KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,187
- 17,167
Bahati mbaya mbumbumbu hao sahizi wanakuwa miongoni mwa viongozi wa CCM. Sijui CCM itakuwaje siku za mbeleni kwa kuwajaza hawa wasio na akili waliotoka upinzani.
Uelewa wangu ni kuwa hadi sasa wengi wa hao wahamiaji ni wale waliohama toka huko wanakohamia sasa.Mwanzo wao ulikuwa ndani ya CCM.
Ndio, ninakubaliana kabisa na kuhoji 'integrity' ya viongozi hawa na wengi wengine waliomo ndani ya vyama hivi vya siasa. Tunaijua na kuikumbuka sana CCM ya Kikwete, hata ile ya Mkapa. Hawa watu ni walewale, hata kama sasa wamewekewa mfuniko wasisikike na kuonekana ndani ya CCM hii iliyopo sasa. Mfuniko ukiondolewa utaiona CCM halisi ya Kikwete na Mkapa. Hakuna kitakachokuwa kimebadilika.