Mokaze
JF-Expert Member
- Aug 3, 2018
- 14,370
- 14,929
Kuna comment hapo juu umesema hakuna viumbe kama hivyo
Halafu hapana unaelezea kuhusu viumbo hivyo
Nimeshindwa kukuelewa
Ni hivi; kimsingi Jinn ni viumbe au vitu vyenye sifa ya kuto kuonekana kwa macho ya kawaida, kwahiyo jinn anaweza kuwa ni mtu, mdudu, hali fulani isiyoonekana inayompata mtu nk.
Mfano, Bakteria wote na virusi wanaitwa majinni kwa sababu hawaonekani kwa macho ya kawaida hadi utumie microscope.
Mtu mgeni anaweza kuitwa jinn kwasababu yeye anaonekana tu kipindi kile yupo na mwenyeji wake na baadaye anaondoka, hapa anaitwa jinn ki-sifa.
Watu wakubwa kama viongozi, matajiri, watu mashuhuri kama wanasayansi pia wanaitwa majinni kwasababu ni muhali kuwakuta kuchangamana kirahisi na watu wa kawaida hivyo ni shida kuonekana mara kwa mara nao wanakuwa na sifa ya kuitwa majinn.
Ule ugonjwa unaowashika hususan kina mama na watu huuita "majinn", unaitwa hivyo kwasababu inaonekana ni kama vile kuna kiumbe fulani kimemuingia huyo mama na ndicho kinachomfanya afanye mambo ayafanyayo, hapa ndipo mimi ninakataa kwamba hakuna kiumbe kama hicho kutoka nje kinachomuingia huyo mama, kilichopo ni kwamba huyo mama kashikwa na ugonjwa unaoitwa Hysteria na jinsi unavyoathiri unaweza kusema, KI -SIFA, kwamba ugonjwa huo ni "jinn", kwasababu huo ugonjwa hauonekani lakini athari yake inaonekana kwa mgonjwa, maana yangu ndiyo hiyo.
Hakuna jinni kiumbe wa ajabu aghalabu anayefanana na mtu/watu, kama jinsi watu wengi wanavyoamini kimakosa.lakini wapo majinni viumbe niliowataja hapo juu na wao wanaitwa majini kutokana na sifa waliyonayo ya "kutokuonekana" (concealment) kirahisi kama jinsi nilivyoeleza.
Utaona watu wamewapa majina eti, jinni mahaba, Subiani, Jinni makata nk, nasema hakuna viumbe hao. Tafsiri ya ufupi ya jinn ni hiyo niliyoiweka hapo juu.
Nadhani utakuwa umenielewa.