Mr Dudumizi
JF-Expert Member
- Sep 9, 2020
- 7,799
- 14,215
Habari zenu wana JF wenzangu, bila kupoteza muda ngoja niende kwenye mada husika ili kuwarahisishia wasomaji wasiopenda kusoma maandishi mengi.
Ni hivi... baada ya mama mwenye nyumba kufanikiwa kukitia chama chake mwenyewe mfukoni, na kuwadhibiti wale wote waliokuwa na ndoto ya kutaka kupimana nae ubavu mwaka 2025, sasa amehamisha mikakati yake ya ushindi kwa viongozi wakuu wawili wa vyama vyetu vikuu vya upinzani.
Viongozi hao ambao ndio nguzo kuu ya vyama vyao, tayari wameshatengenezwa kimkakati na mmoja wao aliwahi kuitwa mara mbili katika lile jumba jeupe la taifa na kukabidhiwa bahasha yake kimya kimya kama ishara ya shukran kwa makubaliano yao waliofikia na mama huyo wa nyumba yetu pendwa.
Viongozi hao licha ya account zao kuvimbishwa ili kupata nguvu ya kukamilisha walichopanga, lakini pia walihakikishiwa ulinzi wa maisha yao, ulinzi wa familia zao, ulinzi wa mali zao na pia kufutiwa kesi zao nk.
Mkakati huo utatimiaje, sasa fuatilia vizuri kile ninachoandika hapo chini 👇
Ikumbukwe kwamba vyama vya upinzani vimekuwa vikiitaka serikali itengeneze katiba mpya ambayo wanahisi itaweza kuwasaidia wao kushinda chaguzi mbali mbali na hatimae na kushika dola. Lakini kwa upande mungine pia wanaitaka serikali iifumue tume iliyopo na kuunda tume nyingine "huru" ambayo itawashirikisha wadau wote kwa ukaribu zaidi.
Kwahiyo sasa haya mambo mawili ya "katiba" na "tume huru" ndio yatakayotumiwa na wasukaji wa mpango huo kama kichochoro cha kutimiza mikakati ya ushindi wa mama huyo mwenye nyumba.
Inasemekana kitachofanyika ni kwamba serikali itaendelea na msimamo wake wa kutokuwa tayari kutengeneza katiba mpya wala kuunda tume huru, baada ya hapo kiongozi mmoja "mlamba asali mkongwe" wa upinzani atajifanya kuchukizwa na hali hiyo, kisha atatumia uwezo wake na madaraka yake makubwa katika chama kuwashawishi wenzake ambao asilimia kubwa ameshawatia mfukoni, kwamba wasusie uchaguzi wowote utakaofanyika nchini.
Wakishakubaliana kususia inamaana ushindani wa vyama vingine vya upinzani vilivyopo utakuwa mdogo sana hivyo kumpa mama mwenye nyumba fursa ya kuendelea kutawala yeye na bunge lake kama ilivyo sasa.
Yule kiongozi mungine ambae anatokea katika mkoa uliyopo pembezoni mwa ziwa fulani, atabaki kupewa nafasi ya kubwabwaja bwabwaja pale inapobidi ili kuwafunga macho wale wasiojua kile kinachoendelea katika siasa za nyumbani kwetu.
Dalili za mipango hiyo zimeshaanza kuonekana kwa viongozi hao kutia zip midomo yao, na mmoja wao kufikia hatua ya kwenda kumfagilia mama mwenye nyumba huko katika dunia ya kwanza.
Hii mada ni kwa ajili ya wale watu ambao wako huru kifikra na ki akili, wale ambao wanaona mbali na hawana mihemko ya kisiasa.
Hakika "moyo wa mtu msitu", unachokipanga wewe, sio kile anachokipanga mwenzio. Wakati kuna chawa wanashinda mitandaoni kuwapigania, kuwasifia na kuwafagilia viongozi wao wa vyao, wao wanaopiganiwa, wanaofagiliwa na kusifiwa wako busy kulamba asali kimya kimya na kutelekeza mipango ya vyama vyao kiaina.
Jioni njema wakuu. 🙏