Rakims
JF-Expert Member
- Jun 4, 2014
- 5,002
- 4,571
- Thread starter
- #41
Swali zuri,Naomba unieleweshe hili ndugu.Kwa mjibu wa utaratibu wa kimajini na tiba zake na hata kumuita jini inaonyesha j mosi ni siku mbaya na hata huo mda unaoonyesha saa sita usiku mda huo huo mtawala anakuwa ni mtu wa damu je inakuwaje uite jini mda huo.lingine kwa mjibu wa mambo ya majini chumba unachomuitia jini kinakuwa hakina kitu chochote tofauti na mikeka au jamvi la kukalia ww sasa hiko kitanda cha chuma inakuwaje!
Kwa mujibu wa utaratibu wa kimajini na tiba zake na hata kumuita jini inaonyesha j mosi ni siku mbaya hili si kweli na wala si sahihi.
Kipengele kingine cha swali lako ni kuwa mtawala wa saa hiyo anakuwa ni mtu wa damu si kweli.
Kipengele kingine cha mwisho ni kuwa chumba kinatakiwa kiwe tupu hii ni kwa baadhi ya majini tofauti na huyu mahaba. na sio wote waliobaki,
Kiujumla swali lako naweza kukujibu hivi, siku ya Jumamosi ni siku kielimu ya juu zaidi kuliko hiyo uliyoishia ni Siku ya Zohali (Saturn) Siku hii hutawala sana jini aina ya MAIMUN, ambaye ni mfalme miongoni mwa majini wasiokuwa na sheria ya kuolewa au kuoa hasa kwa waliokufuru, Usiku wa siku hiyo ya Jumamosi kielimu huitwa usiku wa Atwarid (Jumatano) sasa kimahesabu ya juu kabisa saa hiyo inakuwa ni saa ya Shamsi (Jua au Jumapili) ambayo hudeal zaidi na commandment ya Shamhurash jini wa Jumapili, sasa hawa mahaba mfalme wao huwa ni Maimun au wabongo humuita
MAIMUNA, na huyu huwa yupo chini ya SHAMHURAASH ambaye ni mfalme wa Jumapili. mkuu hadi hapo nahisi utakuwa unajua nazungumzia nini nikiendelea naweza kukuvuruga tu, yule anaekwambia jumamosi ni siku mbaya na saa hiyo ni ya damu elimu yake bado ni Shallow kwa maana anategemea nguvu ya MARUHANI/Majini katika shughuli zake wala hataki kuhangaika na kuwashurutisha ndio hawa huwapa sadaka majini bila kujua kampa sadaka jini wa namna gani,
Rakims