Sadock Kabuko
JF-Expert Member
- Mar 26, 2013
- 1,166
- 1,075
huyo nyelele ni wa nchi gan tena?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Grade II in the house hahahahahhhh!
Msimchanganye Mwenyewe anataka histolia ya mwalimu nyelele! Nyie mnamlazimisha mumpe ya Mwalimu Nyerere.Naitaji kujua histolia ya mwalimu nyelele
ungeandika hivi:
Nahitaji kujua historia ya Mwalimu Nyerere
Umetoka kwenye kutafuta mke.sasa umehamia kwenye historia ya mwalimu nyerere.
Ha ha ha. Asante kunipa kicheko.Mwalimu nyelele ndio mimi hapa una bei gani? Hakuna histolia ya bulebule vp unaitaji.
Mshana,
Kalaydo ahsante.Sheikh Mohamed Said pole kwa usumbufu wa hawa wengine ila mimi nakupa shukrani zangu za dhati na pia nasubiri kupokea historia na mafunzo toka kwa wazee wetu wengi wengine.
[HASHTAG]#ShukranMohamedSaid[/HASHTAG]
Sent using Jamii Forums mobile app
Mshana,
Hii hapo chini si sawa:
Mwaka 1953
alichaguliwa kuwa raisi wa chama cha Tanganyika African
Association (TAA), chama ambacho alikisaidia kukijenga
alipokuwa mwanafunzi katika chuo kikuu cha Makerere.
Hebu soma hii kutoka kitabu cha Abdu Sykes:
''Uchaguzi baina ya aliyekuwa rais wa TAA, Abdulwahid na mwalimu wa shule asiyefahamika vyema pale mjini, Julius Nyerere, ulifanyika kwenye Ukumbi wa Arnatouglo tarehe 17 Aprili, 1953. Nje ya uongozi wa TAA ambao ulimpendekeza kugombea nafasi hiyo, Nyerere alikuwa mgeni kabisa kwa wote aliokuwa akiwaomba kura zao. Maisha ya Nyerere katika siasa yalianza hapo. Nyerere alikuwa mgeni na alikuwa hana historia ya kuongoza mapambano ya umma dhidi ya serikali ya kikoloni. Ukoo wa Sykes ulikuwa unatambulikana katika siasa za Dar es Salaam kwa takriban robo karne. Ukoo huu ndiyo ulioanzisha na kuongoza vyama vyote viwili, African Association na Al Jamiatul Islamiyya. Ukoo wa Abdulwahid, mtoto wa Kleist Sykes ulikuwa unafahamika kwa kuongoza mapambano dhidi ya serikali. Ushahidi wa haya ulikuwa unapatikana katika nyaraka kati ya ukoo huu na serikali ya kikoloni. Katika kipindi cha miaka zaidi ya ishirini, serikali kwa nyakati tofauti, kati ya mwaka 1929 hadi 1953 ilikuwa na barua za Kleist Sykes na za mwanaye Abdulwahid wakiwa viongozi wa African Association kuhusu madhila tofauti yaliyokuwa yakiwakabili wananchi.''
Nyerere angekuwa ameijenga TAA akiwa Makerere asingekuwa
mgeni katika uchaguzi uliomwingiza madarakani 1953.
Ukipenda kusoma habari hizi zaidi angalia:
Listowel, Judith, ''The Making of Tanganyika,'' Chatto and Windus, London, 1965.
Ukipenda kusoma historia iliyokamilika ya Baba ya Taifa Mwalimu Nyerere na jinsi
alivyoingia katika siasa alipofika Dar es Salaam, 1952 soma kitabu cha Abdul Sykes.
![]()