Mjue Jini Mahaba: Fahamu mengi kuhusu jini mahaba

Very good with imagination mkuu!,
Elewa jambo moja ya kuwa kwa asilimia kubwa sana wewe unaweza kuwa sio Muislamu lakini pia unaweza kuwa sio mkristo unless hizi dini wewe huzisoma kwa kudokoa yale unayoona yanakufaa na yasiokufaa unaachana nayo my friend in this you have failed sita ingia sana kwenye upande wa wakristo nitakupa maana hapa hapa ambapo wewe umeona kuwa umeweza then mwisho wa siku i think you are Atheist.

Wajue majini kwanza kutoka katika Qur. an na hadithi ya mtume unavyodiliki hujui kuhusu maana hasa ya majini,

JE, hazijawahi kukupitia hizi aya masikioni mwako? Na je, hujawahi kuzisoma hata kwa macho?
Kama jibu ni ndio basi zisome leo na utapata faida kubwa In shaa Allah

USHAHIDI WA QUR.AN

Surat Rahman Aya 74:

لَمْ يَطْمِثْهُنَّ إِنْسٌ قَبْلَهُمْ وَلَا جَانٌّ
Hajawagusa mtu wala jini kabla yao.

Hao ni wanawake wa peponi wanaotajwa katika sura hiyo Unaelewa jini ni nini hapo?

Sura Naml Aya 39

قَالَ عِفْرِيتٌ مِنَ الْجِنِّ أَنَا آتِيكَ بِهِ قَبْلَ أَنْ تَقُومَ مِنْ مَقَامِكَ ۖ وَإِنِّي عَلَيْهِ لَقَوِيٌّ أَمِينٌ

Akasema Ifrit katika majini mimi nitakuletea kabla hujainuka pahala pako na mimi kwa hakika nina nguvu na muaminifu.

Hapo kilikuwa kisa cha nabii Suleiman mfalme wa majini watu na vyote alivyoruhusiwa na Allah. sasa huyo Jinn kwa maana yako anaweza kubeba hicho kiti cha BalKis Malkia wa Sheba?

Sura An'am aya 100

وَجَعَلُوا لِلَّهِ شُرَكَاءَ الْجِنَّ وَخَلَقَهُمْ ۖ وَخَرَقُوا لَهُ بَنِينَ وَبَنَاتٍ بِغَيْرِ عِلْمٍ ۚ سُبْحَانَهُ وَتَعَالَىٰ عَمَّا يَصِفُونَ

Bado wamemfanyia mwenyezi Mungu majini kuwa washirika wake, na hali yeye ndiye aliye waumba na wakamzulia bila ujuzi wowote kuwa anawana wa kiume na wakike subhanallah ametakasika na ametukuka juu ya hayo wanayombambikiza nayo.

Sura An'am 130 na al al raaf 38 na aya na sura zingine pia











Mkuu kama na hizi hazijakutosha nikuangalizie na Hadithi au nikupekulie na kwenye biblia?

Rakims
 
Yupi kati bin adam na jin anakiwa powerfull zaid ya mwenzake endapo individual akifika kwenye maximum spiritual and quantum mind set?

Pia naomba maelezo kuhusu pazia linalotufanya tusiwaonee? Ila nadhan wao wanatuona sio
Nikipata muda mkuu nitakupa jibu nikiwa nimetulia maana nimehama kidogo kifikira
 
Nimejikuta nacheka!
 
Jazaka llahu kheir
 


Mkuu, rudia kusoma kwa makini hiyo habari yote niliyoandika na uwe huru (neutral), yaani unaposoma achana na preconceived ideas, hapo ndipo utaelewa kile nilichoandika.
 



Mkuu, inaonekana wewe unataka Qur'an watu tuisome kama jinsi watoto wanavyosoma "fables"(ngano)., katika kusoma Qur'an ni lazima Tadabbur itumike.

Nilikuwa najaribu kupitia nukuu za kamusi (Lane na Aqrab, the arabic english lexicons) chini ya neno jinn (جن), ninanukuu hapa chini;

"" جن (jinn) is derived from جن (janna) which means, it veiled, concealed, covered or protected himor it. جن (jinn) means such beings as remain aloof from the people concealing themselves; strangers; the main or chief part or body of mankind, etc.""

Jinn inaweza kuwa;
(1) wadudu wadogo wasioweza kuonekana kwa macho bali kwa vyombo kama microscope nk, Baktetia, Amoeba, paramecium, virusi nk, vyote vimo katika kundi hilo, na wanakula takataka na uchafu mbalimbali ndiyo maana mtukufu mtume (saw) aliwakataza waarabu kuchambia mifupa na kinyesi kikavu cha ngamia ili wasidhurike na akawaambia ni chakula cha majini. Na hapa wale majinn ambao Qur'an inawasema waliumbwa kwa mwale wa moto wanaingia hapa nao ni Bakteria Eukaryotes na pykaryotes.

(2) Wageni nao wanaweza kutwa majini kisifa kwa sababu wageni nao huonekana pale anapokuja kutembelea wenyeji tu. (Strangers), na wale majini wanaotajwa katika Surah Jinn walikuwa ni wageni wa kiyahudi, hawakuwa Waarabu.

(3) Watu mashuhuri, kama viongozi na wataalamu, wanasayansi maarufu (genious/ distortion of the arabic word jinn) na wao wanaitwa majinn ki sifa--- hapa ndipo wapo Ifrit wa Nabii Suleiman (as) nk. Pia watu wakubwa kama maraisi nk, (such beings as remain aloof from the people---) na Ibilis yumo katika kundi hili.

(4) kundi la mwisho ni majinn wa dhahania (abstract), hawa ndiyo wanaitwa mapepo, maruhani (روحهن), wanaowakumba hasa kina mama, inadhaniwa na watu kimakosa kwamba hao majinn ni viumbe hai aghlabu mithili ya umbo la watu au mtu na linamuingia mwanamke kichwani na kuweka makazi yake humo na baadaye linafanya mambo linalotaka kupitia huyo mwanamke. Huo ni Uongo mkubwa kusema kwamba kuna kiumbe-jinn mithili ya mtu ndiye huingia kichwani kwa mtu.

Mapepo kitaalamu ni ugonjwa wa akili unaojulikana kama "Hysteria", ni ugonjwa unaosababishwa na hali za kimwili na hali za kimazingira yanayomuhusu mgonjwa kwa wakati huo, mgonjwa anaweza kuweweseka na kuongea lugha za ajabu au anaweza katika usingizi akaota mambo ya ajabu nk,------ sasa kwanini watu hali hiyo wakaihusisha na majinn??, sababu ni kwamba mgonjwa hufanya mambo bila hiyari yake na inaonekana kama kwamba ipo nguvu nyingine inayotenda kazi ndani ya mgonjwa na nguvu hiyo (wanaamini) ni kutokana na kiumbe mwingine aliyeingia kichwani mwa mgonjwa🤣🤣!!, -- sijui alipitia puani, sikioni, machoni au??, hakuna majibu.

Majinn niliowataja katika kundi la 2 na 3, hawa ni binadamu na ndio hawa Allah amewataja katika ile aya alipotuusia juu ya wajibu wetu katika kumuabudu aliposema; " Na sikuwaumba majinn na watu isipokuwa waniabudu"---- majini waliotajwa hapa ni watu mashuhuri, hao majini waliotajwa hapo kwenye hiyo aya ni watu maalum (mashuhuri) kwa sababu Qur'an inajisema yenyewe kwamba ni muongozo kwa "watu" pekee pia Allah katika hiyo Qur'an anawahusia "watu" pekee wamuabudu, ndiyo maana nikasema hao majini waliotajwa katika hiyo aya ni watu maalumu.

Kinyume na mtazamo huo Qur'an itakuwa ni kitabu cha fables and tales, Mungu apishe mbali.
 
Sawa broo ila swali langu umeliona
 
Unacheka mkuu me nimeuliza sisi wengine hatuna tunachojuwa . Kumbe Backeria wanafanya uote unasex


Hiyo ipo katika kundi namba 4 la majinn, kuota unasex ni matatizo ya kisaikolojia yanayomkumba mtu husika, kwakuwa tatizo hilo ni "involuntary action" (haliko chini ya ridhaa au maamuzi ya muhusika mwenyewe) hivyo inadhaniwa KIMAKOSA kwamba kuna kiumbe fulani aitwaye Jinn kutoka nje ndiye anayesababisha hali hiyo ya kusex kwa muhusika, mimi nakataa katakata hakuna kitu hicho bali ni uzushi watu wanazua kwa makusudi au kwa kutokujua kiini cha jambo hilo.

Tukio hilo la kusex linaweza kuitwa kwamba limesababishwa na jinn KI-SIFA tu na wala siyo kidhahiri kama watu wanavyoaminishwa, ki-sifa kwasababu ugonjwa huo wa kisaikolojia unatenda jambo hilo ndani ya muhusika bila ya yeye mwenyewe kutaka kwa maana hiyo tunaweza kusema huo ugonjwa ni nguvu iliyojificha ndani ya muhusika, na huko kujificha ndani ya muhusika (Concealment) ndiyo sifa ya "UJINN" (janna)--- hivyo inaposemwa fulani kashikwa na jinn mahaba ni katika muktadha huo tu na si vinginevyo.

Mimi ninajaribu kuweka wazi mambo ambayo yamekuwa hayajukikani mantiki yake na hivyo watu wanapotosha na kuwapotosha wengine kwa mambo ambayo yapo wazi, mbaya zaidi zinachukuliwa aya za Qur'an na kupotoshwa hatimaye Qur'an inaonekana ni kitabu kilichojaa "fables" za majini (mfano hadithi za sungura na fisi). Audhubillahi min dhalika.
 
Uliubwa unajua kila kitu sio kilakitu lazima subconscious ikushirikishe kaakili kako. Mbona ukiota sua za watu ambao huwajui huuliz
 
Ndugu nipo hapa kwaajiri ya kujifunza na sio kupinga Mada au kukubali Mada
Uliubwa unajua kila kitu sio kilakitu lazima subconscious ikushirikishe kaakili kako. Mbona ukiota sua za watu ambao huwajui huuliz
 
Samahani, mkuu naomba unikumbushe hilo swali.
BRO nimekuelewa Sana ila naomba nijue kweli nakubaliana na wewe kuwa ni saikolojia inakufanya uote sasa na wale wanaotumiwa na waganga katika kujuwa tatizo au kujuwa solution ya tatizo pia ni saikolojia inatumika au ni vipi utakuta anapandisha alafu anasema je nini hcho kinachoeleza mambo yote au ndio ugongwa wa akili??
 


Mkuu, ingawa hujafafanua swali lako ila nitakujibu kulingana na uzoefu wangu kuhusu mambo hayo; unauliza juu ya wale waganga wanaopandisha hayo yanayoitwa majinni na wakishapandisha majinni hayo majinni yanaeleza shida za mgonjwa kabla hata mgonjwa hajaeleza shida zake na inakuwa "kweli".


Mkuu, mimi ni Muislamu na ninaiamini Qur'ani tukufu yote kwamba ni kitabu cha Mungu neno kwa neno, sasa tumsikilize Mungu anasemaje;

قل لا يعلم من فى السموات و الارض الغيب إلا الله و مايشحرون أيان يبعثون

Yaani:- Sema (ewe Muhammad) hakuna yeyote mbinguni na ardhini anayejua ghaibu ila Allah na hawajui watafufuliwa lini (27:65).

Sehemu nyingine Allah anasema; A'limul ghaibi falaa yudhhiru a'laa ghaibihi ahadan illa mani rtadha min rrasuulin. Yaani; (Yeye) ni mwenye elimu ya ghaibu basi hamdhihirishii yeyote (ghaibu) ila kwa mitume aliowaridhia. (72:26).

Ghaibu ni elimu ya mambo ya siri, elimu hiyo anayo Mungu pekee na anapoamua kuitoa basi humpa yule aliyemridhia katika mitume wake, hivyo tunaona ni mitume tu ndiyo watu wanaoweza kueleza mambo ya ghaibu baada ya kupashwa habari hizo za ghaibu na Mungu mwenyewe.

Kwa minajili hiyo anapotokea mtu/mganga ambaye sio mtume na akapandisha "majinni" na kueleza mambo ya siri (ghaibu) ya mgonjwa basi huyo atakuwa anaongea vitu vya uongo, na hao ndio wale waganga wapiga ramli chonganishi kwa lengo la kujipatia kipato na ili aaminike mbele ya wateja hujifanya kapandisha hayo yanayoitwa "majinni" kusudi wateja wake waamini kuwa anayesema huo utabiri ni majinni na sio yeye.

Duniani kuna elimu mbalimbali pamoja na elimu za kiakili/kifikra (pysche), kuna watu wanaweza kuangalia macho yako kwa muda tu na kujua kwa muda huo kile unachofikiri, inakuwa ni kama Radio na transmitter (Radio station), transmitter inatoa matangazo kwa njia ya mawimbi na radio inakamata hayo mawimbi, ni katika mfano huo kuna watu wanaweza kumuangalia ntu machoni na macho yao yana "pair" na macho ya muhusika hivyo wanajua kile akili yako inachofikiria kwa wakati huo na hiyo ni elimu waliyonayo watu fulani, ni kipaji kama vipaji vingine, sasa mtu mwenye kipaji cha aina hiyo anaweza kutumia hicho kipaji na akala fedha za watu kwani watu wanapoambiwa shida zao kabla hawajazisema hupatwa na mshangao na imani kwa huyo "mganga" kumbe maskini, hawajui mtu huyo anayo elimu ya kusoma macho ya watu, na hiyo siyo ramli.

Ninachotaka kusema ni kwamba elimu ya ghaibu anayo mungu pekee na mitume ambapo Mungu huwapa hiyo elimu. Kama mtu yeyote atatokea na kusema anaweza kutenda elimu ghaibu bila kutumia elimu ya "pysche" au kusoma mazingira na nyakati basi huyo atakuwa ni Muongo na anataka kula pesa za watu bure.
 
Asante kiongozi ndani ya familia yetu yupo mtu ambaye anaayo mambo ila sio mganga na ila anauwezo wa kuongea lugha tofauti tofauti akipandisha hadi muda mwengine hadi sauti za kike na anasema tatizo liliopo na niukweli na anasema jinsi ya kulimaliza hapo ndipo nakosa jibu sahihi.
Me nadhani jinn haonekani ila jinn pia inaweza kuwa ni roho inayoishi kwa kuzingatia maelezo yangu hapo juu
 



Mkuu, kuongea lugha mbalimbali huyo nduguyo anayo Hysteria na hali hiyo inaitwa (Ravings).

Ipo hivi; ubongo wa mtu ni kama memory card-- unahifadhi kila jambo inalolisikia katika mtiririko wa "the first in the first stored", kumbuka kwamba watu huwa tunafariki ilhali sehemu kubwa sana ya memory ya ubongo wetu huwa haijatumika, sasa inapotokea mtu wakati fulani alisikia lugha fulani, (na hilo ni jambo la kawaida mtu katika maisha anaweza kusikia watu wakiongea lugha tofauti tofauti), na lugha zote hizo huifadhiwa na ubongo katika mtiririko (sequence) licha ya kwamba lugha hizo huyo mtu hazijui, mfano anaweza kusikia, kisukuma, kiha, kiingereza, kirusi, nk, lugha ambazo hazijui kabisa na hasa kama alizisikia katika umri mdogo pale ambapo akili ya mtoto inapokuwa ni rahisi kujifunza lugha mbalimbali, sasa anaposhikwa (anapopandisha) hiyo Hysteria (majinn) akili yake wakati huo unajifungua ule mlango wa lugha zilizohifadhika (retrieval ) na anaanza kuongea hizo lugha na watu huanza kushangaa,🤣🤣🤣.


Pia Kumbuka kwamba mtoto huanza kujifunza misingi ya lugha kupitia kwa mama yake tangu akiwa tumboni.

Hivyo mkuu, hayo anayopandisha nduguyo si chochote bali ni Hysteria, na ugonjwa huo hutokea kwa styles tofauti tofauti kulingana na ubongo wa mtu, mwingine akishikwa haongei lugha yoyote ila ni kupiga kelele na kujirusha hovyo na asipodhibitiwa anaweza kupata mpasuko katika fuvu (concurtion).

Na ugonjwa huo huwapata sana akina mama 99%, 🤣🤣, kwanini isiwe kwa akina baba??--, kama jinn ni kiumbe anayetokea nje na kumuingia mtu kwanini wanawaogopa akina baba??🤣
 
Kuna comment hapo juu umesema hakuna viumbe kama hivyo
Halafu hapana unaelezea kuhusu viumbo hivyo
Nimeshindwa kukuelewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…