Mkakati wa mama mwenye nyumba kushinda uchaguzi mkuu wa 2025 kwa 95% huu hapa umeshawiva tayari

Umeandika UWONGO ulioratibiwa vizuri uonekane kama KWELI.

Kweli ni kuwa Mmebutuliwa kwenye CC, safu mlopanga imevurugwa.

Karibu tupambanie KATIBA mpya itokanayo na Rasimu alosimamia Judge WARIOBA.

Aamen
 

Acha umuch know. Mbona hawakushiriki 2019 walijitoa wote. Cha msingi upinzani wasishiriki huo uchaguzi wananchi wengi watawaunga mkono.
 
Kwa aina hii ya viongozi wa upinzani butu tuliokuwa nao, CCM bado iko madarakani kwa zaidi ya miaka 50 ijayo kama alivyosema Lowasa katika uchaguzi mkuu wa 2015.

CCM itaondolewa na wananchi wenyewe wakiichoka. Siku madeni yatakapoielemea na kushindwa kulipa mishahara ndipo utajua wenye nchi ni akina Nani. CCM haina jipya. Sasa hivi wanafanya maamuzi kwa mitandao.
 
Kama leo 2022 tumefilisika, je 2025 itakuwaje?.

Fikirieni kulipa madeni na kupunguza matumizi. Ni aibu mishahara kulipwa kwa mikopo.
CCM imewahi kupitisha nchi kwenye hali ngumu, kwa sasa mambo si magumu, nchi itapita kwa wepesi tu.
 
Moja ya mbinu zao ni hiyo ya kuwatumia wachumia tumbo wakubwa wa vyama vya upinzani.
Kama unafikiria kuwa kuna mpinzani au mwanasiasa ambae atakukomboa ujue unajidanganya sana.
Kiongozi yeyote wa chama chochote atakayekubali kushiriki uchaguzi bila katiba mpya na bila Tume huru huyo ni wa kupiga mawe
 

. Serikali inayotumia Kodi za wananchi kulipa wapinzani lakini mishahara hailipi hiyo ni serikali ya matahira.
 
Wad
Halafu watu watakuamini. Eti vitengo. Upinzani upo daima, Hakuna wa kuuzima labda Mungu mwenyewe.
 

Shida yako ni upinzani? Wanachunia Tumbo wapi?. Wanalipwa shilingi ngapi na Nani?. Yani serikali inayodaiwa Trilioni 94 Sasa hivi, inapata wapi pesa za kuwalipa wapinzani?. Huoni unitukanisha serikali ya CCM.
 
CCM itaondolewa na wananchi wenyewe wakiichoka. Siku madeni yatakapoielemea na kushindwa kulipa mishahara ndipo utajua wenye nchi ni akina Nani. CCM haina jipya. Sasa hivi wanafanya maamuzi kwa mitandao.
Katika watu ambao waliichukia CCM miaka mingi iliyopita mimi ni mmoja wao. Lakini sasa kutokana na siasa za aina ya vyama vyetu vya upinzani pamoja na wapinzani wenyewe, inafika mahala mtu unaona bora tu usiwe upande wowote wa chama, na ikiwezekana uwe shabiki wa mtu yeyote unaeona kwamba anaweza kuleta ukombozi wa kweli ndani ya nchi bila kujali chama alichopo ni CCM, CDM au ACT wazalendo.

Mtu huyo awe mkweli, awe mpenda haki, awe mpenda maendeleo na mabadiliko ya kiuchumi, awe mwenye maono, asiwe na kashfa ya aina yoyote ndani ya chama au nchi kwa ujumla.

Kwa sasa ndani ya vyama vyetu vya siasa vyote hayupo mtu huyo, na kama yupo basi bado hajaanza kujulikana.
 
Upinzani unapigania kubadilisha mfumo wa nchi. Ndio maana CHADEMA wanataka katiba mpya. Sio Sasa hivi serikali inakopa kulipa mishahara.
Chadema wanataka katiba mpya ipi ikiwa ya kwao wenyewe imewashinda?
Je wakiingia madarakani na kuirudisha hii iliyopo ili imnufaishe mwenyekiti na genge lake kama alivyofanya kwa katiba ya chama chake ni nani atamzuia?
 
Kiongozi yeyote wa chama chochote atakayekubali kushiriki uchaguzi bila katiba mpya na bila Tume huru huyo ni wa kupiga mawe
Nina uhakika mzee wa ubwabwa ataingia ulingoni kupimana ubavu na mama mwenye nyumba.
Huyu mzee vituko vyake huwa namfananisha na hayati Mtikila 🤣🤣🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…