To yeye
JF-Expert Member
- Oct 4, 2022
- 35,686
- 86,968
Inachosha sana
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Inachosha sana
Hapa dawa ya viongozi njaa wa upinzani Ni
Kumuomba Mungu Dr Slaa Arudi Chadema
Kwa kushtukiza Hapo 2025 mwanzoni.Na Halafu aruhusiwe kugombea Urahisi kupitia upinzani.PATAMU HAPO NAKWAMBIA.
Wanachoboa wale watu ni ile kususa susa aisee.
Kuna time unataman kuwafatilia sera zao, usimame nao kwenye uchaguzi, mara paam wamesusa.
Sijui kususa kunawanufaishaje.
Umeandika UWONGO ulioratibiwa vizuri uonekane kama KWELI.Habari zenu wana JF wenzangu, bila kupoteza muda ngoja niende kwenye mada husika ili kuwarahisishia wasomaji wasiopenda kusoma maandishi mengi.
Ni hivi... baada ya mama mwenye nyumba kufanikiwa kukitia chama chake mwenyewe mfukoni, na kuwadhibiti wale wote waliokuwa na ndoto ya kutaka kupimana nae ubavu mwaka 2025, sasa amehamisha mikakati yake ya ushindi kwa viongozi wakuu wawili wa vyama vyetu vikuu vya upinzani.
Viongozi hao ambao ndio nguzo kuu ya vyama vyao, tayari wameshatengenezwa kimkakati na mmoja wao aliwahi kuitwa mara mbili katika lile jumba jeupe la taifa na kukabidhiwa bahasha yake kimya kimya kama ishara ya shukran kwa makubaliano yao waliofikia na mama huyo wa nyumba yetu pendwa.
Viongozi hao licha ya account zao kuvimbishwa ili kupata nguvu ya kukamilisha walichopanga, lakini pia walihakikishiwa ulinzi wa maisha yao, ulinzi wa familia zao, ulinzi wa mali zao na pia kufutiwa kesi zao nk.
Mkakati huo utatimiaje, sasa fuatilia vizuri kile ninachoandika hapo chini 👇
Ikumbukwe kwamba vyama vya upinzani vimekuwa vikiitaka serikali itengeneze katiba mpya ambayo wanahisi itaweza kuwasaidia wao kushinda chaguzi mbali mbali na hatimae na kushika dola. Lakini kwa upande mungine pia wanaitaka serikali iifumue tume iliyopo na kuunda tume nyingine "huru" ambayo itawashirikisha wadau wote kwa ukaribu zaidi.
Kwahiyo sasa haya mambo mawili ya "katiba" na "tume huru" ndio yatakayotumiwa na wasukaji wa mpango huo kama kichochoro cha kutimiza mikakati ya ushindi wa mama huyo mwenye nyumba.
Inasemekana kitachofanyika ni kwamba serikali itaendelea na msimamo wake wa kutokuwa tayari kutengeneza katiba mpya wala kuunda tume huru, baada ya hapo kiongozi mmoja "mlamba asali mkongwe" wa upinzani atajifanya kuchukizwa na hali hiyo, kisha atatumia uwezo wake na madaraka yake makubwa katika chama kuwashawishi wenzake ambao asilimia kubwa ameshawatia mfukoni, kwamba wasusie uchaguzi wowote utakaofanyika nchini.
Wakishakubaliana kususia inamaana ushindani wa vyama vingine vya upinzani vilivyopo utakuwa mdogo sana hivyo kumpa mama mwenye nyumba fursa ya kuendelea kutawala yeye na bunge lake kama ilivyo sasa.
Yule kiongozi mungine ambae anatokea katika mkoa uliyopo pembezoni mwa ziwa fulani, atabaki kupewa nafasi ya kubwabwaja bwabwaja pale inapobidi ili kuwafunga macho wale wasiojua kile kinachoendelea katika siasa za nyumbani kwetu.
Dalili za mipango hiyo zimeshaanza kuonekana kwa viongozi hao kutia zip midomo yao, na mmoja wao kufikia hatua ya kwenda kumfagilia mama mwenye nyumba huko katika dunia ya kwanza.
Hii mada ni kwa ajili ya wale watu ambao wako huru kifikra na ki akili, wale ambao wanaona mbali na hawana mihemko ya kisiasa.
Hakika "moyo wa mtu msitu", unachokipanga wewe, sio kile anachokipanga mwenzio. Wakati kuna chawa wanashinda mitandaoni kuwapigania, kuwasifia na kuwafagilia viongozi wao wa vyao, wao wanaopiganiwa, wanaofagiliwa na kusifiwa wako busy kulamba asali kimya kimya na kutelekeza mipango ya vyama vyao kiaina.
Jioni njema wakuu. 🙏
Hata kabla ya uchaguzi mkuu wa 2020 CDM ilijifanya kususa ili kuwaaminisha watu kuwa hawatoshiriki uchaguzi mkuu. Lakini kwa vile hapakuwa na deal lolote sisi wenye akili hatukuandika haya tukiamini kuwa CDM ni lazima ingeshiriki.
Lakini huu uchaguzi wa 2025 nimeandika kwa sababu najua haitoshiriki kweli kutokana na mpango uliosukwa kati ya mama mwenye nyumba na kigogo mkuu wa chama hicho.
Huenda wewe unaebisha ndio muhusika mwenyewe ila humu unatumia ID tofauti tofauti na kujifanya kubishana na mada yangu ili kuendelea kuwarubuni wanachama wako wasijue kinachoendelea.
Lakini pia KATIBA mpya haidaiwi Kwa njia SOFT pekee, tutapita NJIA ngumu pia ikibidi anazoongelea TINDO.Katiba mpya ndo jambo la msingi mkuu
Kwa aina hii ya viongozi wa upinzani butu tuliokuwa nao, CCM bado iko madarakani kwa zaidi ya miaka 50 ijayo kama alivyosema Lowasa katika uchaguzi mkuu wa 2015.
CCM imewahi kupitisha nchi kwenye hali ngumu, kwa sasa mambo si magumu, nchi itapita kwa wepesi tu.Kama leo 2022 tumefilisika, je 2025 itakuwaje?.
Fikirieni kulipa madeni na kupunguza matumizi. Ni aibu mishahara kulipwa kwa mikopo.
Kiongozi yeyote wa chama chochote atakayekubali kushiriki uchaguzi bila katiba mpya na bila Tume huru huyo ni wa kupiga maweMoja ya mbinu zao ni hiyo ya kuwatumia wachumia tumbo wakubwa wa vyama vya upinzani.
Kama unafikiria kuwa kuna mpinzani au mwanasiasa ambae atakukomboa ujue unajidanganya sana.
upinzani una muda wa nini sasa? Na unapinzana na kitu ganiupinzan hauna mda wa kupigania mapumbavu ya tanzania yasiyojielewa.
Alieshindwa kununulika ni yule aliepigwa risasi tu peke yake, lakini huyu ninaemzungumzia hapa amenunulika kiurahisi toka 2015 kupitia kwa Lowasa ndomaana yuko hai mpaka leo hajaguswa hata na wembe.
Habari za mashamba na club bilkanas ni porojo tu za kuwahadaa watu kama nyinyi msiojiongeza kufikiri.
Tatizo vyama vyao vinaongozwa na makada wa kile kitengo cha wasiofahamika. Kwahiyo inapoonekana kuwa kuna uchaguzi ambao utakuwa mgumu kwa chama tawala kushinda, basi wazee wa kitendo wanawashtua wa vitengo wenzao wanaoongoza vyama hivyo watengeneze mgomo (wasuse) utakaosababisha chama tawala kipate ushindi mnono na hivyo kuendelea kutawala nchi yetu.
Nchi haijawahi pitia ukopaji Holela na deni kufika TRI Zaid ya 90,CCM imewahi kupitisha nchi kwenye hali ngumu, kwa sasa mambo si magumu, nchi itapita kwa wepesi tu.
Unamaanisha kwamb Nyerere ndie aliejenga mfumo wa vyama vya upinzani unaoongozwa na wachumia tumbo?
Ama kweli mtamtupia Nyerere kila aina ya lawama hata zile ambazo zinasabishwa na viongozi wenu wa vyama, kisa tu kukwepa kuwakosoa na kuwaambia ukweli.
Katika watu ambao waliichukia CCM miaka mingi iliyopita mimi ni mmoja wao. Lakini sasa kutokana na siasa za aina ya vyama vyetu vya upinzani pamoja na wapinzani wenyewe, inafika mahala mtu unaona bora tu usiwe upande wowote wa chama, na ikiwezekana uwe shabiki wa mtu yeyote unaeona kwamba anaweza kuleta ukombozi wa kweli ndani ya nchi bila kujali chama alichopo ni CCM, CDM au ACT wazalendo.CCM itaondolewa na wananchi wenyewe wakiichoka. Siku madeni yatakapoielemea na kushindwa kulipa mishahara ndipo utajua wenye nchi ni akina Nani. CCM haina jipya. Sasa hivi wanafanya maamuzi kwa mitandao.
upinzani una muda wa nini sasa? Na unapinzana na kitu gani
Na ndio maana uozo wa CCM ili ukomeshwe ni lazima ifumuliwe kutokea ndani na sio upinzani njaa wa chadema na ACT rejea "Trojan Horse".#njaahainabaunsa
Chadema wanataka katiba mpya ipi ikiwa ya kwao wenyewe imewashinda?Upinzani unapigania kubadilisha mfumo wa nchi. Ndio maana CHADEMA wanataka katiba mpya. Sio Sasa hivi serikali inakopa kulipa mishahara.
Nina uhakika mzee wa ubwabwa ataingia ulingoni kupimana ubavu na mama mwenye nyumba.Kiongozi yeyote wa chama chochote atakayekubali kushiriki uchaguzi bila katiba mpya na bila Tume huru huyo ni wa kupiga mawe