Taifa limejaa wajinga hili ,sina hakika kama na mataifa mengine wapo wajinga kwakiwango hiki cha Tanzania
Fanya utafiti kwanza ndo useme usemavyo. Kwa taarifa yako mataifa mengi duniani watu wamekengeuka, wanatafuta kitu cha haraka kitakachodhihirisha nguvu, na utatuzi wa matatizo yao.
Si Tanzania tu hata Ulaya. Kumekuwa na imani New age, watu wanaabudu mizimu, wanaongea na wafu. Wanajali utabiri wa maisha yao. Kuna dini inampinga Yesu, ila wao wanamwabudu Mungu, wanasema Yesu aliomba nao wanauwezo wa kuomba wananguvu za kimungu. Hawaamini katika ubatizo.
Hivyo ukitaka kuwa mfuasi wao wanaondoa ubatizo uliokuwa nao. Wananguvu za kuuwa wanapotaka. Kiujumla inanguvu za kichawi na giza. Hawa ndo wazungu unao dhani wao si kama usemavyo.
Si hayo tu kuna imani za makanisa wao ukiingia kanisani ni kuimba na kudance, kunasiku ya kufanya mapenzi, watu wanaabudu uchi. Dunia hii kuna mambo ya ajabu si Tanzania tu.
Hivyo usiwaite wenzio wajinga, kila mtu anauhuru wa kuabudu anachoona kinamfaa. Yesu akuwahi waona watu waliompinga ni wabaya yeye alihubiri yale mahubiri na miujiza iligeuza mioyo ya watu. Kikubwa wanaohubiri wahubiri watu, ili wageuke na kufuata njia ambazo wao wanaona zinafaa, kuliko kutukana na kumsema vibaya Zumaridi au hao waumini wake.
Wachungaji wengi wamekuwa wakijilimbikizia mali, wao na familia zao. Waumini wengi wanashida, njaa. Cha kujiuliza ni nini kimemfanya huyu Zumaridi kupata wafuasi wengi kiasi hicho? Hatuna haja ya kutukana hakuleti ufumbuzi wa tatizo.
Kuna dini za shetani hapa Tanzania, kuna ushoga umejaa kibao, kunawaganga wanaishi na watu na hata kuleteleza mauaji. Hao wameshindwa kuwafuatilia. Huyu Zumaridi si mwamini na sifuati imani yake, lakini, tujiulize hao watu wote anaokaa nao kunawaliolalamika kufanyiwa mambo mabaya?
Nacho ona huyu yeye anapenda kutukuzwa, na anaushawishi mkubwa sana, kiasi amevuta watu wengi kuwa wafuasi wake. Wanasema anasaidia saana watu wenye shinda mabalimabali. Hawa viongozi tulio nao hata hawana haja ya kusaidia wananchi wenye shida.
Tanzania hii imejawa na mafisadi watu wanakula fedha ya serikali hawafanywi kitu. Mtu anaejitafutia sifa zake katika imani yake, huku akitunza na kulisha mamia ya watu nyumbani kwake, anaonekana mbaya. Anapachikwa kesi zisizo na miguu wala kichwa. Kisa wivu tu wa baadhi ya watu.
Ni kiongozi gani Tanzania hii ya leo ambapo kiongozi anaweza karibisha watu kuishi kwake na kuwalisha bila tatizo. Sana sana ni Enzi za Nyerere ambae nyumbani kwake hasa Butiama watu walijaa, ukifika unakula na waweza kukaa bila kusumbuliwa.
Pole Zumaridi umaarufu umekuponza. Kwa sababu kuna wengi kama wewe ambao wanafanya ufanyavyo wala hawafuatiliwi. Ila unauthubutu na kujiamini. Unaushawishi mkubwa. Pole hii ndo Tanzania.