi basi ikifika wakati wetu na sisi atatuongoza kama vile anavyowaongoa waliopotea na kuwaweka kwenye mstari au njia sahihi! Allahuma Amin. sina cha kubishana na wewe tena kuhusu uwepo au kutokuwepo kwa majini.

Rakims
 



Sasa tufanye jambo moja, ewe rafiki yangu Rakims.

Tufafanulie hayo majini katika hiyo aya, yaani toa maelezo ili mtu anayetaka kujua hayo majini katika hiyo aya ajue ni kitu gani !!----- kutokana na jibu lako ndipo nitajua msimamo wako.

Mimi niliisha fafanua katika post moja aina 3 za majini waliotajwa katika Qur'an pamoja na aina 1 ya "majini"/ maruhani wanaowashika akina mama, yote hayo nilitoa ufafanuzi wake.

Ufafanuzi wangu ni kinyume na itikadi potofu inayoshikiliwa na watu wengi hususan Waislamu kwamba majini ni viumbe fulani wasioonekana na wanaweza kufugwa kama mbwa na kutumwa kufanya kazi fulani, pia eti, kuna watu wanaweza kuwatengeneza majini na katika hao majinni wapo jini makata, subiani, kishkish, jini mahaba nk, na pia wanasema hayo majini yanayowashika hasa kina mama hutokea nje na kumuingia mwanamke kichwani (anapokuwa kapandisha). Kuna dhana ya uongo inayoaminiwa juu ya "majini".

Narudia tena, kwamba kuna majini wa aina 3 waliotajwa katika Qur'an, na mimi sipingi majinni waliotajwa na Allah ndani ya Qur'an, ninachopinga ni dhana za uongo zinazosemwa kuhusu "majini", mfano eti kuna jinni mahaba nk,😛😛.


Mtu akichukua ufafanuzi huo wa uongo kuhusu majini na akaenda kusoma Qur'an na akakuta majini wamezungumzwa humo, moja kwa moja anapata hisia kwamba majini hao ndio wale wanaitumwa kudhuru watu au ndio hao jini mahaba wanaoingilia watu usiku au ndio hao popobawa nk, sasa hatuwezi kuruhusu Qur'an iaminike kuwa ni kitabu cha "fables and tales" za majini popobawa, watu wengine wataogopa kuishika Qur'an kwa sababu ya woga wa " kukumbwa na majini mliowaaminisha kwa uongo wenu".
 
Quote number 195,
kipengele cha kwanza hadi mwisho.

Rakims
 



Read posts No, 111 na 132. Ili ujue nilichosema.

Malaika kuumbwa kwa nuru na majini kuumbwa kwa moto, hii haina tofauti na mtu kuumbwa kwa haraka,--- خلق الاسن من عجل---

(21:37) Mtu ameumbwa kwa haraka--


👆🏻Unaelewa nini kuhusu hiyo aya??
 
Quote number 195,
kipengele cha mwisho.

Rakims
 
Quote number 195,
kipengele cha mwisho.

Rakims


(1)"Kila kitu chenye uhai kimeumbwa kutokana na maji"

(2) "Na tumemuumba mtu kutokana na udongo utoao sauti" ---- Qur'an hiyo.

👆🏻Na hapo umeelewa nini??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…