tzcountry I love
JF-Expert Member
- Jul 28, 2018
- 729
- 641
Sasa nunueni na wananchi basi!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Siku hizi wameona hakuna umuhimu kununua wananchi, wananunua Polisi na ma DED basi. Kura wananchi wanachagua mgombea A wao wana tangaza mgombea B.Sasa nunueni na wananchi basi!
Huwezi kuwa malaya au kuitwa malaya kama au kabla hujafanya umalaya.JARIBU KUWA MTU MWENYE KUJENGA HOJA KWA KUSHIRIKISHA UBONGO usikurupuke kuandika.Kumbe mmejaza Malaya? Acha wanunuliwe maana ukienda kona bar ni kama uko Chadema unajichagulia Malaya unayemtaka.
Kila bidhaa ina tarehe yake ya kuingia na kusajiliwa.Naona chama kubwa wamesha-order bidhaa zao, kufikia December zitakuwa zimewasili. Ama kweli bishara ni kipaji.
Ni ulimbo uleule uliowavuta kina Ole Millya, Bulaya toka CCM kwenda chadema.HIVI WAKUU HAWA WABUNGE NA MADIWANI HAMAHAMA WANAVUTWA NA ULIMBO GANI AISEEE???
AU NDO VIWANDA TULIVYOAHIDIWA??THIS IS TOO MUCH ASEE
Gud analysis though. Still story za vijiweni zisikusumbue. Ushindi huamuliwa na wanaoenda kupiga kura sio wanaojua kuongea siasa. Ni wazi asilimia kubwa ya wananchi mijini kwa sasa wanapenda upinzani kuliko CCM but tofauti hiyo bado ni ndogo kuliko ilivyo tofauti Kati ya CCM na Upinzani huko vijijini. Kama mpaka Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2014, Vijiji vingi vilichukuliwa na CCM bila hata Upinzani kuweka Mgombea, hiyo inamaanisha nini?Ukiwatizama wapo happy,
That means inawezekana sio wote wanaohamia wameubga juhudi mkono. Yawezekana wengine kazi maalum. Lakini wangekuwa wameishiwa mbinu wangeanza kutumia misuli lakini inavyoonekana wanayo plan B na si ajabu na plan C.
Lakini pia tafiti ndio jibu sahihi kuweze kusema wameyumba au la. Tukitudi nyuma taasisi ya twaweza ilitoa report na kusema CCM wamepoteza mvuto kwa kiasi kikubwa nataasis hiyo imepigwa marufuku.
Hicho na mengine chaweza kuwa sababu inayoendelea kuwapa confidence.
Ukiangalia kwenye vijiwe, bar kwenye daladala na sehemu za kazi linapozungumziwa siasa utaona wengi wapo upande mmoja.
Kwetu pazuri
Wanaoweka uwanja sawa wa siasa siyo watawala bali ni wananchi. Siku wananchi wakiamua kuwa, kufanyike mabadiliko fulani ujue hakuna wa kuyazuia. Lakini ukiona jitihada kubwa za Upinzani kutaka kubadilisha vitu fulani lakini hawaungwi mkono na umma, basi ujue wabaya ni Wapinzani na wala siyo wananchi ambao hawajashawishika. An Organisation normally reflects the Society's behavior.Pamoja na kuchakachua lkn upinzani ulipata kura milioni sita. Unafikiri hawa ni raia wa nchi gani? Na unahisi maisha yameboreka sana kiasi kwamba sasa wanaitamani ccm. HEBU WEKENI UWANJA SAWA WA KUFANYA SIASA NDIYO UTAPATA MAJIBU KM HUYO MTU ANAKUBALIKA AU LA. ila alijua na anajua hana chake akirihusu harakati za siasa zishamiri km zamani na anajua bila hii tume ya uchaguzi, bila polisi, bila hili bunge kibogoyo ambalo ameliweka mfukoni hana lake hata humohumo ndani ya Ccm watamwondoa.
MIkutano ya kisiasa ipo kisheria /kikatiba ndicho nilichomaanisha .Wanatumia majeshi kuiharamisha.Kwani katiba iliyoruhusu kuwepo mikutano ya vyama vya siasa si mali ya wananchi? au kwako wewe katiba ni mali yanani.Mikutano ya siasa ni takwa la kikatiba.Kuwa mtu unaefikiri kabla ya kuandika.tumia akili .Nashangaa wewe unaniletea hoja za kipumbavu hapa.Wanaoweka uwanja sawa wa siasa siyo watawala bali ni wananchi. Siku wananchi wakiamua kuwa, kufanyike mabadiliko fulani ujue hakuna wa kuyazuia. Lakini ukiona jitihada kubwa za Upinzani kutaka kubadilisha vitu fulani lakini hawaungwi mkono na umma, basi ujue wabaya ni Wapinzani na wala siyo wananchi ambao hawajashawishika. An Organisation normally reflects the Society's behavior.
Kwahiyo chadema kuna watu wasio na akili?Kwa sasa siyo habari tena.
Jambo lililo wazi ni kuwa kumbe ndani ya vyama vya upinzani kumekuwa na wawakilishi wengi wasio na uelewa, waliokosa akili na sifa za uongozi. Sifa kubwa ya kiongozi ni kusimama juu ya yale unayoyaamini.
Bahati mbaya mbumbumbu hao sahizi wanakuwa miongoni mwa viongozi wa CCM. Sijui CCM itakuwaje siku za mbeleni kwa kuwajaza hawa wasio na akili waliotoka upinzani.
Tunawasubiri kwa hamu hao waliotajwa.View attachment 890013
Mjumbe wa Kamati ya Itikadi na Uenezi Mkoa wa Dar es Salaam, Frey Edward Cosseny, amewarusha tena roho juu wafuasi wa Vyama vya Upinzani baada ya kudai kuwa, kuna Wabunge wengine sita wanafuata baada ya Mbunge wa Simanjiro, James Ole Millya (CHADEMA) kujiunga na CCM.
Frey Cosseny amedai kuwa, Wabunge watakaojiunga na CCM kutokea CHADEMA ni wanatokea Mikoa ifuatvyo:
Mkoa wa Kilimanjaro - Wabunge wawili (02),
Mkoa wa Dar es Salaam - Wabunge wawili (02),
Mkoa wa Manyara - Mbunge mmoja (01),
Mkoa wa Mara - Mbunge mmoja (01).
View attachment 890012
Haya Wazee wenzangu wa mapovu camp, naomba tutiririke hapa kubashiri Wabunge hao walio mbioni.
Kwa Mkoa wa Mara nahisi Ester Matiko (Tarime Mjini) hatasalimika na hizi radar za CCM. Utakuwa ni usajili mzuri.
Tutaje wa Mikoa mingine.