Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hii itabadili nini?
Wai. Bora kupigania katiba mpya. Huu mpango wako labda usubiri wajukuu.Itaondoa uhalali wa umma wa walioko madarakani bila ridhaa yao. Hii itatoa mwanya hata wa mapinduzi kwani watajua hata walioko madarakani hawako kwa ridhaa ya umma.
Wai. Bora kupigania katiba mpya. Huu mpango wako labda usubiri wajukuu.
Katiba mpya ndo jambo la msingi mkuuNiko tayari kusubiri wajukuu boss, kuliko kwenda kupoteza muda kwenye mstari wa kura. Na ndio maana mimi ni mdau wa katiba mpya na sio huo upuuzi uitwao uchaguzi kwa tume na katiba hii.
Siku wananchi wakigundua wao ndio wenye mammlaka ya kuweka kiongozi wamtakae. Mambo yatabadilikaHabari zenu wana JF wenzangu, bila kupoteza muda ngoja niende kwenye mada husika ili kuwarahisishia wasomaji wasiopenda kusoma maandishi mengi.
Ni hivi... baada ya mama mwenye nyumba kufanikiwa kukitia chama chake mwenyewe mfukoni, na kuwadhibiti wale wote waliokuwa na ndoto ya kutaka kupimana nae ubavu mwaka 2025, sasa amehamisha mikakati yake ya ushindi kwa viongozi wakuu wawili wa vyama vyetu vikuu vya upinzani.
Viongozi hao ambao ndio nguzo kuu ya vyama vyao, tayari wameshatengenezwa kimkakati na mmoja wao aliwahi kuitwa mara mbili katika lile jumba jeupe la taifa na kukabidhiwa bahasha yake kimya kimya kama ishara ya shukran kwa makubaliano yao waliofikia na mama huyo wa nyumba yetu pendwa.
Viongozi hao licha ya account zao kuvimbishwa ili kupata nguvu ya kukamilisha walichopanga, lakini pia walihakikishiwa ulinzi wa maisha yao, ulinzi wa familia zao, ulinzi wa mali zao na pia kufutiwa kesi zao nk.
Mkakati huo utatimiaje, sasa fuatilia vizuri kile ninachoandika hapo chini 👇
Ikumbukwe kwamba vyama vya upinzani vimekuwa vikiitaka serikali itengeneze katiba mpya ambayo wanahisi itaweza kuwasaidia wao kushinda chaguzi mbali mbali na hatimae na kushika dola. Lakini kwa upande mungine pia wanaitaka serikali iifumue tume iliyopo na kuunda tume nyingine "huru" ambayo itawashirikisha wadau wote kwa ukaribu zaidi.
Kwahiyo sasa haya mambo mawili ya "katiba" na "tume huru" ndio yatakayotumiwa na wasukaji wa mpango huo kama kichochoro cha kutimiza mikakati ya ushindi wa mama huyo mwenye nyumba.
Inasemekana kitachofanyika ni kwamba serikali itaendelea na msimamo wake wa kutokuwa tayari kutengeneza katiba mpya wala kuunda tume huru, baada ya hapo kiongozi mmoja "mlamba asali mkongwe" wa upinzani atajifanya kuchukizwa na hali hiyo, kisha atatumia uwezo wake na madaraka yake makubwa katika chama kuwashawishi wenzake ambao asilimia kubwa ameshawatia mfukoni, kwamba wasusie uchaguzi wowote utakaofanyika nchini. Wakishakubaliana kususia inamaana ushindani wa vyama vingine vya upinzani vilivyopo utakuwa mdogo sana hivyo kumpa mama mwenye nyumba fursa ya kuendelea kutawala yeye na bunge lake kama ilivyo sasa.
Yule kiongozi mungine ambae anatokea katika mkoa uliyopo pembezoni mwa ziwa fulani, atabaki kupewa nafasi ya kubwabwaja bwabwaja pale inapobidi ili kuwafunga macho wale wasiojua kile kinachoendelea katika siasa za nyumbani kwetu.
Dalili za mipango hiyo zimeshaanza kuonekana kwa viongozi hao kutia zip midomo yao, na mmoja wao kufikia hatua ya kwenda kumfagilia mama mwenye nyumba huko katika dunia ya kwanza.
Hii mada ni kwa ajili ya wale watu ambao wako huru kifikra na ki akili, wale ambao wanaona mbali na hawana mihemko ya kisiasa.
Hakika "moyo wa mtu msitu", unachokipanga wewe, sio kile anachokipanga mwenzio. Wakati kuna chawa wanashinda mitandaoni kuwapigania, kuwasifia na kuwafagilia viongozi wao wa vyao, wao wanaopiganiwa, wanaofagiliwa na kusifiwa wako busy kulamba asali kimya kimya na kutelekeza mipango ya vyama vyao kiaina.
Jioni njema wakuu 🙏
...hakuna ulichoongeza. mengi yanajulikana. Utaeleweka. Ila umepindisha kudai ni 'Wapinzani" wanaotaka Katiba mpya! Hapana.Ok nimekuelewa mkuu, huenda aina ya uandishi wangu umekufanya uone kama kuna kitu nimeongeza.
Mtu anashindwa kujiuliza kama amenunulika sa hivi kwa nini Magu alishindwa kumnunua wakati mwendazake alikuwa anatembeza bahasha kwa madiwani na wabunge.
Mkuu mi natafuta pesa,siasa sitaki kujishirikisha.Moja ya mbinu zao ni hiyo ya kuwatumia wachumia tumbo wakubwa wa vyama vya upinzani.
Kama unafikiria kuwa kuna mpinzani au mwanasiasa ambae atakukomboa ujue unajidanganya sana.
Kufuatilia au kujishirikisha kwenye siasa za Tanzania ni sawa na kujitengenezea stress za kudumu katika maisha yako.Mkuu mi natafuta pesa,siasa sitaki kujishirikisha.
Mungine kaenda Marekani juzi na kuutangazia umma kwamba safari yake imefanikiwa kwa msaada wa mama mwenye nyumba, yani mama mwenye nyumba tunaemzungumzia hapa ndio huyo aliedhamini safari ya jamaa. Huyo wa act yeye ndo kabisa haungoji kuuliza maana vitendo vinajieleza.Ha haa. ATCL wamekuja juu wakihoji; mbona Zito amekuwa mzito kuzungumzia juu ya mazito yanayoikabili nchi yetu? Kama vile mgao wa umeme n.k.
Inaonekana Zito ni mzito wa kula na wenzake!