Mjue Peter Mollel Gumbo aka Pierre Konki Mzee wa Liquid ambaye wengi hawafahamu vizuri

Mjue Peter Mollel Gumbo aka Pierre Konki Mzee wa Liquid ambaye wengi hawafahamu vizuri

Sijawahi kuwa shabiki Wa mhe. Makonda lakini kuponda tabia ya ovyo kama ulevi namsupport. Hivi tushabikie ulevi halafu tutajenga taifa la aina gani ? Congo walishabikia muziki angalia Leo taifa lao likoje. Taifa linajengwa na watu sober wanaotulia na kukuna ubongo , sio kushangilia na kushabikia tabia za ovyo kama ulevi na mambo megine ya kipuuzi . Makonda nakusifu kwa hill ingawa wapuuzi watakushambulia lakini umetimiza wajibu Wa kukemea upuuzi .Konki mlevi 42 years hana mke wala Mtoto , ndio awe shujaa Wa taifa hili ? Role model Wa vijana wetu. ? Tusipotoke kama taifa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Makonda anaweza kuwa sahihi

Lakini katika muktadha ambao si sahihi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katika ubora wake
IMG_20190407_123849.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Heshima ya chuo inaaribiwa na waliosoma hapo kutojua kuwa wahasibu kutumia neno weakness katika kazi zao ni utaratibu sahihi ambao upo katika IFRS ambao wasomi wa hapo hawajui...Mngepata bahati ya kusoma UNISA au Stellenbosch university ukutane na watu genius mpaka kazini sijui ungesemaje hapo kimezalisha matakataka kibao tuu yanaangamiza Taifa...
hayo matakataka ndio yanasababisha utype

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Konki Liquid. Pierre. Mama nakufa. Chii. Ni utambulisho wa mwanamume aliyeishika mitandao ya kijamii wakati huu.


Huyu ni Peter Mollel aliyejizolea umaarufu baada ya video iliyomuonyesha akisema “mama nakufa” kuzagaa mitandaoni mwishoni mwa mwaka jana.
Leo Machi 13, 2019 ametembelea ofisi za kampuni ya Mwananchi na kufunguka mengi kuhusu maisha, umaarufu na mipango yake ya baadaye.



Pamoja na wengi kumfahamu kwa video hizo zinazomuonyesha akiwa kwenye vilabu vya usiku na baa, Pierre anasema yeye si mlevi kama wengi wanavyomtambua.


“Kuna mtu aliandika katika mitandao ya kijamii akisema mimi ni mlevi wa taifa, hilo halina ukweli wowote kwa kuwa nina shughuli zangu na huwa nakunywa baada ya mambo mengine, angeniita mnywaji angepatia,” amesema Pierre huku akitabasamu.



“Mimi kama hamjui nina ofisi ya kuuza samani pale Keko na sofa moja nauza kuanzia Sh3 milioni, meza Sh1.2 milioni . Umaarufu pia umeniongezea chanzo kingine cha mapato. Katika shoo moja nalipwa hadi Sh3 milioni kwa usiku mmoja,” amesema Pierre.



Alipoulizwa kuhusu familia, Pierre mwenye umri wa miaka 42 amesema hajaoa na hana mtoto na kueleza kwamba katika suala la ndoa hataki kukurupuka na kuja kujutia baadaye.



Wakati kwa upande wa ratiba yake ya kila siku, amesema huwa mara nyingi analala saa tisa usiku na kuamka saa nne asubuhi na jambo la kwanza analofanya ni kusali kwani anaamini Mungu ndio kila kitu pamoja na kwamba kwake starehe ni kila siku.View attachment 1044853

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyu si ndiye RC wake alisema mtu wa hovyo kwenye mkutano wa mtendaji mwenzake
 
Back
Top Bottom