Tetesi: Mjumbe aliyetaka Samia na Hussein Mwinyi watoke kwenye kikao ili wawajadili aitwa kujieleza

mdukuzi

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2014
Posts
20,925
Reaction score
51,688
Mdomo uliponza kichwa.

Wazazi, pelekeni watoto shule. Huyu mjumbe wa mkutano mkuu, kama angekuwa amemaliza hata kidato cha nne kwa alama 31, angeelewa kwamba lile lilikuwa tu igizo.

Kikao kilikuwa kimepangwa vizuri, kila jambo likiwa limeandaliwa kwa mpangilio maalum, lakini mtoa hoja aliamua kwenda kinyume na mpango uliokuwepo.

Soma, Pia: Rais Samia aligoma alipoambiwa atoke ili wajumbe wapige kura na kumpitisha. Hii ina maanisha CCM wengi hawamtaki?

Nusura aharibu kabisa mwelekeo wa kikao.

Bahati nzuri, Steering Committee ilistukia haraka mchezo na kuchukua hatua za haraka kuzuia hali isiwe mbaya zaidi.

Ilikuwa ni hali ya hatari, hasa kama Mwenyekiti angeamua kuwapa nafasi wapinzani wa hoja hiyo. Ingekuwa balaa, kwani wapo ambao wangejitokeza kuipinga kwa nguvu hoja hiyo.

Kama hali hiyo ingekuwa imeachwa, Mwenyekiti angejikuta kwenye shinikizo kubwa, na huenda angeishia kuwa Rais wa muhula mmoja tu katika historia yetu.
 
Hata sasa anabaki kuwa Rais wa muhula mmoja tu
 
Huo mbona ni utaratibu wa kawaida na ushatumika awali?
 
mbona kuwa wa muhula moja uko palepale
 
wasije wakampa kesi y amauwaji tu au wasije wakampa sumu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…